Sheria inataka Waziri wa Ulinzi ateuliwe baada ya muda gani, au hata asipokuwepo sawa tu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Je, Kuna sheria inayomtaka Rais kuteua Waziri wa Ulinzi baada ya muda fulani pale anapotenguliwa, kuacha uwaziri au kufariki?

Kama hakuna sheria je Kuna ulazima wa kuwa na Waziri wa Ulinzi? Na je Nini kilimsukuma JPM kuteua Waziri wa sheria Mara tu Mzee Maiga alipofariki?
 
Mawaziri husimamia sera na siyo wataalam.
Kuwepo au kutowepo kwa waziri hakusimamishi utendaji wa siku kwa siku wa serikali.
Wizara zaweza kupunguzwa au kuongezwa wakati wowote na hakuna badiliko litakaloathiri moja kwa moja huduma kwa wananchi.
 
Hapa kwetu hata pasipokuwepo na baraza la mawaziri na hata wabunge sawa tu!!!sasa kuna maana gani tozo/sheria zinapitishwa , watu hawajui, zikianza kutumika tu wananchi wapoanza kupiga kelele!!ndio nao wanaibuka na kuanza kushangaaa "ETI JAMAANI HILI LILIPITAJE HUMU BUNGENI"
 

JIWE aliwahi kusema waziri wa ulinzi hana umuhimu kwakua CDF akiwa na shida anaweza kuwasiliana na Rais moja kwa moja
 
KWA sasa tunaishi na siro mzee wa double standard 😳
 
Mbona mnashupalia sana hili...!!!??
Kwani hata asipokuepo wewe inakupunguzia nini!??
 
Huenda mama Samia anatengeneza mkeka wa Mawaziri wengine .
Hawa akina Doroth Gwajima mhhh hawatatufikisha kwenye maendeleo.
 
Mbona mnashupalia sana hili...!!!??
Kwani hata asipokuepo wewe inakupunguzia nini!??
Hii mitandao ipo kwa ajili ya watu kukutana nakujadili au kufahamishana mambo mbalimbali.hayo ya kijinga ya kushupalia baki nayo mwenyewe.
 
Ni vitu vichache sana katiba imemshinikiza Rais, mambo mengi anafanya bila shinikizo. Hakuna ukomo wa muda wa kuteua waziri wa kawaida, kuna sharti kwenye uteuzi wa Waziri Mkuu
 
Haya mambo tusiyachukulie juu juu yana msukumo mkubwa sana kiroho.. Hiki kitete sio cha bure na hakuna anayeweza kuki contol
 
Mbona Magufuli alikaa miezi 3 bila Baraza la Mawaziri na Tanzania iliingia kwenye Uchumi wa kati?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ni utashi tu wa Rais,kazi za wizara zinafanywa na katibu mkuu.
Kila Rais ana moyo wake,mama kaona asubiri walau 40 ipite,atateua tu
 
Awe asiwepo hakuna manufaa yoyote kwa taifa kwanza ni hasara tupu
 
Mbona mna kiele ele Naibu wake si yupo?
Chadema mbona hamna jema! Vipi kama ule mshahara unafanyia mambo mengine?
 
Kikao cha Bunge kimefanyika na maswali ya wizara hiyo yamejibiwa.Lakini Kuna waziri asiye na wazira, Pengine ndiye anashikilia kwa kipindi hiki Cha mpito
 
Ni jinsi atakavyoona inafaa, cha muhimu ni Wizara siyo Waziri. Mtendaji mkuu ni Katibu Mkuu, wakuu wa vikozi jeshi anga nchi kavu wapo. Rais ndiye Waziri ya Ulinzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…