well, kisheria ni kwamba kuanzia mahakama kuu kuja mpaka mahakama ya mwanzo zote zina uwezo wa kusikiliza kesi za talaka na migawanyo ya mali, na mawakili wanaweza kwenda kuwateteni nyie wataliki kuanzia mahakama ya wilaya kuja mahakama kuu.
sasa hakuna ndoa itakayo vunjwa kama haijapitia baraza la ndoa la kata, kwaio kwenye baraza huko mtathibitishwa kwamba sasa hamuwezi kua pamoja mnatakiwa muende mahakamani mkavunjiwe ndoa na mali zigawanywe rasmi. sijui mkeo aliwezaje kwenda kwenye baraza mwenyewe na akapitishiwa kua sasa aende mahakama kuu ku process talaka, labda ulipotea kwa miaka zaidi ya mitano bila kujulikana uko wapi then waka assume umekufa 'pressumption of death'.
usiogope, mali ulizo zipata sasa ukiwa hauko na uyo mwanamke ni zako na haziwezi kuhesabiwa kama ni matrimonial properties, sheria ya ndoa ina ruhusu wana ndoa kua na mali zao apart bila shida na hazitousishwa na maswala yao ya ndoa, na vile vile endapo kutatolea mgawanyo wa mali, mali zitakazo gawanywa ni zile ambazo mlizipata wakati mkiwa wote kwenye ndoa na hapa itaku favor wewe zaidi ambae ukiamua unaweza kudai mgawanyishwe mali, huku hizi zako za sasa za hapa dar zikiwa safe bila shaka yoyote.
mali ulizo nazo sasa ni zako, ulijitaftia mkiwa mko separate kitu ambacho sheria ya ndoa inakijua.
wewe kutokuwepo nchi hio siku kesi haiwezi kuamuliwa exparte(upendeleo wa kuskilizwa kwa mtu mmoja) ila itahairishwa tu na useme siku utakayo kuwepo, lakin pia unaweza ajili mwanasheria akawa ana kuwakilisha au unaweza mpa mtu nguvu kwa kutumia power of attorney na mambo yakaenda vizuri tu.
shida sasa na ubaya watu wa humu jf tunawashauri kweli, tatizo hamletagi mrejesho wala hamtoi ata hela ya bia nyie mpo tu na kusema ahsante basi wakati maarifa haya ni mazito tunayo wapeni.
wakili.