Sheria ya droo (sare) kwenye mpira wa miguu iangaliwe upya

Sheria ya droo (sare) kwenye mpira wa miguu iangaliwe upya

Au basi iwe point moja apewe alietoka sare ya magoli, mkitoa droo ya bila magoli msipate chochote
 
Asante kwa kuleta hoja fikirishi!! Mimi naamini lengo la mpira wa miguu ni magoli!! Ili kuongeza kiu ya kufunga magoli napendekeza ifuatavyo:
1. Timu inayofungwa ipate robo pointi kwa kila goli walilofunga. Lakini mwisho wa pointi za mtindo huu iwe ni 1.
2. Timu iliyofunga/iliyoshinda ipate pointi 4.
3. Timu iliyopata sare isiyokuwa na magoli kila timu ipate pointi 1.
4. Timu iliyopata sare yenye magoli kila timu ipate pointi 2.

Nawasilisha.
Wakifanya hivyo mpira utakua wa hovyo sana, Lengo la mechi ni kushinda, na magoli ndiyo yanayoleta ushindi, kwaiyo ili kujihakikishia ushindi kuna mambo mawili, funga magoli mengi ili mpinzani wako asiweze kurudisha au funga goli moja alafu paki bus ili kulinda ushindi.
 
Kabla ya hapo timu.iliyokuwa inashinda ilikuwa inapata pointi mbili na draw pointi moja ili kuondoa tofauti ya draw na ushindi na kuhamasisha timu zishinde ndio wakaweka mshindi apate pointi tatu. Tukiweka draw pointi mbili tutarudi kulekule.
 
Wakuu mpo?

Naamini wengi tunaangalia mechi inayoelekea mwishoni kati ya Chelsea na Man City ila pia huenda tunnangalia mechi inayoendelea kati ya Lazio na Roma ambayo huenda ikaisha kwa suluhu ya 0-0.

Hivi kwa logic ya kawaida ni sahihi Chelsea na Man City walifungana 4-4 wapate point moja moja sawa na Lazio na Roma ambao huenda wakatoka 0-0?

Kwanini game za moto kama hii ya Chelsea na City wasiwe wanapewa point 2 na hii inayoisha 0-0 wakapewa point 1?
Umewaza vzr sana mkuu nakuunga mkono

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya hapo timu.iliyokuwa inashinda ilikuwa inapata pointi mbili na draw pointi moja ili kuondoa tofauti ya draw na ushindi na kuhamasisha timu zishinde ndio wakaweka mshindi apate pointi tatu. Tukiweka draw pointi mbili tutarudi kulekule.
Kumbe iliwahi kuwa hivi sikuwahi kujua
 
Back
Top Bottom