Mkuu nipo idara husika, aina ya kesi yako ina changamoto kwa kweli.
Niseme tu kutokujua idadi sahihi ya mali ulizonazo sio kitu. Mahakama ikitaka kujua unachomiliki itajua tu.
Kisheria yule bado ni mkeo hata baada ya kumuachia kila kitu ukaja kuanza maisha mapya na kumiliki hizo mali ulizonazo bado kuna gawio linalomuhusu kisheria kutoka kwenye hizo mali ulizo nazo.
Ulifanya kosa kama kumpa talaka ilibidi umpe wakati ule ambao ulimuachia kila kitu.
Maswali ya kujiuliza?
Je, Wakati unamuachia kila kitu uliandikishana nae au ulifanya kumsusia?
Mahakama haiwezi kutambua vitu ulivyomuachia kama mgao wa mlichochuma mkiwa pamoja ikiwa ulimuachia kienyeji.
Inahitaji upate mtu wa kukutetea ila kisheria kesi yako inabidi ianzie mahakama ya mwanzo ambayo huwaga inatakiwa muhusika awepo si muwakilishi na hata wakili hatakiwi.
Endapo kesi ya ikaisha na huyo mwanamke akashinda utahitaji kukata rufaa kwenda Mahakama ya wilaya husika ambapo hapo una uwezo wa kumuajiei wakili atakaeisimamia hiyo kesi.
Ila mara vipengele vingi kwenye sheria ya ndoa vinam,beba mwanamke hasa ikiwa mna watoto mliozaa pamoja.