Sheria na taratibu za kuasili (Adopt) mtoto Tanzania

Helooo wapendwa.....
Mimi ni mzima wa afya, hofu na mashaka ni juu yenu nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu....lakini natumai salam zangu zimewafikia popote pale mlipo....na poleni na harakati za kutafuta grisi....
Moja kati ya malengo niliyojiwekea mwaka huu ni kuweza kuwa na mtoto wangu....sio wa kuzaa.....ila nataka nipate mtoto kwa njia ya kuasili (adoption)....japo ni njia ambayo kwa hapa kwetu sijaiona sana watu wakiitumia ila mie nina sababu zangu za msingi.....hivyo ningependa kujuzwa sheria...taratibu.....na taasisi zinazohusika na hili swala.....asanteni
 
Tafuta ofisi za ustawi wa jamii popote ulipo au wakili anayejuwa sheria ya kifamilia. Vile vile unaweza kwenda wilayani watakusaidia.
 
nenda kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ama kama tayari umempata sehemu .nenda ofisi za kata ambazo siku hizi kuna ustawi wa jamii. hawa watakuhoji maswali kadha na watakupa form maalum baada ya kujaza na kurudisha wao watafanya uchunguzi wao.then ukikizi vigezo na masharti utapewa mtoto. wataangalia uwezo wa kumlea,mazingira ya kumlelea,capital nk nk
 
Asante mkuu....
Naomba nikuulize japo kidogo tu japo hili swali naweza kuuliza huko uliponielekeza.....ni lazima niwe nimeoa?
 
Asante mkuu....
Naomba nikuulize japo kidogo tu japo hili swali naweza kuuliza huko uliponielekeza.....ni lazima niwe nimeoa?
ni rahisi zaidi ukiwa umeoa lkn hata kama hujao bado una nafasi ya kupata kuna vitu vingi wanaangalia back ground history,criminal history ,nk nk
 
EM hawezi kuzaa na wewe?
 
Taratibu za ku asili mtoto Tanzania zikoje?Hakuna kiasi cha pesa unatakiwa kulipa? Kama ukiasili mtoto kutoka kituo cha yatima baadae wakajitokeza ndugu (kama hana wazazi) wakadai wanaweza kumtumia sheria inasemaje?

Mwanamke aki asili mtoto mchango chini ya mwaka je anaruhusiwa kuchukua likizo ya maternity?
Kama kuna taarifa zaidi juu ya kuasili mtoto naomba kujulishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari za asubuhi, naomba kwa wanaojua mnisaidie.

Je, ni taratibu gani zinapaswa kufuatwa ili mtu aweze kuasili(adopt) mtoto?

Ni umri gani unaruhusiwa na kwa mazingira gani?

Na ni Nani amayeruhusiwa kuasili?

Karibuni wadau, shukrani sana.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…