VeronicaAmadu
JF-Expert Member
- May 4, 2011
- 310
- 380
50.-(1) Bila kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha faini kwa kosa hilo.
(2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa -
(a) ya maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1);
(b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na
(c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu.
Mamlaka ya kutengeneza Kanuni
51. Waziri anaweza kutunga Kanuni kuhusiana na jambo lolote ambalo linatakiwa kuainishwa na Sheria hii au ambalo ni la umuhimu au uharaka kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii.
Unyanyasaji kwa kupitia mtandao
23.-(1) Mtu hataanzisha au kukadimisha mawasiliano yoyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la kurubuni, kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi ya hisia.
(2) Mtu akataye kiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Lakini mkuu, katika ile sheria ya taarifa za uongo mimi binafsi sioni kama kuna tatizo.
Kumekuwa na upotoshaji mwingi sana kupitia mitandao nadhani hii sheria itasaidia kidogo
Watawala wenyewe wanapotosha mangapi kwa maslahi yao ya kisiasa?Ukiwa sio muongo, mdaku sheria ni murua Kabisa... Tutaanza kusoma Vitu vya ukweli sasa sio mazagazaga. Sometimes we waste a lot of time kusoma maujinga ambayo mtu Hana hakika nayo.
Lakini mkuu, katika ile sheria ya taarifa za uongo mimi binafsi sioni kama kuna tatizo.
Kumekuwa na upotoshaji mwingi sana kupitia mitandao nadhani hii sheria itasaidia kidogo
Huyo ndo makamba mchumia njaa anayetaka uraisi?huu ni upuuzi wa kiasi cha juu sana ukipitisha muswada namna hii
Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,
Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,
Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?