Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
- Thread starter
- #41
HAKIKA! sijapata kuona mwalimu mzuri, mpole,mcheshi, mwenye hekima, busara, anayejua nini amfundishe mwanafunzi, asiyekuwa mchoyo wa maarifa aliyo nayo nk: niishie tu kwa kusema kuwa wewe ni mwalimu mwema. Kwa jinsi nimesoma kwa utaratibu sana yameniingia kweli kweli. Kumbe kwa kusoma tu haya unakuwa na uwezo wa kumtazama mtu na ukajua mawazo anayowaza. Shukrani sana mkuu.
Nashukuru sana ndugu yangu.
Labda nikupe somo moja zuri, mimi sina tofauti na wewe, ninapotumia muda wangu kushare ninachokifahamu ninafurahi kwani SIAMKI peke yangu, bali TUNAAMKA wengi. Elimu yangu siipati kwa kigezo kuwa nimebarikiwa kuliko wanadamu wengine wasiojua, bali mimi ni mwanadamu wa kawaida na mwenye thamani sawa na wanadamu wote. Ninachokielekeza sio kilichopo nje yangu bali kila mtu ana jibu hilo ndani lakini anakuwa amefungwa na hali na vitu vichache kuona utajiri walionao.
Asante sana ndugu yangu.