Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
Jitahada zipo mkuu na ndio maana waliojiajiri ni wengi zaidi kuliko walioajiriwa, ila tu waajiriwa wengi wana hofu kujiajiri pia hata wale ambao hawajaajiriwa hasa tunaowaiita wasomi (certificate, diploma na degree holder) wengi wao wana kelele sana kuhusu tatizo la ajira kwamba ni bomu kutokana na kujengwa kisaikolojia kwamba ukisoma lazima maisha yako yatakuwa mazuri ila kwa kuajiriwa na si kujiajri na kuufanya ule msemo wa wahenga (elimu ni ufunguo wa maisha) kuonekana kama haupo valid sana maana mafanikio mengi ya kazi za kisomi (tuondoe elimu ya msingi na sekondari) yanatokana na ajira zaidi