USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Marais wa awamu ya Pili hadi ya Tano wamehudhuria hapa mama maria nyerere yupo hapa pia kama mke wa mwasisi wa Taifa hili
Mh Rais amewazawadia marais wastafu zawadi ya ndege tausi 25 kila mmoja pamoja na hati za umiliki wa ndege hao, mc wa sherehe anasema tunao tausi zaidi ya 2800+
Ikulu ya Chamwino ndio Ikulu Kubwa kwa eneo kuliko Ikulu yoyote Duniani
Ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la Ikulu ni mkubwa kuliko ule wa Mirerani
Kuna mpango wa kuifanya Ikulu ya Chamwino kuwa na mbuga ya wanyama
Ikulu hii tayari inao baadhi ya wanyama wa kuanzia
Kikwete:
Makongoro:
Mzee Mwinyi:
===
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Mei 30, 2020 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ikulu mpya ya Chamwino jijini Dodoma, zoezi lililohudhuriwa na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete sambamba na viongozi wengine wa sasa na wastaafu.
Aidha, katika kufafanua jambo hilo Rais Magufuli amesema wakati anapokea Uenyekiti wa CCM, Julai 2016 aliahidi kwa kipindi cha miaka mitano angehakikisha Serikali yote inahamia Dodoma lakini hakuwa na uhakika kama kwa muda huo angefanikiwa na ila anafaraja sana kwani ametekeleza ahadi hiyo.
Sambamba na hilo, Rais Magufuli ameeleza kuwa Ikulu ya Chamwino ndio Ikulu Kubwa kwa eneo kuliko Ikulu yoyote Duniani. Ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la Ikulu ni mkubwa kuliko ule wa Mirerani. Hivyo, Kuna mpango wa kuifanya Ikulu ya Chamwino kuwa na mbuga ya wanyama Ikulu hii tayari inao baadhi ya wanyama wa kuanzia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Marais Wastaafu katika harakati za uwekaji wa jiwe la msingi.
Sambamba na hilo pia katika hafla hiyo, Rais John Magufuli amewakabidhi ndege aina ya Tausi 25 kila mmoja kwa Marais mstaafu wa nchi hii, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere ambapo Mama Maria amepokea kwa niaba ya mumewe.
Aidha, Wastaafu wote wamezungumza kwenye hafla hiyo, huku mama Maria akiwakilishwa na mwanaye Makongoro Nyerere na kwa pamoja wamemshukuru Mheshimiwa Rais.