Mungu alimchezea Rough sana shetani kwa nini aliachia uovu uingie moyoni mwake!! wkt aliweza kuuzuia! hata kumbadirisha mwanae?? ivi wewe utaacha first born wako apotee iviiv? wkt umemsomesha? kwa ninialimuumba mshindani wake?? au ina maana hakujua?? Kwa nini wana tuchezea ivo?
Kwani si ndo Mkuu wa ulimwengu huu!! kwa mujibu wa Biblia!!! sasa akavinjari wapi!???.......Mungu lazima ajibu hoja zetu tunamuhtaji sana!! aje faster hapa!!...... anachelewa tu!! akifika mniite!
Hapana shetani ameshinda mara kibao tu.......Bustanini kuleee Eden ali mu-win Adamu kirahisi sana !! kupitia Eva hata hawakufaidi maisha ya kule bustanini!! wakafukuzwa Bustanini mpaka leo kizazi cha Adamu kinahangaika kusiko julikana ,
Na ni marufuku kukanyaga, wala kujua Bustanini kulipo!! mpka leo hii!!..... huyohuyo dogo satan! alifanikiwa kumuua Abel na wakamzika pyuuu mpaka leo hakuacha uzao wala mtoto wa kusingiziwa!!!...... je Mungu anamuogopa??
shetani alifanikiwa kumnyanganya urithi naniliu yule ....esau.. kaka yake Yusufu!!...na huyu Yusufu! akaiba mibaraka ya kaka yake ( Esau) kiutapeli sana tena waziwazi!! mbele ya Malaika,ile ya uzaliwa wa kwanza akatorokea kwa Rabani ...unabisha?? na Mungu aliagiza usiibe....kwa nini dogo aliiba na kutoroka na Mali ya Mibaraka???
Matokeo ya uwizi wizi!!! ule ndo maana walikaa utumwani Misri iviivi miaka mia nne! wakiteseka!!! Yusufu alikuwa Tapeli wa mibaraka ndo maana hata Taifa la Israel liliishi kwa shida mnooo!!...mara wapigwe vita wafe , mara wateswee!
Mpaka leo hawajulikani wako wapi yaani wamepigikaaa!!! hoi bin taabani!!! hawajui hata wao ni wateule wa Mungu!!!! wachache sana tunajua siri hii!!...yoote haya ni sababu ya wizi wizi wa mibaraka isiyomuhusu!
ange baki nazo yule mzaliwa wa Kwanza tu Esau! hata wao hao madogo wangeishi kwa amani na upendo! mpaka leo ndo wangekuwa wanaenda mwezini huko! na kurudi! ila sasa
ajili ya ule utapeli..... hata sometimes walikuwa wana mwasi Mungu! waliishi kimagutu sana miaka yao yote mara wa mwasi Mungu!! mara wapotee kabisaa Duniani hawana heshima ajili ya tapeli mmoja!
Tena msipotezee watoto wa Esau ndo hao wanao enda Mwezini wao wanapeta dogo ange acha ile mibaraka na wao wangepeta ila alikuwa mvurugaji sana! alipata lkn yuko wapi?? kizazi chake ndo hao watumwa!!
Kizazi cha Esau unakisikia wewe?? ......wale wanakula Bata mwanzo mwisho!....huyu alijiingiza kwenye maatizo tu!! na kamwe hajawahi kuwa na amani! je hapa shetani haja fanikiwa kumdanganya dogo, awe mwizi??
Yaani kamwe Israel isinge yumba! yumba hivi km leo!! na ukiangalia sana shetani alikuwa anamtumia mwanamke kuharibu mambo!! hapa kwa yusufu pia Mamake alihusika! Kuharibu mipango ya Mungu! km haitoshi...
SHetani huyuhuyu alimshinda Yuda Iscariote mtu aliye tembea na upako wa Yesu-Mungu mwana miaka kibao na akashawishika kwa laki tatu tu!! na ku zamisha Yesu kwa Wajeda na mafarisayo wa kirumi,
hii ikapelekea Yesu apate kichapo cha mbwa mwizi kikali sana pale Golgotha!! mpaka akalia kilio kikuu je hayo si mafanikio ya shetani??? make ndo alitaka hivo!! ikawa ivo kweli! kwanini Mungu hakuingilia kati kumuokoa Yuda??
au basi ampe adhabu nyingine japo kwa kificho huko!! unadhani sisi tulio watoto wake tukiona ivo hatutishiki???
Mkuu
Shetani kuwawin hao watu uliowataja kuanzia na Adam siyo kumuwin Mungu!
Ukizungumzia vita hii kati ya Shetani na Mungu , God is the winner and the controller
Lakini Vita ya Shetani na sisi binadamu ibilisi ni mshindi!
That’s why Mungu alitoa Kafara Ili sisi tukombolewe kutoka kwenye yake ibilisi na sasa hivi tuko Huru!
Mambo ya Ukombozi kupitia kafara yana mwanzo kutoka kwa Mungu Mwenyewe na hii pia Shetani amekopi!!
Vijana wake na all of his followers anawadanganya hadi kufikia point ya kuua!!
Kwa hiyo Shetani ni Copist ( Copycat) mzuri tuu!
Kitu ambacho Shetani hajawahi kuiga ama kitu pekee ambacho Shetani amekivumbua kwa akili yake chafu ni Uovu tuu peke yake!!
Mengine yote akifanya anafanya kumuiga Mungu!
Kama ni Maandiko anayajua sana pengine kuliko wanadamu wengi waliowahi kuishi!
Angalia alivyokua ananakiri biblia wakati anajaribu Kumdanganya Yesu kule mlimani!!!
Anaqoutw mstari kumbe ameumisquote makusudi ( UONGO HUO)
anatoa tafsiri kumbe ametafsiri Kiuongo makusudi ( UONGO)—- Anamisinterpret verses makusudi!
Ndiyo maana nasema Shetani ni Muongo sana
Hata wewe Mkuu anagalia asikudanganye akakuaminisha kwamba yeye ameshinda Mapigano hayo kiasi kwamba ukamuona hero anaestahili kusifiwa!
“Mamlaka yote Juu Mbinguni na Duniani Nimepewa mimi “ Kristo .
Hapo unaona kabisa Shetani hana Mamlaka Hata Duniani Tena!!
Tayari Ibilisi Hana Mamlaka Yoyote!
Ni Loser!
Ibilisi ni Loser!! The biggest Deceiver Has Lost it all linahangaika tuu!
Mpingeni!
Shetani ni wa kawaida Mno sasa ivi hana ishu anawakamata Wasiojielewa tuu!
Kwanza ni Kiumbe!
Sasa Kiumbe anamshindaje Aliyemuumba!
Kama ni Miscalculation mbaya kuwahi kutokea basi ni ya Shetani kutaka kuwa Mungu hadi akaanzisha vita ambayo kwa ujinga wake alidhani angeshinda!
Matokeo yake Akatupwa chini kutoka Sehemu ambayo alikua na Mungu—-satans first trouble
Then likadhania litatawala dunia, Yesu akaja!
Shetani akaplan kumuua akidhani atashinda kumbe wapi!! Likatumika kutimiza matwaka ya Mungu ya ukombozi wetu!!
Jamaa ana hasira hadi bible imeandika kiasi cha hasira yake!!
Ana hasira because ashajua sasa Fate yake ni ipi Si alijitia Ubabe akajiona Kama Mungu!
Sasa hakujua atakuwa handled vipi hatimaye!
Ikafunuliwa Kwamba wewe Mahali pako ni Katika ziwa la Moto!
Kati ya Kiumbe chenye mwisho mbaya basi ni Shetani!!