Siku mbili nyuma nimeshuhudia tukio ambalo serikali imelikalia kimya ila lingeweza kuleta madhara makubwa sana kwa Jamii.
kondoo zaidi ya mia 4 zimechinjwa bila kufuata taratibu za kiafya na kisha kugawiwa kwa raia!
Je, hii mifugo ilikuwa salama kiafya haikua na magonjwa yoyote?
serikali ilituma wawakilishi wake kusimamia usalama katika machinjio yale yasiyokuwa rasmi?
Kama lengo ni kujua either walikuwa sawa au hawakuwa sawa kuchinja hao wanyama na kugaia watu basi Naomba nikupe majibu
Serikali haikukaa kimya kama unavyodhani, bali ilikuwa ishamaliza taratibu zote ambazo wao walipaswa kuzifanya ili kuhakikisha usalama wa raia wao
Kinachofanyika ni kwamba, mtu alieamua kujitolea kununua wanyama na kuwachinja ili agaie watu, lazima aende Halmashauri husika kuonana na mkurugenzi
Kwakuwa lengo ni kutoa msaada/suna/zawadi Sijui wenzangu waislamu wanaitaje hii kitu watanisadia, hivo mkurugenzi hutoa taarifa kwa Maafisa Mifugo waliopo chini ya Halmashauri yake na sehemu ambayo tukio litatokea
Baada ya hapo hutolewa kibali Maalimu ambacho hutoa ruhusa ya kuchinja wanyama sehemu tofauti na machinjioni na kukabidhia hao watu ambao wataendesha hilo zoezi
Na taratibu zingine za ukaguzi huanza rasmi baada ya hao wanyama kuwasiri, ambapo kama zoezi la uchinjaji ni kesho, basi leo hii hao wanyama watakaguliwa wakiwa hai ili kujiridhisha kama watafaa kwa kuchinjwa
Na siku ya tukio zoezi la uchinjaji litaendelea likiwa chini ya Afisa Mifugo wa Eneo husika akishirkiana na wengine katika ukaguzi wa wanyama watakaochinjwa, na baada ya zoezi kimalizika Maafisa mifugo walioshirki hupewa pesa pamoja na nyama kama Asante
Kwahiyo nikutoe hofu mkuu, Serikali ilikuwa na taarifa zote na wakajiridhisha juu ya usalama wa wanachi wao