SHETA hatoshi kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam, CCM fanyeni vetting ya viongozi wa wakubwa

SHETA hatoshi kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam, CCM fanyeni vetting ya viongozi wa wakubwa

Binafsi Sina chuki yoyote na SHETA ni kuwa naheshimu sana, ila Niseme wazi huyu bwana hatoshi kuwa Meya wa Jiji la Dar

CCM heshimuni basi wananchi kidogo

Mnafanya mambo kishabiki mno.

Mnawapa watu dhaifu madaraka makubwa mno

Au ndo mnawapa madaraka ili muweze kuwaendesha na kupitisha mikataba na zabuni zenu kifisadi na Kwa ulaghai

SHETA ni msanii hajawahi kuwa hata balozi, mmeiba uchaguzi mkampa kura hewa na eti Leo SHETA ndo Meya wa Jiji la Dar es salaam

Jiji la Dar es salaam ndo lango la Tanzania, East Africa na nchi zote za maziwa makuu

Dar ina Fursa nyingi na changamoto nyingi

Leo mnampa SHETA ambaye ni mchanga kwenye uongozi, mnampa Jiji kubwa kama Dar es salaam
View attachment 3511336
Ongelea uchaguzi uchafuzi wa Ccm, ila kum attack mtu personal haijakaa poa.

Kiuhalisia tunataka vijana wabichi washike nafasi kubwa kubwa za uongozi kama hizo!

Sema Ccm wanewapaka matope sana hata wale wazuri waliokuwa ni chaguo la jamii.
 
Nyumbu huna akili serekali iliyopo unasema huitambui alafu unawachagulia mayor awe nani?

Kweli nyumbu ni msahaulifu sana, nyumbu anamuona mamba lakini ndani ya sekunde mbili anasahau na kusema ni gogo lile mwisho wa siku analiwa.
Hivi ndugu yangu kila alie kinyume na mtazamo wako anakuwa nyumbu?
 
Hoja dhaifu sana hii
Ni ni wakati gan mtu anaacha kuwa mchanga kiuongozi?
Tatizo letu tunakuwa wakali sana kwenye maeneo mengine ila ikifika kwenye viongozi vigezo ni bare minimum.

Jiulize swali moja...ingekuwa anatafuta kazi ya branch manager NMB angepewa tu namna hii?

Mtu anakuwa diwani mara ya kwanza, na umeya juu, wa moja kati ya majiji yanayokuwa kwa kasi duniani?

Are we serious kweli? Au ndio ile tafsiri kwamba mambo yanakwenda na autopilot, hata tukiweka papai hamna shida.

Kama unakumbuka, Jiji la Dar es Salaam kuna kipindi wakati wa Mkapa liliwekwa chini ya uangalizi maalum baada ya Serikali kuona madiwani na meya wao wanazingua... Tume ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Keenja.
 
Ukae ukijua sheta ni form four failure Tena wa division 0 sasa sijui wametumia vigezo Gani kumpa majukumu mazito ivo
Tunaomba risiti mkuu mambo Kwa ushahidi
Hapa jamii forums Kuna matomaso wengi
Tupe majina yake kamili na mwaka alohitimu
 
Wewe unashangaa SHETA kupewa umeya. Je? Mbunge kutoka zanzibar kupewa uwaziri kwenye wizara ambayo sio ya muungano? Wakati kuna ma professor huku wabobezi wa curriculum development.
 
Wewe unashangaa SHETA kupewa umeya. Je? Mbunge kutoka zanzibar kupewa uwaziri kwenye wizara ambayo sio ya muungano? Wakati kuna ma professor huku wabobezi wa curriculum development.
Inasikitisha kwakweli
 
Wachina wote wanaongea Kiingereza? Mbona wana maendeleo? Uelewa wa Mtu haupimwi kwa Mtu anaongea lugha ya kigeni kiasi gani? Na uelewa wa Mtu haupimwi kwa kuwa Mjuzi wa kuongea Kiingereza. Ndiyo maana kwenye mikutano mikubwa huwa kuna Translators. Kiswahili ni lugha inayokua Afrika na duniani. Kwahiyo atawatumia Translators, yeye ataongea Kiswahili Mtafsiri ataongea kwa lugha ya hao wageni. Kwahiyo siyo jambo kubwa sana hilo ni vile tulivyoziweka akili zetu wabongo kwamba mtu asipokuwa Mfasaha wa kiingereza tunamuona kituko.
Hata kwa kiswahili enyewe, huyo Shetta atatoa hoja gani za maana mbele ya kadamnasi?
Ifike hatua tuambizane ukweli, HATOSHIIIII.
 
Na nyuma ya pazia huyu kijana huwa anajishughulisha na nini? Kweli nchi imefika pabaya sana. Huyu kijana biashara yake inajulikana, ila anakuwa mayor kweli? Si ndio muendelezo wa hiyo biashara mpaka vijana wote waishe. Lawama hizi bado ni za huyo huyo mama.
Ndo maana amewekwa hapo kimkakati ili kurahisisha hiyo biashara hapo jijini.

Kila kiti kiko planed, hakijatokea bahati mbayaa.
 
Hata kwa kiswahili enyewe, huyo Shetta atatoa hoja gani za maana mbele ya kadamnasi?
Ifike hatua tuambizane ukweli, HATOSHIIIII.
Labda amepewa cheo Kwakuwa ni mtoto wa Kova ambaye alimzaa Kwa mchepuko
 
Back
Top Bottom