Sheria ya Faini ya Millioni 50 kwa kila chombo kilichopata ajali na Fidia ya Millioni 500 kwa kila kifo, ajali zote zingeisha ndani ya siku moja

Sheria ya Faini ya Millioni 50 kwa kila chombo kilichopata ajali na Fidia ya Millioni 500 kwa kila kifo, ajali zote zingeisha ndani ya siku moja

Umeandika vizuri lakini umesahau 99% ajali zinasababishwa na dereva,
Dereva ndio anajua hapa nalimwaga hapa nachomoka
Niliwahi kuandika huko nyuma ukisikia story za madereva wa lorry na buses wakiwa pale magufuli au TPA basi kama una gari dogo hizi barabara utaziheshimu
Napendekezs kwa dereva aliesababisha kifo kuwe na adhabu ya KIFO refer kwa ajali za Allys Star na Train, New Force, Ahsante rabi mwaka jana mwishoni, kina Sauli karibia ma Chalinze na Kibaha na wengine

Ukihukumu mmiliki huyu dereva anaenda kampuni nyingine na anawalaza kama kawaida,
Dereva akisababisha ulavu kue na kifungo cha maisha
Adhabu zikiwa kwa wamiliki huku sio wao watoa license au kujua kiundani historia ya dereva kwangu sio sawa
 
Sidhani kama umefikiria vyema

1. Anayelipa ni mmiliki wa chombo au dereva aliyesababisha ajali?

2. Unaposema bima ya lazima, kwani sasa hivi sio lazima kuwa na bima?

Mbona kama lengo lako ni kuwakomoa wamiliki wa vyombo vya usafiri? Una ugomvi nao au ndio ile masikini anakuwa tu na chuki na tajiri hata kama hakuna sababu?
 
Sidhani kama umefikiria vyema

1. Anayelipa ni mmiliki wa chombo au dereva aliyesababisha ajali?

2. Unaposema bima ya lazima, kwani sasa hivi sio lazima kuwa na bima?

Mbona kama lengo lako ni kuwakomoa wamiliki wa vyombo vya usafiri? Una ugomvi nao au ndio ile masikini anakuwa tu na chuki na tajiri hata kama hakuna sababu?
Kwa hiyo dereva ndio analipa, dereva ndio mmiliki wa gari?
 
Narudia kwa kusema Leseni za udereva zitolewe kwa watu wenye elimu ya kuanzia Diploma na mwenye diploma lazima awe amehitimu elimu ya Sekondari.

Alafu sheria zingine ziwekwe vizuri ikiwemo fidia kwa waathirika zinazosababishwa na ubovu wa miundo mbinu kama barabara, ubovu wa chombo husika, uzembe wa dereva, ufugaji wa mifugo kama ng'ombe kula majani mbembezoni mwa barabara, nk.

Haya yote hayawezi kufanyika kwa Serikali ya chama hiki kilichokaa madarakani kwa zoidi ya miaka 60.

TUNAHITAJI CHAMA MBADALA.
 
Mkuu hoja yako ya faini umeweka upande wa Hasira sana,umewahi kufanya au kusimamia kazi za usafirishaji?

1. Magari mengi yaliyo barabarani hayana hali nzuri sababu hatuna mifumo na manpower kubwa ya kukagua road worthiness ya kila gari. Baadhi ya kampuni zinafanya Preventive Maintenance Services na hizi ni mara chache kukuta gari zao zimepata ajali na breakdown

2.Matumizi GPS tracking na dash camera kwa ajili ya ku monitor gari na dereva kama kachoka kampuni au mmiliki aweke sera gari ikitembea masaa 6 dereva apumzike nusu saa ndio aendelee na safari na mmiliki anaona gari imepaki,muda na eneo ilipopaki.

3. Kwa magari ya local na trip town kuwe na sheria dereva wawe wawili endapo gari inafanya 24hrs au kampuni ikimtumia dereva kwa 24hrs siku inayofata apewe mapumziko. Nature ya kazi za Container za Trip town dereva anaweza akakesha zaidi ya siku 3 anaenda ICD/Bandarini/final destination kwa mteja kwenda bandarini anakutana na foleni na kuendesha kwenye foleni umakini unakuwa mkubwa anaingia kwenye uchovu(fatigue). Dereva akichoka umakini unapungua, anakuwa hatarini kupata ajali. Wengine wanawachia wasaidizi ambao hawana uzoefu turnboy.

4. Magari ya abiria na mizigo ya kuanzia tani 3 na kuendelea inabidi iweke sheria yanapoingia nchini lazima yawe na Hill climbing assistance,Lane Departure warning system, ABS kwa trailer na tractor truck, Trailer Anti Rolling System. Nchi za wenzetu huwezi sajili gari ya kazi bila kuwa na safety system kama hizo.

5.Madereva wengi hawana mafunzo ya gari (Drivers Training)husika kabla ya kukabidhiwa gari. Kampuni kama Scania huwa wana utaratibu wa kutoa mafunzo kwa madereva kwa kila toleo la gari yao, au kuwapa mafunzo madereva wa kampuni zinazotumia huduma zao. Trucks zipo za aina nyingi mifumo inakuwa tofauti ni lazima dereva apewe mafunzo ya gari husika kabla hajakabidhiwa.

6. Miaka ya saizi vijana wadogo under 20yrs wanapata leseni daraja E wengi uzoefu wanakuwa hawana na hawendeshi kwa kujihami(Defensive driving) hawajali watumiaji wengine wa barabara na wanakosa maamuzi sahihi.
 
Umeandika kana kwamba huijui Tanzania wewe.
Hapo kwa hiyo sheria utatengenea mabilionea wapya kutoka jeshi la polisi na ajali hazitakwisha.
Ajali sababu zake kuu ni 3.
1.Uzembe wa dereva
2. Hitilafu ya chombo
3.Ubovu wa miundombinu au miundombinu kutokukidhi viwango.
Haya hapo kosa la serikali (miundombinu), kosa la dereva (uzembe) na kosa la mmiliki (hitilafu ya chombo) iweje adhabu atwikwe asiyehusika?
 
Bongo Sheria ni biashara nani atasimamia hayo mapato.
Hakimu ukimpa tu 10m anakupa ushindi
 
Je ile adhabu ya kutaifisha nyumba/chombo cha moto kinachotunza/kubeba madawa ya kulevya imefua dafu?

Sheria kali zinafanya kazi kwenye taasisi imara
 
Back
Top Bottom