Karma ni uhalisia wa ulimwengu kuwa, kila chanzo kina matokeo yake. Ni sawa na kusema tenda mema upate mema. Ulivyo hivi sasa ni kutokana na matendo yako, mawazo yako na maneno yako yaliyopita. Karma ni kama mkia ambao unakufuata kutokana na ulivyo na utendavyo.
Karma ni kama mkusanyiko wa matendo yako, mabaya na mema, pamoja na matokeo yake mabaya na mema. Ni msemo unaoaminika hasa katika imani za Mashariki kama vile Hinduism na Buddhism. Kila mwanadamu ana Karma yake, Karma inapaswa kuwa safi kwa kutenda mema, kuwaza mema na kisema mema. Kila hali imetokana na Karma fulani, inaweza ikawa sio yako au ikawa ya mwenzio ambayo ikakuadhiri na wewe kutokana na muunganiko wa Karma zenu.
Wapo waliofika mbali na kusema kuwa, Unapokufa Karma inaondoka na wewe, kama ulitenda mema karma yako inakuwa nyepesi na sio nzito. Karma ya mabaya ni nzito kulinganisha na roho yako, karma ya mema ni nyepesi sana. Ukifa kama ulikuwa na Karma nyepesi nafsi yako inakuwa nyepesi na kuruhusu nafsi yako kurudi katika chanzo kikuu (ulipokwepo kabla ya kuzaliwa), lakini kama ulikuwa na karma mbaya, nafsi yako inazidi kushikiliwa katika ulimwengu wa chini kwa uzito wa karma na unaendelea kuzunguka katika ulimwengu wa chini, wengine huzaliwa upya katika form tofauti tofauti ya uhai bila kujitambua kuwa umerudi lakini deeply inside roho inakumbuka. Kukumbuka ulipopitia katika maisha yako ni mpaka uungane na roho yako kwani inahifadhi maisha yako yote. Wapo walioona hayo, wengine walibahatika mpaka kukumbuka walipokwepo zamani.
Huo ni mtazamo ambao sikupenda sana watu waanze kuuelewa, lakini cha msingi fahamu kuwa Karma ni matokeo ya matendo yako na mawazo yako. Hukufuata kama vile kivuli kikufuatavyo, nakaribisha na wewe uelezee uelewa wako wa Karma ili nami nifahamu zaidi.