KERO Sheria inayompa mamlaka makubwa DPP, kuwa apeleke au asipeleke kesi mahakamani, ni mbaya na inafaa ifutwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ofisi ya DPP, haina chama, ila DPP anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote.
P
Hatujali yeye kuwa mwanachama wa CCM.

Tunachopinga sisi ni yeye kupendelea Kwa uwazi kabisa watawala wa. CCM na kuwakandamiza wapinzani wa serikali hii ya CCM, kinyume Cha kiapo chake
 
Ikisimamiwa kwa haki sio mbaya ila ikifanya Kazi kwa maslahi ya watawala ni mojawapo ya sheria mbovu na mbaya kabisa
 
eleza, ni namna gani haki zinanyimwa, usionge kiujumla. pia, peruzi hata mtandaoni nchi zingine mamlaka ya DPP yapoje ndio uje hapa kujadili kwa hoja sio mihemko. sikatai, kuna mazingine DPP huwa anaweza kuegemea kwa watawala na kutumika kama zana, ila hiyo haiondoi umuhimu wa yeye kama mwakilishi wa republic kuwa na mamlaka ya control of prosecutions kwa namna ilivyo sasa. zaidi ya yote, akiabuse powers, kuna remedy kwenye sheria pia ndio maana hata tukienda Mahakamani kuyapinga hayo mamlaka, tutapigwa chini kwasababu remedy ipo.
 
kwa fununu zilizopo (mimi na wewe hatuna jalada, sote ni raia, majadala ni ya serikali) ushahidi ulikuwepo, kama unazijua definitions za ugaidi.wengi wanaamini ugaidi hadi mtu avae mabom ajilipue au alipue wengine. mbowe inasemekana ushahidi ulikuwepo na yeye alikuwa anajua upo nata lisu alijua upo ndio maana alikimbia mbio nyingi kwenda ubelgiji, na samia alimsaidia tu. hakuwa na mabom ila kwa mujibu wa sheria ya ugaidi, wanasema evidence ilikuwepo.
 
pole kwa bike, ila hizo makitu ya kina shivji na wengine unataja, hayapo siku hizo bro, kwa sasa kuanzia arrest hadi mahakamani CPA imecontrol, yale mambo ya kuambiwa hakuna kutoka mkoa huu unaambiwa na serikali hayapo yalikufa zamani sana. na ukiona haupo huru siku hizi umenyimwa uhuru na Mahakama kutokukupatia bail ila sio DPP, na mahakama inafanya hivyo kwa kufuata sheria. naelewa shivji miaka hiyo alishawahi pelekwa sumbawanga akaambiwa hakuna kutoka mkoa ule, na alitii, ila sheria hizo hazipo tena. ubarikiwe.
 
Ikisimamiwa kwa haki sio mbaya ila ikifanya Kazi kwa maslahi ya watawala ni mojawapo ya sheria mbovu na mbaya kabisa
Huyu spika na hilo bunge kwa ujumla LIMEWADHARAU NA LINAWAONA WATANZANIA NI WAENDAWAZIMU TU

ova
 
Huo ni uongo wa mchana!

Hivi unaweza kukubaliana na huu ushahidi wa Kingai, aliyedai eti kuwa Mbowe, ali-mobilize watu, Ili wakate miti na kuilaza barabarani??

Ili Barabara hizo zisipitike??😎
 
Ni sheria ya kijinga sn, kwanini awe na uwezo wa kufungua kesi hapo hapo anaweza kuifuta bila maelezo? lazima kuwe na maelezo ya kufungua kesi na ya kufuta ni sheria ya kijinga sn ni kwa sababu hujawahi kubambikwa kesi lakini ndiyo ungejua kuwa ofisi ya DPP ni tawi kuu la CCM na haipo kwa maslahi ya umma, angalia kipindi cha Mganga kulikuwa na kesi kibao za uhujumu uchumi sahivi ziko wapi? mambo mengine ni ya kijinga sn.
 
Hata Petrol alisema siyo mfuasi wa Yesu lakini matendo yake yalimsuta, ulitaka DPP akiri kuwa ni kada wa CCM?
Hapana, kuna baadhi ya positions, mtu hatakiwa kuwa kada wa chama chochote wakiwemo watumishi wa ngazi kuanzia waandamizi wa serikali, polisi, jeshi na usalama, ila ndani ya mioyo yao, wanaruhusiwa kuwa na mapenzi na chama chochote, na baada ya kustaafu utumishi wa umma, wanaruhusiwa kuomba nafasi za kisiasa ambazo ni haki yao kikatiba, tumeshuhudia mtu aliyekuwa CJ, akigombea urais, ubunge ndio usiseme!, hiyo ni haki yao
P
 
Hii katiba nani anaifuata Paschal? tuache basi kujitoa ufahamu, kipindi cha Magu ofisi ya DPP ilikuwa imejaa kesi za uhujumu uchumi wa matajiri sahivi zipo wapi? kwanini DPP awe na uwezo wa kuondoa kesi mahakamani bila maelezo? kuna mtu anaweza kuteuliwa Tanzania kwa nafasi yoyote bila kuwa kada wa CCM? mimi nimekuwa kiongozi wa UVCCM 2014 mpk 2017 nilipojitoa kwa ngazi ya Mkoa madudu nayajua vizuri sn nimeyaishi ni utapeli tupu.
 
Hii sheria... ambayo ilitungwa maalum Kwa kuwakinga baadhi ya watu
Ilitungwa makusudi, ndio.

Julius Kambarage Nyerere is singlehandedly culpable of this criminal design.

Anaitwa Baba wa Taifa for a reason. Kila uovu wa kiutawala wa nchi hii aliusimika mizizi yeye.

And he knew better. Nyerere akiwa mwanafunzi Scotland alikuwa mwanachama wa the Fabian Society. Hawa kucha kutwa kazi ku debate tawala na siasa za dunia zinavyokwenda. Alijua tawala za dunia zinafanyaje kazi, akaja kutuletea uozo, sijui aliutoa wapi.

Hawa waliomfuata kina Mwinyi, Mkapa, JK, hawa ni monkey see, monkey do, hawana hatia, they can plead insanity, hawakuwa na upeo wa kubadilisha chochote cha Nyerere.

We unadhani Samia Suluhu Hassan akisoma hapa ataelewa tunalalamika nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…