Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mkuu kwani lazima uwe na hatu ya usuruhisho ndo ukubariwe kufungua shauri mahakamani? Ikiwa mwenza wako hakutaka usuruhisho katoroka na hataki kusuruhishwa inakuwaje ? Mahakama inaweza kupokea ombi la taraka?

Ikitokea hali hiyo hapo ndiyo huwa na urahisi wa mahakama kutoa talaka!
Ikithibitika amekutelekeza yani shukuru Mungu maana hapo kupata talaka ni rahisi sana kuliko vinginevyo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 19:9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Wewe umeelewaje hayo maandiko? Wengi wameyakariri tu!
Hapo Maana yake pale itakapothibitika pasipo shaka kuwa mwanandoa mmoja au wote kuwa wamefanya uasherati maana yake kuachana ni ruksa na kwenda kuolewa na mtu mwingine


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ufafanuzi wako . Hebu nisaidie hili kwa zaidi ya Mara 3 make wangu ameondoka nyumbani pasipo kuaga na amekaa huko kwa zaidi ya Sikh 10 bila hata mawasiliano .Aliporudi akajitenga na chumba hata alipokuwa akilala sipajui kwa zaidi ya week 2 . Kimaadili ya ndoa na uhusiano mm nimechukuliabkuwa this is maximum provocation that means uhusiano hapa hautengamani maana ndani yake kumejaa.dharau. To that extent nilitoa talaka
Je hii talaka kwa ndoa iliyokuwa ya bomani na baadaye kuwa ya Ki Islam unataka kunieleza kuwa si halali . Nini nifanye maana hii ndoa hata mimi SIHITAJI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za majukumu!

Kuna shauri lilipelekwa Kanisani (Anglican) kwa ajili ya usuluhishi ikashindikana na kwa kuwa matatizo yao yalishapita kwenye vyombo vingi vya usuluhishi kama vile Mwenyekiti wa Mtaa, Kanisani na Polisi baada ya mwanamke kujeruhiwa kwa vipigo vingi tofafuti na RB zipo zaidi ya tatu kama ushahidi. Mlalamikaji mwanamke akaomba apewe barua kwenda mahakamani kwa hatua zaidi ili aweze kupata talaka.

Mahakama ikampa fomu Na 3 tatu ili kanisa iweze kuijaza ili utaratibu wa kimahakama uweze kuendelea tangu mwezi Novemba, 2018. Mpaka muda huu ninapoandika Kanisani wanadai kuwa hawajakaa kikao chochote bado wako kwenye hatua za awali kulishughulikia jambo hili.

Kisheria hii imekaa je? Nitashukuru kwa ushauri wako ili kujua ni hatua gani za kuchukua.
 
Naomba kuuliza.
Mimi ni Mtanzania lakini nilibahatika kupata marafiki na sasa nchini mwao kuna machafuko ya kivita. Wameniuliza kama inawezekana kwao kuja kufunga NDOA hapa Tanzania, hivyo ningependa kujua kama sheria zinaruhusu na utaratibu upi ufuatwe ili waweze kuja.
Ahsante.
 
Naomba kuuliza.
Mimi ni Mtanzania lakini nilibahatika kupata marafiki na sasa nchini mwao kuna machafuko ya kivita. Wameniuliza kama inawezekana kwao kuja kufunga NDOA hapa Tanzania, hivyo ningependa kujua kama sheria zinaruhusu na utaratibu upi ufuatwe ili waweze kuja.
Ahsante.
 
Nisadie ksi hii tafadhali nakuomba. nitupie inbox, najua unayo maana lazima uwe na TLR kama hii
SARJIT SINGH v SEBASTIAN CHRISTOM 1988 TLR 24 (HC) Court High Court of Tanzania - Dar Es Salaam
Judge Kyando J
 
Hiyo nyumba wawape watoto wairithi mme na mke waondoke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa darasa nzuri sana. Nimejifunza mengi sana kwenye darasa hili.
 
Je kama mm mwanaume ni mfanyakazi halafu nikawa naishi na mwanamke bila kufunga ndoa kwa miaka miwili .Halafu nikachukua mkopo benki nikanunua kiwanja .je siku tukiachana hicho kiwanja tutakigawana ? Wakati mimi bado deni benki wanalikata kwenye mshahara.hapo inakuweje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini,kama ni mali ya pamoja watoto wa nje ya ndoa (kwa ndoa za bomani na za kikristo) hurithi kutokana na matakwa ya wanandoa tu na si vinginevyo.
Mheshimiwa ina maana mke wa ndoa ana HAKI ya kukataa watoto wa nje ya ndoa wa mme wake wasirithi mali?
 
Kama ni mali zako binafsi,haziwezi kuwa machumo ya ndoa. Hivyobasi,hazitagawanywa. Lakini,hakikisha zinakuwa kweli mali zako binafsi kwa kutunza nyaraka za uthibitisho wa hilo.
Mkuu naomba Ufafanuzi hapa, labda ni kwa kutojua sheria hasa kwa mke anaposhirikiana na mme wake katika matumizi nyumbani kiasi kwamba kipato chake chote kinatumika kwa mfano chakula, matibabu, mavazi nk halafu mume yeye ananunua viwanja na kujenga ama anaanzisha kampuni au kitega uchumi chochote kisha hivyo vyote anaandikisha kwa jina lake. Je hapa mke anakuwa na haki ya umiliki? Wakiachana mke watagawana mali au mke ataondoka mikono mitupu? Urithi je, ana haki ya urithi!/ umiliki wa mali hizi?
Asante.
 
Muheshimiwa Petro E. Mselewa kama mme wa ndoa amezaa nje ya ndoa halafu mme anataka kumchukua huyo mtoto kuishi naye, je mke wa ndoa ana haki ya kukataa kumpokea/ kulea mtoto huyo?
 
...kwa hiyo hapa Mkuu Kasabuku ina maana kuwa mnaweza kuishi hata miaka 15 pamoja kwa hiyo mantiki ya kwamba baada ya miaka mi2 tu mmefahamika kama wanandoa...lakini baada ya hiyo miaka 15 mmoja wa wanandoa hao akaamua tu ku move on, habanwi na chochote wala yule aliyebaki hana Say yoyote katika hili??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu Mkuu Kasabuku.
Kama bado upo humu nitakushukuru sana ukinitolea ufafanuzi wa hili...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…