Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

KWAKO .....
YAH: Kuvunja Mahusiano.
Mimi Karungu Yeye.....Niliyekuwa na Mahusiano na Bibi.Mtembezi Mgawaji....Nathibitisha kwamba kuanzia leo tarehe 17./07/1980 Nimevunja rasmi Mahusiano na Wewe.
Nakutakia Safari Njema

Saini:...........
Saini ya Shahidi:.......
Tarehe:.../.../....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sio kweli hapa umeongea vitu usivyovijua, soma text inayofuata
 
well, kisheria ni kwamba kuanzia mahakama kuu kuja mpaka mahakama ya mwanzo zote zina uwezo wa kusikiliza kesi za talaka na migawanyo ya mali, na mawakili wanaweza kwenda kuwateteni nyie wataliki kuanzia mahakama ya wilaya kuja mahakama kuu.

sasa hakuna ndoa itakayo vunjwa kama haijapitia baraza la ndoa la kata, kwaio kwenye baraza huko mtathibitishwa kwamba sasa hamuwezi kua pamoja mnatakiwa muende mahakamani mkavunjiwe ndoa na mali zigawanywe rasmi. sijui mkeo aliwezaje kwenda kwenye baraza mwenyewe na akapitishiwa kua sasa aende mahakama kuu ku process talaka, labda ulipotea kwa miaka zaidi ya mitano bila kujulikana uko wapi then waka assume umekufa 'pressumption of death'.

usiogope, mali ulizo zipata sasa ukiwa hauko na uyo mwanamke ni zako na haziwezi kuhesabiwa kama ni matrimonial properties, sheria ya ndoa ina ruhusu wana ndoa kua na mali zao apart bila shida na hazitousishwa na maswala yao ya ndoa, na vile vile endapo kutatolea mgawanyo wa mali, mali zitakazo gawanywa ni zile ambazo mlizipata wakati mkiwa wote kwenye ndoa na hapa itaku favor wewe zaidi ambae ukiamua unaweza kudai mgawanyishwe mali, huku hizi zako za sasa za hapa dar zikiwa safe bila shaka yoyote.

mali ulizo nazo sasa ni zako, ulijitaftia mkiwa mko separate kitu ambacho sheria ya ndoa inakijua.

wewe kutokuwepo nchi hio siku kesi haiwezi kuamuliwa exparte(upendeleo wa kuskilizwa kwa mtu mmoja) ila itahairishwa tu na useme siku utakayo kuwepo, lakin pia unaweza ajili mwanasheria akawa ana kuwakilisha au unaweza mpa mtu nguvu kwa kutumia power of attorney na mambo yakaenda vizuri tu.


shida sasa na ubaya watu wa humu jf tunawashauri kweli, tatizo hamletagi mrejesho wala hamtoi ata hela ya bia nyie mpo tu na kusema ahsante basi wakati maarifa haya ni mazito tunayo wapeni.


wakili.
 

Hahahahaha bos kuna mwanasheria alinifata dm akanishaur vzr ishu inaendelea vzr soon talaka itatoka na ntampa soda usijal
 


Ndio mana napenda kuoa mwanamke aliyesoma sheria ili niwe napata mambo matamu tamu kama haya
 
Mkuu nitoke nnje ya mada kidogo.

Ilikuchukua muda gani mpaka ukasimama tena kiuchumi,
Huko dar ulienda kufungua biashara au ulitegemea ajira..

Ikitokea mkeo ameolewa na mtu mwingine roho haitakuuma??

Ikitokea umeenda kuangalia mtoto ukiona mkeo kapendeza hautatamani kupasha kipolo??

Ni nini hasa kilichosababisha mkatengana na mke wako,usaliti? Dharau au kiburi cha mke wako baada ya kupata kazi yenye mshahara mkubwa.

Unatuambia nini sisi vijana ambao bado hatujaoa
Tuoe mwanamke wa aina gani
 
Mwanamke akikukatalia kwamba mtoto sio wa kwako nawewe unataka kumchukua ili uishi naye je sheria inasemaje..??
Kumbuka huyo mtoto hujawai kumlea wala huyo mwanamke hujawai kuishi naye zaidi ya kumpa mimba tu
 

Mahakama inatambua ndoa ya watu walioishi pamoja kuanzia miaka miwili na jamii inayowazungua wawe wanatambua kwamba nyie ni mke na mume.

Kwaiyo kama mnataka kutengana ni vizuri mkaenda makahamani mkatengana na kugawana mali na kupewa maelekezo jinsi ya kulea watoto kama wapo? Haya yote yatafanyika kwa maandiashi na kuhusu mali mtagawana kwa kadri kila mmojawenu alivyoshiriki
 
Kuvunja ndoa mwambie mwenzio humtaki, humpendi sababu ni feki. Hana sura nzuri hana sifa. Baada ya hayo yeye ndio atafuta njia ya kuivunja ndoa yenu, asipoivunja yeye wewe usihangaike.

Kwa nini ni rahisi kuoana na ngumu kuachana?
 

Shukrani
 
Pamoja na sheria za kuvunja ndoa kuwepo sishauri wana ndoa kuvunja ndoa zao.Ndoa zinahitaji uvumilivu sana.Kuna dhehebu fulani wao wanasema ndoa ni nyumba yenye mlango mmoja tu wa kuingilia,hakuna mlango wa kutoka nje!
Mlango Wa kutokea Upo n uamuz wako tu!! Soma Kumbukumbu la Torati 24:1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hasa ukizingatia kwamba ndoa inafungishwa na mawakala tu wanaoganya kazi ya Mungu wakati huohuo wakiwa ni binadam wenye milango ya faham ambao wanaweza kudanganywa vzuri sana. Ndoa ingekua perfect kama Mungu mwenyewe angesimama kufungisha, la sivyo wanadamu waweza ungisha ndoa bado ikawa batili (maana yake angesimama Mungu mwenyewe asingefungisha).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaweza fungua shauri la kuomba mgawanyo wa mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…