Sheria inasemaje kuhusu Tundu Lissu Kwenda kwenye mazishi ya kaka yake?

Nimekumbuka Kabendera na msiba wa mama yake
 
Hatuna sheria inayohusu familia ya Lissu, nielewe.

Bado unajibu hoja kiwendawazimu! Unaulizwa kama kuna shetia inaruhusu mahabusu kuhudhuria msiba wa mwanafamilia, badala ya kujibu swali, unaleta uwendawazimu wako! Kama huna jibu, au hufahamu, si ukae kimya ujifunze kutoka kwa wenye ufahamu watakapotoa jibu la swali lililoulizwa?
 
Sidhani kama ipo Tanzania. Kabendera alifiwa na mama yake tena kesi yake haikuwa kubwa kama ya Lisu lakini hakwenda kumzika mama yake.
 
Mbona umejibu kama huna akili timamu!! Mleta mada ameuliza sheria au kanuni zinasemaje, wewe unajibu kwa upunguani mkubwa wa akili! Ina maana huna hata akili ya kuweza kuelewa swali?
Yaani hata mimi nimeshangaa!
 
Lissu siyo mfungwa kabla ya hukumu.
Mahabusu kuna sheria yao tofauti na mfungwa.
OP anahoji uwepo wa sheria inayoweza kumpa ruhusa ya kwenda kushiriki kumzika ndugu wa mahabusu.
Ndo ungesaidia kuiweka hiyo sheria nasi tuijue mkuu.
 
Hilo lipo chini ya mahakama kama atahitaji kwenda kumzika basi yampasa kupeleka maombi mahakamani (Application under Certificate of Urgency) ili aruhusiwe kwenda kumzika
 
Maendeleo yafaa Nini ikiwa Kuna watu wanaishi kama watumwa kwenye nchi inajinadi ni kidemokrasia.
 
Ibara ya 13 (6) b ya katiba inatoa presumption of innocence
"Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo."
Hii inahusikaje na kupata ruhusa ?
Hebu tusaidie kuifafanua mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…