nyocksie
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 406
- 265
Mkuu mawazo yako ni mazuri. Lakini kuwa na taarifa tu haitoshi, je! Unaweza ku-analyse hizo taarifa!? Watu wanazo taarifa na wengi wanakoswa ku-analyse hizo taarifa, mwisho wa siku inakula kwao.Pale ulipo...uwe kwenye group la masomo,mazoezi au lolote lile ndipo ulipo mtaji wako.
Mtaji mkubwa sio wazo pekee bali ni TAARIFA sahihi kuhusu kitu,jambo au biashara fulani.
Kumbuka kila kitu duniani ni biashara...Je ww unajua nini kwa undani ?
Hicho unachokijua kigeuze kiwe biashara na mtaji wa biashara hiyo ni huo ujuzi wako(Taarifa sahihi kuhusu unachokijua)
Mifano ni mingi kwa waliotumia wanachokijua kupata mitaji na kuifanya hiyo ndio biashara.
Mf.Dada mmoja aitwa Jamila ni mnene sana ...ktk kutaka kupungua akajiunga na group la WhatsApp linaitwa Loose weight. Pale akakutana na member wenzie wa mikoani (yy yuko Dsm)ilipokua wanazungumza biashara yy akawa anawaelekeza maeneo mazuri ya kupata bidhaa wanazozitaka hapa Dsm..na alikua anaelekeza mpka bei na ubora wa bidhaa husika..(kwamba ukitaka bei nafuu ni mtaa flani duka flan lkn quality kanunue duka flani.Ikaenda mpka akawa anawapokea baadhi ya wafanyabiashara na kuwapeleka madukani..ukizingatia hakua busy sana na shighuli zake.
Hivi ninavyoandika hapa account yke inasoma mzunguko wa mil 20 mpka 70 kila mwezi.
Anatumiwa pesa anawanunulia bidhaa na anawasafirishia mikoani na ameshafungua duka lake Tabata..kila mwezi hakosi mil 3 .
Huo ni mfano mmoja tu ambao umetokana na kua taarifa sahihi na kugeuza kua mtaji.
Inawezekana!
Kitu ambacho mm nakiona ni kwamba watu hawapotezi muda kujua chochote...Hii ni mbaya sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app