Sheria ya kuruhusu wenye mimba kuendelea na masomo,je imejaribu kutazamwa kwa upande wa mtu aliyesababisha hiyo mimba?

Sheria ya kuruhusu wenye mimba kuendelea na masomo,je imejaribu kutazamwa kwa upande wa mtu aliyesababisha hiyo mimba?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Sheria ya kuruhusu wenye mimba kuendelea na masomo,je imejaribu kutazamwa kwa upande wa mtu aliyesababisha hiyo mimba?

Wakati huyo mwanafunzi analea, mimba yake akiwa darasani je, huyo aliyetungisha, mimba atakuwa wapi?

Sheria itaruhusu mwenye mimba kuendelea na Masomo kwa kujiamulia tu au kuna taratibu za kimahakama zitafuatwa kwanza?

Msababisha mimba yeye atakua wapi wakati huo?

Na kama ikijulikana msababisha mimba ni mwanafunzi mwenzake wa kiume na yeye ataruhusiwa kuendelea na Masomo?? Kama inavyoelezwa kwenye orodha ya haki za binadamu kwamba elimu ni haki ya mtoto.

Na ile sheria ya miaka 30 sasa ndio itaendelea kama vilevile au ndio imefikia kikomo?
 
Atakuwa jela (miaka 30)
Sasa hapa kuna haki gani inatendeka wakati watu walikubaliana. Mbona kama sheria inaegemea upande mmoja.
Assume aliyetungisha hiyo mimba naye nimwanafunzi, huoni kama nayeye kumfunga miaka 30 jela ni kumnyima haki yake ya kielimu ambapo ni kinyume na haki za binadamu??
 
Kutembea na mtu chini ya 18 years ni ubakaji, labda na wewe uwe under 18. So hupelekwi jela miaka thelathini sababu ya kubebesha mimba, bali sababu ya kubaka.
 
Mimi naona Sheria irekebishwe iangaliwe na upya kwakua hata aliesababisha mimba anahaki ya kupata elimu
 
Ningeshangaa sana Rais mwanamke kuendelea kugandamiza watoto wa kike.
Uwe unajenga hoja mkuu usiwe bendera fuata upepo tu. Umepewa akili zako zitumie vizuri. Kumpeleka jela aliyetungusha mimba kama ni mwanifunzi unahisi sio ukandamizaji??
 
Kwa shule nilizosoma, mkikamatwa na ikabainika bila shaka kwamba mmekula tunda (iwe serious au kimasihara) hapo hapo ni kwenda kuchukua mabegi yenu kwenda kwenu. Haufai tena kwa matumizi ya shule.

Sasa hapa mtu akiwa mjamzito ni ushahidi bayana kwamba huyu binti ametafuna tunda na adhabu iko wazi, kufukuzwa shule.

Sasa nnachotaka kuuliza ni Je, ile sheria ya awali ya ukikamatwa umekula tunda shule hauna tena inabaki pale pale au inarekebishwa?
 
Labda naomba kuuliza kwani akirudi Kama wale reseaters (QT) nayo si anakupa kapata elimu au elimu Ile haitambuliki??
 
Uwe unajenga hoja mkuu usiwe bendera fuata upepo tu. Umepewa akili zako zitumie vizuri. Kumpeleka jela aliyetungusha mimba kama ni mwanifunzi unahisi sio ukandamizaji??
Wapi nimesema kuwa kuwapeleka jela wajaza mimba siyo ukandamizaji?Kuna sehemu yoyote nimezungumza juu ya wajaza mimba?
 
Kuruhusu mwanafunzi aliyekwisha zaa kurudi shule hapo tumekosea (kwa maadili ya Kitanzania hapa tumeingia chaka) labda kama watarudishwa kwenye shule zao special kwa ajili ya wanafunzi wazazi ila kuchangamana na wale waliojitunza ni big no!!!

Au ikaziwe msababisha mimba ni jela maisha with no parole,vinginevyo tutoto twa form II tutajitegesha mimba kwa bodaboda vichwani vikiwa na mawazo ya kukaa bench mwaka ½ kulea kisha virudi shule huku boda wakikimbia,kizazi cha vijana kitazidi kuvurugika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwe unajenga hoja mkuu usiwe bendera fuata upepo tu. Umepewa akili zako zitumie vizuri. Kumpeleka jela aliyetungusha mimba kama ni mwanifunzi unahisi sio ukandamizaji??
Mwanafunzi wa kiume haendi jela kwa kumpa mimba mwanafunzi mwenzie, hii ni tangu zamani
 
Kwa Hali hii walimu wakware watapata pakupumzikia!Binafsi sikubaliani na Jambo hili kwasababu litawavuruga sana wanafunzi.Mzazi mwenye mtoto unamzuiaje kufanya tendo la ndoa?.Wakati hayo ni mahitaji ya mtu mzima?.
 
mtu aliyesababisha mimba kama ni mtu mzima sheria ilishawekwa tangu 1998 atashitakiwa kwa kosa kama la kubaka tu (statutory rape), ila kama ni mtoto mwenzie hata akishitakiwa hatapata kifungo cha ndani. kama una swali lingine uliza.
 
Kutembea na mtu chini ya 18 years ni ubakaji, labda na wewe uwe under 18. So hupelekwi jela miaka thelathini sababu ya kubebesha mimba, bali sababu ya kubaka.
sasa hapo kiongozi alietembea na mwenzake ni nan au kubakwa kupo upande mmoja?
 
Back
Top Bottom