Sheria inasemaje kuhusu Tundu Lissu Kwenda kwenye mazishi ya kaka yake?

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Baada ya taarifa za leo kwamba kaka yake Tundu Lissu amefariki dunia, naomba ufafanuzi kutoka kwa wajuzi wa sheria: Sheria inasemaje kuhusu mahabusu kuruhusiwa kwenda kuhudhuria au kushiriki mazishi ya ndugu yake wa karibu?

Katika mazingira haya, Tundu Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini, huku tarehe 6 Novemba ikitajwa kuwa tarehe muhimu katika mwenendo wa kesi hiyo.

Naomba msaada na ufafanuzi wa kisheria kuhusu iwapo mahabusu anaweza kuruhusiwa, chini ya ulinzi, kwenda kumzika au kuhudhuria mazishi ya ndugu yake wa karibu.

Soma pia :Wakili Alute Lissu Mughwai (kaka wa Tundu Lissu) afariki Dunia
 
Nchi huwa haimtungii mtu mmoja sheria, hatuna sheria inayohusu familia ya Lissu.
 
Hivi, Tanzania ina sheria?Zinafuatwa?Ninavyoona,kuna watu wamejifanya ndiyo sheria zenyewe.Kama sheria-mama inaitwa kajitabu,hizo zingine zitaheshimiwa kweli?
 
R.I.P Alute.

halafu,
wale majamaa wafuata mkumbo wa kushangilia vifo vya watu mbona hawaonekani leo?
 
Kwa mwana familia inaruhusuwa hata akiwa na pingu
 
Mahakama imalizane na Chiba kesho ili tuunganishe na hii kupunguza gharama. Nyumbu hoyeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…