Sheria tatu za kutumiana Meseji

Sheria tatu za kutumiana Meseji

Sheria tatu za kutumiana meseji au kuwasiliana na mpenzi wako,na hii ni mahsusi kwa wale ambao ndio wanaanza mahusiano

Sheria namba moja,je huwa ana kawaida ya kujibu meseji zako,kama huyo mpenzi wako ana utaratibu wa kujibu meseji ni sawa hapo unaweza kuendelea kumtumia meseji lakini huwa anazipuuza basi usimtumie meseji zako,na ni dalili tosha kwamba hayupo interested na wewe period

Sheria namba mbili, je huwa anatumia mda gani kujibu meseji zako,kuna yule mtu ukimtumia meseji huchukua masaa mawili hadi matatu kujibu meseji,basi nawe nenda nae sawa,akitokea kukutumia nawe nenda nae sawa vile kama anavyofanya,kama anajibu fasta nawe jibu fasta,kama baada ya dakika tano nawe hivyo hivyo,malegend tunaweza hilo ila vitoto vya elfu mbili najua hamnielewi

Sheria namba tatu, usitume meseji nyingine kama ya mwanzo haijajibiwa,maana kuna ile umetuma ya kwanza hola hakuna majibu unatuma nyingine,hapana hapo unafeli,kausha hata siku moja au mbili zipite,maadamu text ya kwanza haijajibiwa basi usitume nyingine

kama yeye anajifanya ni mtu muhimu sana hata wewe ni muhimu vile vile

Ni hayo tu!
Agreed
 
Hiyo namba mbili kuna demu mmoja alidhani labda mimi mshamba wa mapenzi sijui? Aisee nikimtumia message moja hasomi mpaka week inaisha ndo anaisoma na kujibu, na mimi nikawa nafanya zaidi yake yani najibu message baada ya week mbili mpaka akakimbia mwenyewe kudadeki.
Mkuu kuna baadhi ya watu hawapo interested kabisa na mambo ya chat.
 
Yan mzee bahat mbaya Kila naempata nakuta kanizidi umri na Ana mtoto au watoto nikitongoza ninaowazidi wananikataa
ebu jaribu kujitathimini namna ya kuwa aproach,kwasababu kukataliwa ni jambo la kawaida ila ishu inakuja je unakataliwa mara ngapi

ebu badilisha namna ya kuwaingia kwa maana tumia stahili tofauti uone itakuwaje
 
Huo muda wa kutumiana Kwanza huo mnautoa wapi?
Mi nidhani wavulana na wasichana ndio wanatumianaga message Kumbe hata watu wazima Kama nyie?

Ina maana hamna kazi za kufanya sio?
Duu hope huu ni utani,hakuna mawasiliano mepesi kama meseji,kwasababu ukiwa umeshughulishwa na mambo na mtu akikupigia inakuwa ngumu kupokea,lkn akituma text hata baadae utajibu kwa mda wako,istoshe hata ukiwa mbele ya watu wengi bado mawasiliano yako ni faragha sana
 
Ye
Muhimu ni mtu kufunguka tu " Am not interested" na sio kujikuta kama celebrity wanapofuatwa DM
Yeah tena hao huwa nawakubali sana tunaokoa mda na tunaendelea na mambo yetu
 
Back
Top Bottom