Mkuu
Yesu Anakuja , kwanza nimefurahi sana kujua kuwa niko humu na mdogo wangu wa UDSM sheria, ni kweli nilimaliza LL.B mwaka 2007 Dean akiwa Dr. Ibrahim Juma. Ni kweli nilikuwa biker na 2008 ile pikipiki imenifanya kitu mbaya.
Hongera kwa kufanya kazi Ofisi ya DPP.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, baadhi ya mamlaka, sheria zetu, taratibu na kanuni sio za haki bin haki.
Moja ya mamlaka hayo ni ile mamlaka presidential preventive detention order, ya rais wa JMT anapoelezwa mtu fulani ni hatari kwa usalama wa Taifa, ana mamlaka ya kukukamata na kuwekwa kizuizini indefinitely bila kuambiwa kosa wala kufikishwa mahakamani. Kina Prof. Shivji, Kanywani, Mgongo Fimbo, Chris Peter, wakaichallenge kwa mandamus na sechorari, Mahakama Kuu ikatengua power hiyo na sasa Rais akimtia mtu kizuizini kwa sheria hiyo, has to give reasons na lazima mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
Everything happens for a reason, mamlaka ya DPP kwenye Nolle bado yapo, DPP hapaswi kutoa sababu yoyote kwa yeyote na hakuna mamlaka ya kuhoji nolle!.
Naunga mkono kuwa kwenye Nolle DPP has to give reasons.
P