Sheria ya kutokumshitaki Rais ndio Rushwa kubwa kuliko

Uhaini ni nini sheikhe?
UHAINI ni huo hapo chini
Raisi analindwa kutenda maovu yake dhidi ya wananchi kwamba akitaka kuchukuliwa hatua na wananchi waliokinai udhalimu wake eti yeye ndio anafanyiwa Uhaini wakati yeye ndio mwanzilishi iwa uhaini. Anayesababisha wananchi waingiwe na hasira ni rais, bunge na mahakama ambazo zenyewe zimepewa kinga kwamba ni sawa wawafanyiavyo wananchi ndio maana tunasema sheria ya kinga kwa raisi, makamu, waziri mkuu, jaji mkuu na spika iondoshwe ambapo 'automatically' kosa la uhaini litamgusa pia.

Huwezi kupindua nchi bila kuwa na kikundi cha kijeshi chenye silaha hao waliokamatwa wana kikundi gani chenye silaha?

(a) Article 39 (1) of the penal code states that anyone who is inside the United Republic or anywhere who tries to kill the president will have committed treason.
(b) Also, anyone who is inside the United Republic or anywhere and starts a war against the United Republic will have committed the crime of treason.
(c) Any person who is within the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or facilitates, incites, persuades, advises, regarding the death, disables, hinders, or imprisons the president will be guilty of treason.
( d ) Any person who is in the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or enables, incites, influences, or advises to remove the president from power illegally will have committed treason.
(e) Any person who is within the Republic of the Union or anywhere who creates, causes or enables, incites, persuades, advises to deprive the president of the honor and title of the head of state, commander-in-chief, or leader of the government will have committed the crime of treason.
(f) Any person who is within the United Republic who builds, causes or facilitates, incites, persuades, advises to overthrow the government in power, threatens the government, parliament, or the courts will have committed the crime of treason.
 

Wanachofanyiwa kina Mwabukusi na wenzake kinaweza kikawa sio Sawa Mbele ya macho ya Haki lakini kikawa Sawa Mbele ya Sheria za Rushwa.

Kulingana na vifungu ulivyovitoa kuna vipengele hasa kipengele C kinachoweza kuwatia hatiani ikiwa waliwahi kutamka au kushawishi kuwa serikali iliyo madaraka ya Samia suluhu iondoshwe madarakani.
Kuhusu Haki ya sheria hiyo sasa hapo ndipo hoja yangu ilipo
 
Uchama sio mzuri.
Napenda nikijadili Jambo nijadili mada husika bila kuingiza uchama, udini au ukabila.
Ila sitazuia wanaopenda tofauti na Mimi.
Mara nyingi nimekuwa nikisema hapa jukwaani hii sheria ya rais kutoshitakiwa ndio sababu hasa ya taasisi zote za kimamlaka kuwa dhaifu. Hivi sasa amri kutoka juu ina nguvu kuliko katiba na sheria.

Sheria hii ya kutoshtakiwa kwa rais ndio imeweka nguvu zote, na kiburi chote kwenye kiti cha urais. Hapo ndio unapokuta mikataba ya kihuni, kuchezea chaguzi za nchi, hadi CCM wanasema ccm itawala milele maana wanajua mamlaka ya rais ambaye hashitakiwi itawabeba, na ndio kinachoendelea hadi hivi sasa. Taasisi zote za kimamlaka na mifumo yote imefunikwa na kinga hii ya rais kutoshtakiwa.

Ukweli mchungu wa kuweza kuondoa kosa hilo kubwa sana la kiutawala, inaweza kubadilishwa kwa kupatikana katiba mpya itakayoingia kinga ya mtu yoyote kutoshikiwa akiwa madarakani, au nje ya madaraka. Ila ukweli mchungu kuliko wote, hakuna uwezekano wa sheria hii kubadilishwa kwa katiba za maridhiano, bali lazima yatokee machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili katiba ya maoni halisi ya wananchi ifanyike bila kutoa upendeleo kwa yoyote, iwe chama, taasisi, vyombo vya ulinzi nk. Hakuna uwezekano wa kupatikana kwa amani katiba itakayotoa kushitakiwa kwa mtu yoyote ikiwemo rais, kwa majadiliano ya mabunge haya yanayoundwa kwa utashi wa rais, huku CCM wakiwa majority kwenye hayo mabunge hayo.
 

Hiyo sheria iondoshwe
 
Nakubaliana naww, cha kushangaza kbs hata yule mzalendo nae akawaongezea kinga na wengine!! Hapo ndipo niliamin hakuna mzalendo humo!!!
 
Wenzetu wameendelea kwa sababu ya mifumo Yao inawabana viongozi wao kutokuwa wapumbavu.
Watawala wa kiafrika hawana mfumo unaowabana wa kuwapa hofu ya kuwatendea haki wananchi
 
Hiyo Sheria ya kutomshtaki Rais akiwa madarakani ina mantiki Kwa nchi ambazo mifumo/taasisi bado hazijakaa vizuri. Hebu fikiria nchi kama yetu nani aanzishe uchunguzi dhidi ya rais aliyepo madarakani!

Pia imagine wahafidhina Kila leo wanamplekea rais hati ya mashtaka Kwa hili au lile...Hawa jinai Hawa madai!
N.b. nchi nyingi sio jambo rahisi kumshtaki Rais.
 
"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake";Mwl.Nyeree

Tanzania ina viongozi wapumbavu,ambao hurejewa na akili timamu baada ya vipindi vyao vya utawala kupita,ukitaka kuthibitisha hili ni kupitia vitabu vyao.

Siku zote mtu asiye tenda haki hawezi kuwa mtenda haki na hawezi kuzungukwa na watenda haki,bali wasio tenda haki maana "ndege wanao fanana huruka pamoja";hili ndo lilipo Tanzania. Viongozi wamejifanya miungu watu (semi-gods),kwa kujiona wao ndio wenye wajibu wa kutoa haki kwa watu na mbaya zaidi ujinga na upumbavu wa watu wameaminishwa kupata haki ni hisani.

Kongole Taikon
 
Hii sheria ya kutokushitakiwa kwa rais ipo tu kwa nchi masikini ambapo sheria zilitungwa na wabunge wengi wao mizigo.huwezi kukuta sheria ya kipumbavu namna hiyo kwenye nchi zilizoendelea.Ndiyo maana mambo ya hovyo yanafanywa na awamu ya sita kwa kuwa wanajua hakuna wakumshitaki
 
Na waasisi wa sheria hizi huitwa wazalendo na walionekana kama watu wenye akili kubwa.
 
Hakika umenena.

Ndiyo maana hufanya watakavyo na watoto na ndugu zao .

Afrika kusini walishatoka kwenye huo ujinga.
 
Afrika kusini ukiapishwa kuwa Raisii sio guarantee kuwa utakuwa Rais hadi muhura wako uishe [emoji108]

Wakiona nyendo zako za mashaka wanaku terminate immediately [emoji108]

Na wanakushitaki.

Na mahakama zao ziko huru na imara
 
Siku hizi hawaoni haya kabisa!

Hadi wakwe zao , wapwa, jamaa n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…