Sheria ya makosa ya shule inasemaje mwanafunzi anapokamatwa na simu?

Sheria ya makosa ya shule inasemaje mwanafunzi anapokamatwa na simu?

jangoma

Member
Joined
Sep 24, 2023
Posts
64
Reaction score
216
Je, simu hiyo anapaswa kurudishiwa, au kuitaifisha au kufanya nini? Tafadhali nijibu kulingana na sheria inavyosema na sio kwa kuzingatia maadili.
 
Mtoto wangu wanaruhusiwa kwenda na simu shule ila anaikabidhi kwa buser mpaka siku anafunga
 
Shule Husika Wakati Unampeleka Mtoto Ulipewa Sheria Za Hapo
Sasa Inategemea Upande Alipo Zinasema Itarudishwa/Kutaifishwa
Shule Nyingine Kukutwa Na Line, Simu, Chaji
Mwanafunzi Anaondolewa Bila Kurudishiwa Kifaa
 
Sheria zinatofautiata kati ya shule na shule.
Kuna shule kongwe ya bording ya serikali, simu NIMARUFUKU.
Ukikamatwa nayo kuna bonge la adhabu na simu ndio huipati tena.
 
Makosa yanaweza kusabaisha mwanafunzi kifukuzwa shule: 1. Kuwa na simu au kifaa chochote cha simu
2. Kupigana au kupiga
3. Kuharibu mali ya umma Kwa maksudi
4. Kugoma adhabu
5. Kupata uja uzito/kusabaisha uja uzito/ kutoka mimba.....
 
hiyo kupata ujauzito sasahivi hawafukuzwi, wana postpone wanarudi waka unaofuata baada ya kujifungua.
 
Nafikiri inategemea na sheria za shule husika.

Adhabu ni aidha kutakiwa kumwita Mzazi/Mlezi atoe maelezo kuhusu hiyo simu...si bure ni mzazi anampa na kuna uwezekano akaondoka na Mwanae, Kufukuzwa shule, kupewa barua ya uhamisho yaani kutafuta shule nyingine au kuchapwa na kupewa adhabu zingine hapo shuleni ....!

So ni maamuzi ya Uongozi wa shule ndio utaangalia
 
Nilikamatwa na sim shule form 3 headmaster akanihamisha shule ndani ya masaa 74 chini ya uangalizi wa jeshi la polis ile shule nyoko..
 
Je, simu hiyo anapaswa kurudishiwa, au kuitaifisha au kufanya nini? Tafadhali nijibu kulingana na sheria inavyosema na sio kwa kuzingatia maadili.
Simu ipondwe na nyundo na mwanafunzi akakae nyumbani siku 21 kisha arudi na Mzazi wake na apatiwe adhabu ya kuchimba visiki[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Je, simu hiyo anapaswa kurudishiwa, au kuitaifisha au kufanya nini? Tafadhali nijibu kulingana na sheria inavyosema na sio kwa kuzingatia maadili.
Me nilikamatwa na cm bwenin nilipokua kidato Cha 3
Nilrudshwa nyumban na barua ya kuludi na mzazi na faini 50k

Sitosahau,walimu walikua wakisoma msg kwenye cm mbele ya baba yangu zile msg zile, walimu walimwambia baba,unasomesha mke wa mtu,nilipigwa na baba yaan walimu ndo kuja kunisaidia Mzee inatosha,

Ukweli ni kwamba ILE cm n yangu ila nilikua siitumii mimi walikua wanatumia wenzangu,mimi sikua babe MIAKA ile
 
Inategemea na sheria zilizowekwa na uongozi wa shule husika.

Kuna baadhi ya shule mwanafunzi akikamatwa na simu, simu inasambaratishwa mbele ya wanafunzi wote na shule ndo inaishia hapo.

Kuna baadhi shule inataifisha na mwanafunzi anapatiwa tu adhabu.

Nyingine inachukuliwa kwa muda siku ya kufunga shule mwanafunzi anakabidhiwa arudishe nyumbani.
 
Me nilikamatwa na cm bwenin nilipokua kidato Cha 3
Nilrudshwa nyumban na barua ya kuludi na mzazi na faini 50k

Sitosahau,walimu walikua wakisoma msg kwenye cm mbele ya baba yangu zile msg zile, walimu walimwambia baba,unasomesha mke wa mtu,nilipigwa na baba yaan walimu ndo kuja kunisaidia Mzee inatosha,

Ukweli ni kwamba ILE cm n yangu ila nilikua siitumii mimi walikua wanatumia wenzangu,mimi sikua babe MIAKA ile
Duh pole sana ila ulifanya kosa baya dana.mwisho wa siku simu ulirudishiwa au ilitaifishwa??
 
Je, simu hiyo anapaswa kurudishiwa, au kuitaifisha au kufanya nini? Tafadhali nijibu kulingana na sheria inavyosema na sio kwa kuzingatia maadili.
Kila shule ina joining instructions zake. Nina hakika masharti kuhusu simu yapo bayana.
Kimantiki mwanafunzi kukutwa na simu shuleni,ni kosa la mzazi aliyemnunulia.
Shule zingine mwanafunzi huamriwa aipasue kwa jiwe,nyundo,nk. Zingine hutaifisha. Zingine huhifadhi hadi atakaopondoka kwenye shule hiyo.
 
Back
Top Bottom