Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal Laws)

Sheria Kuu Kumi za Ulimwengu na Akili (10 Laws of the Mind and Universe/Universal Laws)

Sawa mkuu nashukuru....ngoja niisome maana niliipitia tu juu juu.... siku hizi naonaga uvivu kusoma mada za Kiswahili hasa zikiwa ndefu kidogo nahisi ninamajini ya kizungu
utakuwa wa BK wewe, sasa ya kizungu ikiwa ndefu haikuchoshi?...dah!
 
Nimekuja kugundua kuwa hii ilikuwa ni elimu pana sana niliyokuwa nimeelezea katika posts zangu nilizowahi kupost.

Pia ninashukuru sana wale wote waliosoma na kupata utambuzi.

Mbarikiwe sana.
 
Nimekuja kugundua kuwa hii ilikuwa ni elimu pana sana niliyokuwa nimeelezea katika posts zangu nilizowahi kupost.

Pia ninashukuru sana wale wote waliosoma na kupata utambuzi.

Mbarikiwe sana.
Uzi huu upo vzr sana Apollo naomba usinsahau na kila unapotoa nondo mpya
 
Nimekuja kugundua kuwa hii ilikuwa ni elimu pana sana niliyokuwa nimeelezea katika posts zangu nilizowahi kupost.

Pia ninashukuru sana wale wote waliosoma na kupata utambuzi.

Mbarikiwe sana.
Good
 
Nimekuja kugundua kuwa hii ilikuwa ni elimu pana sana niliyokuwa nimeelezea katika posts zangu nilizowahi kupost.

Pia ninashukuru sana wale wote waliosoma na kupata utambuzi.

Mbarikiwe sana.
Ni elimu kubwa sana mkuu mfano wake hakuna. Mimi nimeamua kufuatilia post zako zote mdogo mdogo nikimaliza ndio natoa maoni yangu.
 
Asante sana mtoa mada nakutakia kila la heri.

Nilichojifunza katika mada hii ni nguvu ya karma,umeelezea kwa ufasaha sana japo ni elimu ya utamaduni wa jamii nyingine ya mashariki huko lakini kimantiki inaendana kabisa na maisha ya kawaida ya binadamu ya kwamba kutenda kunena ba kuwaza mema. Na haina mpishano na mafundisho yetu tunayopewa katika dini hizi zetu.

Pili nimejifunza ya kwamba katika akili ya mwanadamu ndiko kunakozaliwa kila kitu, iwe ni upendo furaha amani mafanikio kama ya afya njema utajiri nk.
Kwamba katika akili ndipo inapozaliwa imani na kuijenga hio imani kwa jinsi inavyotakiwa dhidi ya Mungu.

Kwamba jambo lolote ukilizingatia kwa kuwekea akili yako kwa kiasi kikubwa hilo jambo litakuwa .

General nimejifunza kila tokeo duniani limeanzia katika akili yaani wazo au fikra ndio likaja katika uhalisia.
Ila hio akili inasheria zake na zikifuatwa kikamilifu ndio hayo yatatokea.
Ni zipi hizo sheria?
Nafuatilia sasa katika mada zinazoendelea
Asante Appolo na ubariwe.
 
Endelea baasi kutoa elimu hii adimu.
Nimekuja kugundua kuwa hii ilikuwa ni elimu pana sana niliyokuwa nimeelezea katika posts zangu nilizowahi kupost.

Pia ninashukuru sana wale wote waliosoma na kupata utambuzi.

Mbarikiwe sana.
 
Apollo mimi nadhani hizi sio sheria bali ni kanuni. Sheria hupinduliwa, lakini kanuni hazipinduliwi!

Mfano kanuni ya kutafuta eneo la mraba, mstatili itaendelea kuwa vile vile miaka na miaka. Kinachoweza kubadilika na kupatikana njia mbdala tu lakini will reach at the same destination!

Napenda kanuni, SIPENDI SHERIA/LAW!
Nimekupata vema hapa
 
Apollo; ahsante sana kwa somo zuri ila nashangaa namba mbili link haifungui; kulikoni?
 
Apollo; ahsante sana kwa somo zuri ila nashangaa namba mbili link haifungui; kulikoni?
Pole sana. Nimecheck naona haifunguki. Will see what I can do to assist. Pole sana.
 
Kila siku napita hapa lakini naona bado ina mapungufu. Kulikoni?
 
Asante
Ni kutoka katika Jitambue Sasa.

Unaweza ukaziita Ni KANUNI AU SHERIA AU LAWS.

Akili ya mwanadamu ni sehemu ambayo watafiti wengi wamekuwa wakihamasika kuielewa. Akili ni sehemu pana sana kwa mwanadamu. Ni sehemu ambayo haionekani wala haishikiki lakini ina matokeo makubwa sana kwa mwanadamu. Akili imezaa vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu, mawazo, imani, misimamo n.k. Kama unapenda sana kujifunza na kufahamu mengi lazima utakuwa unatamani kufahamu siri kuu za akili. Kuelewa siri kuu za akili ni kufahamu Sheria ambazo zinaiongoza akili. Katika mada hii utapata kuona mwanga kuhusiana na akili na kuweza kujifahamu vyema.

SHERIA/KANUNI HIZO NI:

  1. Sheria ya Chanzo na Matokeo
  2. Sheria ya Uhuru wa Kufikiria
  3. Sheria ya Umakini/focus
  4. Sheria ya Mawazo
  5. Sheria ya Ubinafsi
  6. Sheria ya Uumbaji
  7. Sheria ya Hisia
  8. Sheria ya Ubadili
  9. Sheria ya Usawa wa Akili
  10. Sheria ya Kutokea.Nini maana ya Sheria za Akili?

Mapinduzi makuu ya sasa ni ufuatiliaji wa asili na jinsi akili ya mwanadamu ilivyo. Sayansi ya kufuatilia akili ya mwanadamu ilivyo ni sayansi ambayo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa kwani akili ya mwanadamu ina sayansi kubwa sana. Asilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu inatengenezwa na akili yake hivyo katika elimu hiyo utaweza kufahamu mengi sana kuhusiana na mwanadamu na jinsi akili yake inavyofanya kazi vyema.

Mlolongo huu wa mada utakuwa na mada kumi, ambapo kila mada itaelezea sheria yake kwa undani kwani kuweka mada moja kuelekeza mad azote hizi kutapelekea uchache wa maelekezo.

Sheria
Kwa lugha nyingine huita "Laws". Sheria ni kama maelekezo ya suala au jambo Fulani. Wengi wanafahamu sheria ya mvutano, ni sheria inayosema kuwa ukirusha kitu juu basi huvutwa kwenda chini kuelekea ardhini. Ni sheria ambayo uwe unaijua au usiijue ukijirusha gorofani lazima uanguke chini. Sheria kuwepo haimaanishi mpaka uijue ndipo matokeo yake huonekana bali hata ukiwa haujui bado sheria itafanya kazi yake katika mangilio wake unavyotaka.

Zipo sheria mbalimbali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikilinda taratibu nyingi. Je umewahi kujiuliza kama kuna sheria au taratibu Fulani ambazo ukizielewa utaweza kufahamu jinsi akili inavyofanya kazi? Ni sawa na mkulima, akipanda maembe atavuna maembe, hata kama anajua kuwa anavuna anachopanda au hajui kuhusiana na uhusiano uliopo kati ya anachovuna na anachopanda bado atapata matokeo sawa. Hivyo ni vyema kufahamu sheria hizo. Ni vyema kufahamu kwani itakusaidia kuweza kuongoza matokeo. Ukiwa unajua kuwa taratibu Fulani hupelekea matokeo Fulani inakusaidia kutengeneza wakati ujao katika njia njema na kupata matokeo mazuri.

Mfano wa sheria nyingine ni sheria za rangi, kila mmoja anafahamu ukichanganya nyekundu na njano unapata machungwa, ni sheria kwani lazima itokee hivyo. Uwe unajua hilo wakati unachanganya au haujui lakini lazima matokeo yake yatokee. Ukichanganya blu na yellow utapata kijani, hiyo ni lazima. Labda uwe haujachanganya vyema au tatizo linguine lakini zikishachanganyika matokeo yake ni mengine.

Lengo la kutoa mifano hiyo ni kukupa mwangaza wa kuwa kuna sheria hapa ulimwenguni. Sheria ni taratibu ambazo zipo. Taratibu hizo hupelekea matokeo Fulani katika taratibu Fulani. Ni vyema kufahamu taratibu za msingi kuelewa mengi kwani ulimwengu upo kwa taratibu maalum. Kama tungekuwa hatujui kuwa ukiruka gorofani utaanguka chini na kufa kwani ukiruka unaanguka chini ni wangapi wangekuwa wamekufa kwa kutojua hayo? Lakini anayeuuzia hayo au kufanya maamuzi bila kujali au kwa kujali lazima taratibu zichukue nafasi yake na kupelekea matokeo yake.





SHERIA KUU ZA AKILI YA MWANADAMU.

Kama dunia ilivyo na sheria zake, serikali zilivyo na sheria zake, dini zilivyo na sheria zake, tamaduni Fulani za watu zilivyo na sheria zako fahamu kuwa hata akili nayo ina sheria zake. Kuna sheria za biolojia, jeographia, fizikia, n ahata saikolojia. Fahamu kuwa na hata akili ina sheria zake. Sheria hizo hutawala maisha ya mwanadamu kwani kila mwanadamu ana akili yake lakini akili zote zina asili moja na sheria moja, tofauti ni utumiaji.

Fahamu kuwa unaweza kuiongoza akili yako na kuitawala akili yako. Akili ni chombo kizuri sana kwa kubadilika lakini pia ni chombo kibaya sana kwa kupotoka.

Mada za Kuhusiana na Sheria hizo zinafuta, na kila sheria itaelezewa katika mada yake na mifano hai ambayo itakufunua mwangaza na kuelewa vyema jinsi akili ya mwanadamu ilivyo ya ajabu.


Sheria Ya 1: Chanzo na Matokeo.




Mawazo yetu ndiyo yanayounda uhalisia wetu na sio vingine. Hii ni sheria ya kale sana tangu enzi za wanadamu wa kale waliopenda kuwa watafutaji wa ukweli wa ulimwengu walikutana nayo. Ni sheria ambayo inafahamika sana na imetafsiriwa katika maelezo tofauti tofauti katika imani tofauti tofauti.
Ni sheria Kuu.

Kama ilivyo leo, hakuna anayefahamu ni kwanini kuna sheria kama vile ya Gravity, sheria za sayansi, n.k. Na hata katika sheria hii hakuna anauejua kwanini sheria hii ipo lakini hiyo haijalishi, kinachopaswa kwetu sisi wanadamu ni kuielewa vyema na kujua jinsi inavyofanya kazi ili nasi tuweze kuishi nayo.

Wazo ndio chanzo, vingine vyote ni matokeo tu.
Watu wengi hasa ambao hawajasoma sana wanafikiri kuwa vitu vya kifizikia ni halisi, wanafikiri ni kweli vitu hivyo vipo kifizikia. Kutokana na uelewa wao huo wanakuwa wanaamini sana ulimwengu wa nje yao na kusahau ulimwengu wa ndani yao. Huwezi kuelewa ulimwengu wa nje bila kuelewa ulimwengu wa ndani, ulimwengu wa nje ni matokeo ya ulimwengu wa ndani. Kutokana na kutoelewa huko watu wamekuwa wakiteseka na kuamini hawawezi kubadili maisha yao kwani hawajui chanzo cha maisha yao. Hawafahamu kuwa maisha yako ni matokeo ya uelewa wako wa ndani yako.

Mfano mzuri katika kuelewesha hilo ni sawa na tunaangalia sinema, kumbe sinema hiyo inatokana na matukio yaliyopo ndani ya ufahamu wetu. Sio sinema iliyopo nje yetu bali chanzo chake cha matukio kinatokana na ufahamu wetu. Sinema yake ni kama display tu ya ufahamu wetu. Kutoelewa hayo wanadamu wengi wamekuwa watumwa na wanateseka kutokana na kutofahamu chanzo cha hayo yote ni nini.

Kumbuka kuwa tunapoangalia sheria za kifizikia tunafahamu dhahiri kuwa HAKUNA JAMBO LISILO NA CHANZO. Na sheria hii ndipo iliposimamia. Hakuna jambo lisilo na chanzo na ndio maana inaitwa sheria ya chanzo na matokeo kwani kila tokeo lina chanzo chake. Hakuna matokeo yasiyo na chanzo kamwe.

Hivyo kama kila jambo lina chanzo chake, tunapaswa kufahamu kuwa uhalisia/reality ni illusion/Uongo kwani reality inatengenezwa na sisi wanadamu wenyewe na sio kwingine. Reality au uhalisia unaoishi unatokana na milango yako ya ufahamu, akili yako, imani yako na uelewa wako.

Kila kitu kina chanzo, huo ni uhalisia. Kila kitu kilianza kama ufahamu, mfano mzuri ni Computer, madirisha, nyumba, simu, nguo, sanaa, na vyote ambavyo vimetokana na ujuzi wa mwanadamu vilianza kama WAZO, baada ya kufanyiwa kazi vikatokea katika dunia ya kifizikia. Lakini hapo kabla vilikuwa ni Mawazo na sio physical things.

Chunguza sana sheria hii, kila tokeo unaloliona lina chanzo chake, kufahamu sheria hii inakusaidia kuwa mtafutaji wa ukweli. Badala ya kupoteza nguvu katika matokeo unapaswa kufuatilia chanzo cha tokeo kwani kubadili chanzo ni kubadili matokeo.

Walimu wakubwa wa ulimwengu huu wote wamefundisha sheria hii, wanaweza wakawa hawajakuambia moja kwa moja kutokana na kuwa uelewa wa wanadamu unatofautiana kwa jinsi wanavyoutumia lakini walimu hao wamekuwa wakitufundisha vyema kwa mifano. Mfano mzuri ni kuwa


  • Unavuna unachopanda: Ukipanda maembe utalima maembe, ukipanda magugu utavuna magugu. Sheria hii ni sawa na kukuambia kuwa kila tokeo lina chanzo, kubadili chanzo ni kubadili matokeo. Huwezi kuvuna maembe katika tawi la mchungwa.
  • Sheria ya Karma: Ni sheria ya mashariki inayosema kuwa kila WAZO, TENDO na MANENO yana matokeo yake katika ulimwengu wako. Kutokana na hilo wakafundisha kuwa kuna Karma ya matendo, Kuna karma ya maneno na kuna karma ya mawazo. Hivyo kila tutendacho, tusemacho na tunachofikiria kina matokeo katika dunia yetu. Nimesema dunia yetu kwani kila mwanadamu anaishi katika dunia yake. Sheria hii nayo nitakuja kuieleza vyema.
  • What goes around comes around: Nayo ni sawa na kusema kuwa kunachokijia ni matokeo ya kilichotoka kwako. What comes around is the result of whats goes out of you. Unachokipata ni matokeo ya ulichokitoa.
Tutakapokuja kufahamu kuwa tunaishi katika ulimwengu unaoumbwa kutokana na ufahamu wetu, kwa kufahamu hayo ni hatua moja ya kwanza katika kuweza kubadili maisha yako na kuweza kuelewa kwanini wanadamu wengine nao wanaishi katika uhalisia tofauti na wewe. Kwa kuanza kuelewa hili utaweza kujiuliza mengi na kujikuta unafahamu chanzo cha mengi badala ya kupoteza muda katika matokeo. Wengi hupoteza muda kubadili matokeo kumbe matokeo ni matokeo, huwezi kuyabadili bali unaweza kubadili chanzo chake.


Maya Angelou aliwahi kusema sentensi moja nzuri sana -

Kwa kuweka sheria hii katika uelewa mzuri na kwa kufupisha vyema ni kusema kuwa:

Mawazo yetu yanaumba ulimwengu wetu, mawazo yetu ndio kiaishiria ya kinachofuatia. Kila jambo lina chanzo, chanzo kikuu na chanzo ambacho ndio cha mwanzo kabisa ni WAZO. Tunaishi katika dunia ambayo inatengenezwa na uelewa wetu. Ndio maana kila mwanadamu anaishi katika dunia yake kutokana na kuwa uelewa unatofautiana baina ya wanadamu.
BADILI MAWAZO YAKO KUBADILI DUNIA YAKO.


SHERIA YA PILI INAENDELEA HAPA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom