Sheria ya kutokumshitaki Rais ndio Rushwa kubwa kuliko

Sheria ya kutokumshitaki Rais ndio Rushwa kubwa kuliko

Uhaini ni nini sheikhe?
UHAINI ni huo hapo chini
Raisi analindwa kutenda maovu yake dhidi ya wananchi kwamba akitaka kuchukuliwa hatua na wananchi waliokinai udhalimu wake eti yeye ndio anafanyiwa Uhaini wakati yeye ndio mwanzilishi iwa uhaini. Anayesababisha wananchi waingiwe na hasira ni rais, bunge na mahakama ambazo zenyewe zimepewa kinga kwamba ni sawa wawafanyiavyo wananchi ndio maana tunasema sheria ya kinga kwa raisi, makamu, waziri mkuu, jaji mkuu na spika iondoshwe ambapo 'automatically' kosa la uhaini litamgusa pia.

Huwezi kupindua nchi bila kuwa na kikundi cha kijeshi chenye silaha hao waliokamatwa wana kikundi gani chenye silaha?

(a) Article 39 (1) of the penal code states that anyone who is inside the United Republic or anywhere who tries to kill the president will have committed treason.
(b) Also, anyone who is inside the United Republic or anywhere and starts a war against the United Republic will have committed the crime of treason.
(c) Any person who is within the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or facilitates, incites, persuades, advises, regarding the death, disables, hinders, or imprisons the president will be guilty of treason.
( d ) Any person who is in the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or enables, incites, influences, or advises to remove the president from power illegally will have committed treason.
(e) Any person who is within the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or enables, incites, persuades, advises to deprive the president of the honor and title of the head of state, commander-in-chief, or leader of the government will have committed the crime of treason.
(f) Any person who is within the United Republic who builds, causes or facilitates, incites, persuades, advises to overthrow the government in power, threatens the government, parliament, or the courts will have committed the crime of treason.
 
Wanachofanyiwa kina Mwabukusi na wenzake kinaweza kikawa sio Sawa Mbele ya macho ya Haki lakini kikawa Sawa Mbele ya Sheria za Rushwa.

Kulingana na vifungu ulivyovitoa kuna vipengele hasa kipengele C kinachoweza kuwatia hatiani ikiwa waliwahi kutamka au kushawishi kuwa serikali iliyo madaraka ya Samia suluhu iondoshwe madarakani.
Kuhusu Haki ya sheria hiyo sasa hapo ndipo hoja yangu ilipo
 
Uchama sio mzuri.
Napenda nikijadili Jambo nijadili mada husika bila kuingiza uchama, udini au ukabila.
Ila sitazuia wanaopenda tofauti na Mimi.
Mara nyingi nimekuwa nikisema hapa jukwaani hii sheria ya rais kutoshitakiwa ndio sababu hasa ya taasisi zote za kimamlaka kuwa dhaifu. Hivi sasa amri kutoka juu ina nguvu kuliko katiba na sheria.

Sheria hii ya kutoshtakiwa kwa rais ndio imeweka nguvu zote, na kiburi chote kwenye kiti cha urais. Hapo ndio unapokuta mikataba ya kihuni, kuchezea chaguzi za nchi, hadi CCM wanasema ccm itawala milele maana wanajua mamlaka ya rais ambaye hashitakiwi itawabeba, na ndio kinachoendelea hadi hivi sasa. Taasisi zote za kimamlaka na mifumo yote imefunikwa na kinga hii ya rais kutoshtakiwa.

Ukweli mchungu wa kuweza kuondoa kosa hilo kubwa sana la kiutawala, inaweza kubadilishwa kwa kupatikana katiba mpya itakayoingia kinga ya mtu yoyote kutoshikiwa akiwa madarakani, au nje ya madaraka. Ila ukweli mchungu kuliko wote, hakuna uwezekano wa sheria hii kubadilishwa kwa katiba za maridhiano, bali lazima yatokee machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili katiba ya maoni halisi ya wananchi ifanyike bila kutoa upendeleo kwa yoyote, iwe chama, taasisi, vyombo vya ulinzi nk. Hakuna uwezekano wa kupatikana kwa amani katiba itakayotoa kushitakiwa kwa mtu yoyote ikiwemo rais, kwa majadiliano ya mabunge haya yanayoundwa kwa utashi wa rais, huku CCM wakiwa majority kwenye hayo mabunge hayo.
 
Hiyo sheria iondoshwe
 
SHERIA YA KUTOKUSHTAKIWA RAIS NDIO RUSHWA KUBWA KULIKO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Takukuru kazi yenu bado itakuwa ngumu ikiwa kuna sheria ambazo zinatoka Rushwa Kwa baadhi ya makundi ya Watu hasahasa viongozi.
Kuna Sheria na kuna Haki. Alafu kuna vyombo vya kusimamia sheria na Haki. Alafu muda huohuo kuna maadui wa Haki, Rushwa ikiwa mmoja wao.

Moja ya Sheria Mbaya zaidi kuliko, sheria yenye kutoa Rushwa, ni Ile inayosema Rais asishtakiwe. Hakuna Rushwa kubwa kama hiyo..

Hatuwezi sema Nchi inaongozwa Kwa Haki ilhali kuna sheria zinazonyima Haki ya usawa Mbele za sheria. Watu wote wapo Sawa Mbele ya sheria ingawaje haimaanishi kuwa wanalingana. Same but not similar.

Rais hawezi sema yeye ni MTU wa Haki au anapenda Haki huku akijua kuwa kuna Sheria zimempa Rushwa ya kutotendewa Haki kama wengine pale anapokosea.

Rais mpenda Haki lazima arekebishe hicho kipengele cha sheria zilizoadui na Haki kama hiyo ya kumkingia kifua asishtakiwe.

Sheria hiyo ndio msingi Mkuu wa Ufisadi, ukandamizaji, udikteta, ubabe usio na kichwa wala miguu.

Wanasheria, wapenda Haki na watu wote waungwana wanaowajibu wa kuifuta hiyo sheria Kwa gharama yoyote Ile.

Mahakama na Bunge, na vyombo vingine vya serikali vitakuwa katika hatari ya kufanya Ufisadi na Rushwa kupitia sheria hizi za Rushwa.

Mahakama haiwezi kutenda HAKI ikiwa kuna Watu ndani ya taifa hawashtakiwi. Itatenda Haki kulingana na utashi wa viongozi na sio kulingana na sheria za Haki zisemavyo.

Nilimsikia, Bw. Rostam akizungumzia kuhusu Mahakama kupokea maelekezo Kutoka juu Hali inayopingisha Haki. Hilo wala halihitaji ushahidi zaidi ya ule ushahidi wa sheria ya ajabu na ya Rushwa inayonyima Haki Kwa Rais na sasa baadhi ya watendaji wa serikali kushtakiwa.

Mahakama na vyombo vyote vya Haki na sheria haviwezi kukataa tuhuma hiyo Wakati sheria ya Rushwa ya kutoshtaki Rais na Baadhi ya watendaji wa serikali ingalipo. Uwepo wa sheria hiyo inathibitisha tuhuma hiyo ni kweli na wala sio tuhuma.

Fikiria Polisi au vyombo vya usalama ambavyo vitaweza kuvunja sheria Kwa ukaidi, ujeuri na Kiburi kwa kile wakiitacho kupewa maelekezo Kutoka juu. Juu walipo wasioshtakiwa, ambao Kwa tafsiri nyepesi wenye ruhusa ya kuvunja sheria ambazo waliapa kuzitii na kuzitumikia. Jambo la aibu ndani ya jamii yetu.

Sheria ya Rushwa(sheria ambazo ni adui WA Haki) kama ya kutoshtakiwa Rais, ndio unaleta lile genge la wahuni lisemalo; unanijua Mimi ni Nani?" Genge hilo kupitia sheria hiyo haliwezi kufanywa chochote.

Hata Huko Mahakamani kuwe na Mahakimu na majaji wenye weledi na uadilifu lakini hawawezi kufurukuta na watakuwa vibaraka wa wale wasioshtakiwa tuu. Watake wasitake.

Rais akishakuwa automatically tutaondoa vibaraka na Machawa ambao wanafanya hivyo ili kujikinga na hatari za kijinai zitakazojitokeza, watatumia kete Yao muhimu ya MTU asiyeshtakiwa kuishinikiza Mahakama au vyombo vya Dola.

Sheria hiyo inamshawishi Rais na viongozi wake kufanya Ufisadi Kwa sababu wanajua hawatafanywa chochote. Sio ajabu kupitia sheria hiyohiyo viongozi Baada ya kuingia madarakani tuu miaka Mitano ni mingi unawakuta wakiogelea katika bahari ya ubilionea ambao moja Kwa moja ni Ufisadi unaotokana na sheria za Rushwa zinazoiminya Haki.

Sheria hiyo inaminya Haki zingine kama Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru WA kutoa Maoni. Vyombo vya habari huchagua habari za kurusha Kwa kuhofia kukutana na fagio la chuma la Fisadi, Kwa sababu Rais asiyeshtakiwa anauwezo wa kukifungia chombo cha habari na ikiwezekana kuwatia matatani Wahusika hata kama Hawana kosa.

Sheria hiyo ni Mbaya wala hakuna Lugha nzuri ya kuielezea. Ukiita ni sheria ya hovyo hautakuwa umekosea. Ni yahovyo Kwa sababu ni adui WA Haki. Na MTU ambaye ni adui WA Haki ni MTU wa hovyo.

Logically, MTU anayeshtakiwa hawezi kumfanya lolote MTU ambaye hashtakiwi. Kumaanisha anayeshtakiwa atakuwa kibaraka au mtumwa wa asiyeshtakiwa.

Sheria ya Rais hashtakiwi ni sheria inayounda magenge ya wahalifu ambao hawaguswi wala kugusika kisheria. Ni kutengeneza na kuwekea mazingira familia Fulani ambazo zitabahatika kushika ngazi ya Urais kutogusika.

Sheria hiyo pia inajenga Utumwa Kwa Rais Mpya atakayeingia madarakani kwani hatafanya kazi Kwa Haki hata iweje labda aifute hiyo sheria. Rais anayeingia madarakani tayari anaandaliwa kuwa Fisadi na MLA Rushwa. Atakuta madudu ya mwenzake (Ma/ Rais w/aliopita) na marafiki zake, atashindwa kuwashughulikia Kwa sababu tayari kuna sheria inayowalinda, na endapo atathubutu kushughulikia angalau hata marafiki wa Rais aliyepita basi automatically atakutana na anguko ambalo hatanyanyuka Kamwe.

Sheria hii inafanya shirika la Usalama wa taifa kuwa shirika la usalama la Watu binafsi ambao wameshakuwa viongozi wa nchi. Hii inawapa tabu Vijana wa Usalama kutofanya kazi Yao Kwa ufanisi kwani badala ya kuitumikia nchi watakuwa wanatumikia Mabwana zao. Automatically huwezi kuwa na Uzalendo kwenye taifa ambalo Rais hashtakiwi. Hakunaga kitu kama hicho.
Utakuwa mzalendo labda ukiwa pekeako Huko kwenye familia yako lakini ukishakuja kitaifa huku utasombaa na mfumo wa Rushwa na kifisadi. Na endapo utaleta fyokofyoko basi utajikuta kwenye matata Makubwa.

Wanasema Haki haipotei lakini kimsingi Haki inapotea ikiwa waendesha nchi watakuwa wanaongozwa na sheria za Rushwa. Mara ngapi umesikia Watu kadhaa wakinyimwa Haki zao iwe za kisiasa, kijamii au kiuchumi, nini kilitokea?

Haki inapotea ikiwa jamii itakubali kuongozwa na viongozi wala Rushwa au wanaopewa Rushwa na sheria za hovyo.

Nilisikia habari za Bandari, viongozi wanalalamika kuwa Hakuna utendaji mzuri wenye ufanisi ndani ya Bandari. Wakaenda mbali zaidi wakasema, pale bandarini mbali na Teknolojia kuwa ndogo lakini changamoto kubwa ni Rasilimali Watu kuwa majizi, mafisadi na wala Rushwa hali inayozorotesha ufanisi wa Bandari.

Lakini lazima tujiulize, kwani hakuna sheria za kudili na watu wanaohujumu ufanisi wa Bandari? Jibu ni zipo sheria lukuki na zenye adhabu stahiki. Lakini tatizo kubwa ni lilelile, huwezi muadhibu au sheria haiwezi kufanya kazi Kwa Watu ambao wamejikinga na mwamvuli wa viongozi wasioshtakiwa.

Hivi utawezaje kumshtaki MTU ambaye unajua anaurafiki na Rais au kiongozi asiyeshtakiwa. Hata Hakimu au Jaji utamtia majaribuni. Ni ngumu Mno.

Mara ngapi umesikia wafanyabiashara au matajiri wakijiunga na vyama vya Siasa Kwa kufuata mkumbo ilimradi kujiwekea Usalama wa biashara zao. Huoni tatizo hapo? Huoni Rushwa hapo?

Nchi haiwezi kuendelea hata siku moja ikiwa sheria zake hajalenga kutoa Haki. Ni sheria zilizolenga kutoa Rushwa ambayo ni adui WA Haki.

Niliona juzi TBC ikimuonyesha Mkurugenzi wa Shirika Hilo(TBC) Dkt Ayoub Rioba akiwa visiwani Zanzibar katika mchakato WA kuchukua Maoni ya wananchi katika tume ya kufanya maboresho ya utoaji wa haki Mahakamani na vyombo kama polisi na upelelezi(kama sijakosea). Ni hatua nzuri. Lakini itakuwa ni kazi Bure na upotezaji wa Pesa ikiwa mzizi Mkuu wa Haki hautaanzia juu kabisa walipo viongozi.

Sio kwamba Watu hawawezi tenda Haki Mahakamani, sio kwamba polisi hawawezi kufanya kazi Kwa ufanisi. Tatizo linaanzia juu kushuka Chini. Juu pakiwa Safi moja Kwa moja Chini kutakuwa Safi.

Ikiwa kuna sheria inamtetea Rais au kiongozi asishtakiwe hapo tafsiri yake hata baadhi ya watendaji wake hawatashtakiwa hata wakivunja Haki Kwa sababu wengi watapokea maelekezo Kutoka juu. Pia Boss lazima atetee watumishi Wake kama watumishi watakavyomtetea kwenye nyakati ngumu.

Pendekezo kuu Kutoka Kwa Taikon Master ni kuzichunguza sheria za Rushwa ikiwemo Hii ya kutoshtakiwa Kwa Rais na Baadhi ya viongozi, zifutwe. Kisha Watu wote wawe chini ya sheria. Alafu muone kama Maendeleo hayatakuja.

Muone kama kuna Panya buku atakayeiba Pesa za Umma.

Taikon Acha nipumzike sasa. Leo sitaki maswali.
Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nakubaliana naww, cha kushangaza kbs hata yule mzalendo nae akawaongezea kinga na wengine!! Hapo ndipo niliamin hakuna mzalendo humo!!!
 
Wenzetu wameendelea kwa sababu ya mifumo Yao inawabana viongozi wao kutokuwa wapumbavu.
Watawala wa kiafrika hawana mfumo unaowabana wa kuwapa hofu ya kuwatendea haki wananchi
 
Hiyo Sheria ya kutomshtaki Rais akiwa madarakani ina mantiki Kwa nchi ambazo mifumo/taasisi bado hazijakaa vizuri. Hebu fikiria nchi kama yetu nani aanzishe uchunguzi dhidi ya rais aliyepo madarakani!

Pia imagine wahafidhina Kila leo wanamplekea rais hati ya mashtaka Kwa hili au lile...Hawa jinai Hawa madai!
N.b. nchi nyingi sio jambo rahisi kumshtaki Rais.
 
"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake";Mwl.Nyeree

Tanzania ina viongozi wapumbavu,ambao hurejewa na akili timamu baada ya vipindi vyao vya utawala kupita,ukitaka kuthibitisha hili ni kupitia vitabu vyao.

Siku zote mtu asiye tenda haki hawezi kuwa mtenda haki na hawezi kuzungukwa na watenda haki,bali wasio tenda haki maana "ndege wanao fanana huruka pamoja";hili ndo lilipo Tanzania. Viongozi wamejifanya miungu watu (semi-gods),kwa kujiona wao ndio wenye wajibu wa kutoa haki kwa watu na mbaya zaidi ujinga na upumbavu wa watu wameaminishwa kupata haki ni hisani.

Kongole Taikon
 
Hii sheria ya kutokushitakiwa kwa rais ipo tu kwa nchi masikini ambapo sheria zilitungwa na wabunge wengi wao mizigo.huwezi kukuta sheria ya kipumbavu namna hiyo kwenye nchi zilizoendelea.Ndiyo maana mambo ya hovyo yanafanywa na awamu ya sita kwa kuwa wanajua hakuna wakumshitaki
 
Na waasisi wa sheria hizi huitwa wazalendo na walionekana kama watu wenye akili kubwa.
 
Hakika umenena.

Ndiyo maana hufanya watakavyo na watoto na ndugu zao .

Afrika kusini walishatoka kwenye huo ujinga.
 
Afrika kusini ukiapishwa kuwa Raisii sio guarantee kuwa utakuwa Rais hadi muhura wako uishe [emoji108]

Wakiona nyendo zako za mashaka wanaku terminate immediately [emoji108]

Na wanakushitaki.

Na mahakama zao ziko huru na imara
 
Siku hizi hawaoni haya kabisa!

Hadi wakwe zao , wapwa, jamaa n.k.
 
Back
Top Bottom