Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Miongoni mwa sheria mbovu sana zilizopo nchini ni inayompa mamlaka DPP ya kuweza kupeleka au kutopeleka kesi yoyote ya jinai, inayomkabili mwananchi yeyote na asitoe sababu za kutoipeleka kesi yoyote Ile mahakamani!
Hii ni sheria mbovu sana, ambayo ilitungwa Kwa nia ya kuwafanya baadhi ya wananchi kuwa ni "untouchables"
Nalielezea hili baada ya Jeshi la Polisi, kutamka hadharani, kuwa limeshakamilisha uchunguzi wake wa kesi inayomkabili yule Mama anayetambukika Kwa jina la "afande" na wamelipeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili eti aamue kuipeleka au kutoipeleka kesi hiyo mahakamani!
Hivi Kwa kosa kubwa kama hili la kuagiza vijana watano waende wakambake yule Binti Kwa kile kinachoitea " rape gang" ambayo Kwa Kila mwananchi aliyesikia huu mkasa anahuzunika sana, sasa inashangaza kusikia kuwa Jeshi la Polisi, limeshakamilisha upelelezi wake, lakini limepeleka jalada la kesi hiyo Kwa DPP, Ili akiamua apeleke kesi hiyo mahakamani na vile vile akiamua asiipeleke kesi hiyo mahakamani na hakuna raia yeyote mwenye mamlaka ya kumuhoji, Kwa nini hajapeleka kesi hiyo mahakamani!😚
Hii sheria ni mbovu sana, ambayo ilitungwa maalum Kwa kuwakinga baadhi ya watu mashuhuli nchini, Ili hata wakitenda makosa makubwa ya jinai ya aina Gani, Ili wajue kuwa wanayo kinga Kwa DPP.
Eti sheria hiyo imempa mamlaka hayo ya kupeleka au kutoipeleka kesi yoyote Ile na Wala asiulizwe sababu za kutoipeleka kesi yoyote mahakamani!
Hawa watawala wetu, wasitufanye sisi watanzania wote kuwa ni wajinga sana, kiasi Cha kututungia sheria za aina hiyo za ubaguzi wa dhahiri ambapo DPP ataangalia hadhi ya mtuhumiwa na kuamua kutoipeleka kesi yake mahakamani na kuamua kupeleka kesi za walala hoi pekee wasio na kinga hiyo ya DPP na kupeleka kesi zao mahakamani!
Hii sheria inaji-contradict na sheria mama ya Katiba ya nchi, inayosema kuwa watu wote nchini, wako sawa mbele ya sheria.
Nitoe wito Kwa waheshimiwa wabunge wetu, wapeleke muswada wa dharura Bungeni, Ili kuibadili sheria hii, ambayo inaonyesha upendekeo wa dhahiri Kwa watu wachache, wenye hadhi mbalimbali hapa nchini.
Mungu ibariki Tanzania