Sheria mojawapo ya Maskini inasema: Usionyeshe wala usi-post Mafanikio yako

Sheria mojawapo ya Maskini inasema: Usionyeshe wala usi-post Mafanikio yako

SHERIA MOJAWAPO YA MASKINI INASEMA: USIONYESHE WALA USI-POST MAFANIKIO YAKO.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuna maskini na umaskini wake. Alafu kuna tajiri na utajiri wake.
Umaskini na maskini wanasheria na kanuni zao.
Matajiri na utajiri wanasheria na kanuni zao.

Wapo maskini wa aina tatu ambao ni Maskini wa kiuchumi (kipato), maskini wa kifikra(kiakili) na maskini wa Kiroho.
Umaskini wa kiuchumi unategemea zaidi aidha wewe ni maskini wa kiakili au Kiroho au vyote viwili.
Yaani ili uwe maskini wa kiuchumi itakupasa uwe aidha mjinga(maskini wa kiroho) au uwe Maskini wa kiroho(yaani unaamini katika miungu isiyo na msaada).

Moja ya sheria ya Maskini katika umaskini inasema USIONYESHE wala ku-post mafanikio yako.
Alafu ukifuatilia hoja yao kuu wanasingizia mambo makuu yafuatayo;
i) Ambao hawajafanikia watajisikia vibaya.
Alafu hapohapo wanamshirikisha Mungu(tajiri Mkuu) kuwa hapendi uonyeshe mafanikio yako. Jambo ambalo ni uongo na uzushi.

ii) Wapo Watu wenye husda ambao wakikuona watakufanyia ubaya ili uanguke. Jambo ambalo pia halina mantiki na linavunja kanuni za uhuru na utajiri.
Kwenye Kanuni za utajiri na nuruni ni kuwa kila unachofanya alafu ukafanikiwa lazima uonyeshe na u-post.

Hoja ya Maskini na umaskini zote ni za kijinga na zimelenga Ushetani na ushenzi. Na ukandamizaji.

Hoja hii ndio imefanya baadhi ya jamii na mikoa hapa Tanzania, vijana wanashindwa kujenga kwao kwa kuogopa kuwa watadhuriwa iwe kwa kulogwa au kwa namna nyingine na wale Watu wenye Chuki.

Jamii yoyote inayoficha Mafanikio, yaani inayotumia kanuni ya umaskini huwezi kukuta imeendelea. Lazima iwe fukara.
Ni uchawi kuficha mafanikio. Dalili mojawapo ya Watu maskini na wachawi ni kuficha vitu Vizuri.

mtu mwenye chuki ana chuki tuu. Na mtu mbaya ni mbaya tuu. Asisingizie kuonyesha kwako mafanikio kama wewe ndiye umemsababishia yeye kuwa na chuki. Nop!
Hata Kaini na Abel Kesi yao iko kwa namna hiyo.

Mwijaku wakati anaonyesha mafanikio yake Maskini na umaskini wao wengi walipiga kelele sana. Sio kwa sababu gani isipokuwa Chuki zao.

Yaani mtu ashindwe kuonyesha furaha yake kisa Chuki iliyopo moyoni mwako.
Mtu ashindwe kujenga kwao ati kisa asionyeshe mafanikio yake. Huo ni Ushetani, uchawi na kuhujumu uchumi wa jamii.

Matajiri wote wakipata mafanikio yao lazima wayaonyeshe kwa kuyafurahia na kufanya sherehe kubwa kwa kualika Watu.
Lakini hiyo kwa shetani na mashetani(maskini na umaskini) huchukulia jambo hilo kama majivuno wakati sio majivuno. Huona kama wanatambiwa au kuringishiwa jambo ambalo sio kweli.

Kwa vile maskini na úmaskini kama ilivyo uchawi wamezoea kula na kufanya sherehe zao usiku wakila nyama za Watu au wakifanya mambo mabaya basi wanataka walete kanuni hizo kwa Watu waliofanikiwa. Sio Sahihi.

Mtu asikutishe. Ukifanikiwa. Onyesha mafanikio yako uyafurahie na uwapendao. Onyesha kuwa Mungu amekusaidia.
Shetani hapendi kazi za Mungu zikiwa hadharani.

Ikiwa kuna mtu yeyote atakayejisikia vibaya kwa kuonyesha mafanikio yako basi jua yeye ndiye anamatatizo. Wewe mafanikio yake hayamhusu hata kidogo. Hujafanya sherehe kwake.

Yeye kama anamcha Mungu na anaupendo hawezi kujisikia vibaya ati kisa wewe unaonyesha mafanikio yako. Atakachokifanya ni kukupongeza na kumshukuru Mungu kwa ajili yako. Alafu yeye atasubiri wakati sahihi Mungu atakapoona naye amfanikishe. Na hata asipofanikiwa haitamuuma kwa sababu huenda ni mapenzi ya Mungu.

Lakini yaani ununue gari kali, uache kuenjoy kisa kuna wachawi wanaumia ukilitumia. Nani kawaambia unawaringishia, nani huyo?

Ati uache kuonyesha unakula vizuri kwa sababu kuna Watu hawali hivyo. Kwani wewe ndio umefanya wasile? Come on!
Kama mtu ana moyo safi anamoyo safi tuu. Kuona mafanikio yako kutampa moyo kuwa kama Mungu amekubariki wewe basi naye sio siku nyingi atabarikiwa..

Utajiri yaani uungu ni kufanya mambo hasa mafanikio yako yaonekane. Na Ushetani ni kufanya mambo yawe gizani, kuyaficha mambo mema na mazuri.

Zingatia, usionyeshe mipango na mikakati. Onyesha mafanikio yako. Sio dhambi.

Taikon nimemaliza! Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Maskini sometimes ni washenzi sana.
Wanakesha page za kina Mange na Manara, Wema na Bichuka kuangalia picha za wenzao na kuzitamani lakini wao wao wanakwambia usimuonyeshe mwenzio mafanikio yao.
Sasa wajiliza kwaninimtu anunue simu ya 3 milioni na kamera nzuri ili apoge picha na kuziweka chini ya kitanda au ili akifa watu wakate na kuweka X?

Maskini hataki mwenzake afanikiwe na huwa ndio wa kwanza kuwa na husda.
 
Kuna watu wana roho za hasada wakikuona akakunenea vitu haviendi
Kama ushagundua Hata kama kuna deal ukifanya kimya kimya linatiki sasa liseme kabla kwa watu
Kama kufanya mambo yako kimya kimya ni umaskini niiteni maskini tena ile venye mnaita absolute
 
Kuifanya vitu kimya kimya huwa vinafanikiwa zaidi
Unajifunzia wapi kufanya hivyo vitu kama si mtu ameposti?
Diamond anaimba kimya kimya?
Bakhresa anauza kimya kimya?
Whozu, vunja Bei wanafanya kimya kimya?
shishi Food anafanya kimya kimya?


Duka la Simu Kariakoo huweki simu zako status na video, unauza kimya kimya?
Huweki page ya instgram unauza kimya kimya?


#Maskini wanajichuja hapa jamvini.
 
Yaan upate frame hujaweka mzigo ushapost, ununue Bajaj ushapost bladifavkyen
Maskini hawataki mtu aposti, ila kila siku wana bando wanakesha kwenye page za kina mange na diamond.
Utakuta maskini anayekwambia usiposti yeye ni follower wa Mange na ame- like lile li benzi la mange G-WAGON.
 
Maskini hawataki mtu aposti, ila kila siku wana bando wanakesha kwenye page za kina mange na diamond.
Utakuta maskini anayekwambia usiposti yeye ni follower wa Mange na ame- like lile li benzi la mange G-WAGON.
Mm siwezi mpangia mtu apost au asipost lkn kushare mambo ni hulka binafsi.....Mimi binafsi siweziiii
 
Sasa tukuelewe vipi mkuu? Tushike lipi kati ya hili la leo ua la kwenye uzi mwingine uliosema tuwe wasiri.
Thread 'Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe' Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe

Mipango na mikakati ndio hukupa utajiri. Nafikiri ukisoma hiyo mada utajua ujumbe ulikuwa upi.
Utajiri haujawahi kufichwa ni kama nuru. Kadiri unavyouficha ndiyo unavyojidhihirisha
 
Back
Top Bottom