Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Mimi pia ni mdau wa Ile Kanuni isemayo kuwa Watu wote ni Sawa Mbele ya sheria, ikiwa ni nguzo muhimu kwenye Rule of law. Yaani kila mtu anapaswa kuwajibika Mbele ya sheria na hakuna ambaye atakuwa juu ya sheria.
Lakini tukija kwenye Falsafa na uhalisia Kanuni hiyo sio halisi, haiko Logically. Kusema Watu wote wawe Sawa Mbele ya sheria ni kauli janjajanja, kauli za kisiasa zinazotumiwa na viongozi kuwalaghai Watu wa kawaida.
Ulimwengu, Una nguvu zake ambazo zinazalisha vijinguvu vidogovidogo kulingana na uhitaji.
Hata hivyo nguvu zimegawanyika katika makundi makuu manne;
1. Nguvu ya Nishati
2. Nguvu ya AKILI (Utashi)
3. Nguvu ya Imani
4. Nguvu ya vitu vilivyopewa thamani na wenye Akili na Imani.
Mwenye nguvu ndiye anayetunga sheria. Hapo ndipo Rule of Law inapoanza kupoteza mwelekeo.
Nguvu ndio inayozalisha Mamlaka.
Ikiwa Mwenye nguvu ndiye anayetunga sheria hapo automatically yeye yupo juu ya Sheria.
Nguvu hutunga sheria zitakazolinda nguvu zake.
Sheria haziwalindi Watu wanyonge, makabwela au mabwege,
Taikon ninapoingia kwenye migogoro na MTU yeyote, cha Kwanza ni lazima niangalie nguvu na mamlaka ya MTU huyo Kabla sijaamua Jambo lolote katika kukabiliana naye. Ukishajua Fulani amekuzidi nguvu za kimamlaka tafsiri yake MTU huyo kisheria hautamuweza.
Zipo Njia zingine za kudili na MTU ambaye amekuzidi kimamlaka na kinguvu kuliko Kutumia sheria ambazo kimsingi hautawezana naye.
Mamlaka huheshimu Mamlaka.
Kama huna mamlaka huwezi kuheshimiwa na wenye mamlaka. Hiyo kiasili haipo hivyo.
Ili mamlaka ikuheshimu lazima uwe na mamlaka zingine ndani yako. Mfano ili viongozi wa kisiasa wa kuheshimu basi itakupasa uwe aidha na nguvu au mamlaka ya kiimani, labda ni Kuhani, Nabii, sheikhe, mtume, au mganga uliyebobea mwenye uwezo wa Hali ya juu.
Au uwe na kipaji kikubwa na ambacho kimewatiisha Watu wengi Mbele yako. Kwa mfano Uwe Mwanamuziki wa kiwango cha juu kama kina Diamond Kwa hapa nchini, au mwanasoka mkubwa kama Ronaldo.
Au uwe na utajiri au Mali ambazo Watu wengi WA kawaida Hawana.
Ukiwa bwege bwege elewa sheria haitakuwa upande wako. Ingawaje watakufanyia unafiki ili ujione nawe unaheshimiwa. Sheria haitakuwa upande wako Kwa sababu haikutungwa kulinda Watu wadhaifu.
Mungu Mtawala na mwenye uweza na mwenye nguvu na mamlaka yote, hata sheria alizoziweka za Asili na zile ambazo alizikasimisha Kwa wanadamu au viumbe wengine ambao watatawala aliunda sheria zinazomlinda yeye mwenyewe.
Mimi na wewe hatuwezi kuwa MUNGU Sio Kwa sababu tuliumbwa nop! Bali ni Kwa sababu tuliwekewa sheria(mipaka) ili tubaki kuwa hivi tulivyo.
Taikon ninaamini kuwa Nguvu hutumia nguvu zingine ili izidi kuwa na nguvu. "Power use other powers to become stronger".
Sio ajabu kuona Mwanasiasa kuungana na matajiri, au watu maarufu ili kuimarisha nguvu zake. Ni Jambo ambalo MTU yeyote mwenye Akili lazima alifanye ili kustawi na kuongezeka.
Kuungana na wanyonge sio tuu kunakupunguzia nguvu Bali pia kunakuangusha Kwa hakika.
Sisemi Watu wasiungane na watu dhaifu, au wanyonge, na mabwege. Nop! Hapa nipo kuzungumzia ukweli na uhalisia wa mambo.
Ukiwa kama mwenye nguvu, ili nguvu zako zidumu Kwa muda mrefu basi itakupasa ujue namna ya kuzitumia nguvu za wenye nguvu wengine. Kisha ujue namna ya kuzishusha pasipo zenyewe kujua zinashushwa, polepole Kwa uhakika.
Ukiwa mtu dhaifu haitakuwa mbinu njema kupambana na wenye nguvu ikiwa wewe unataka kuwa na nguvu kama wao. Kwani Kwa hakika utaanguka na kushindwa tuu. Njia maalumu yenye matokeo yenye tija ni Kutumia nguvu za wenye nguvu ili kuongeza nguvu zako. Wamarekani wao husema " if you can't beàt them join them"
Acha nimalize Kwa kukuambia, Watu hawatumii vitu dhaifu kuwashinda wenye nguvu Bali hutumia vitu vyenye nguvu kuwashinda wenye nguvu au Kupata ñguvu.
Huwezi ipata nguvu Kwa Kutumia Watu wadhaifu au wanyonge, Ila waweza Kupata ñguvu Kwa Watu wenye nguvu ikiwa utawashawishi au utachukua nguvu zao.
Hii ni tofauti na MUNGU muweza wa yote. Yeye hutumia Watu au vitu dhaifu kuvipiga vile vitu au wale Watu wenye Nguvu. Hizo ni Kanuni Ndugu zangu.
Kwa mtakaoona ni useful haya chukueni, Kwa wale mtaoona ni takataka au nadharia zisizo na uhalisia puuzieni.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam