The Bible is infallible and inerrant word of God. Imejaa maarifa ya kila aina. Kuanzia k, wajibu ktk dunia, kujitafutia mali, kupata mwenza, kutunza mke na familia kwa ujumla, kuwajibika kwa wazazi, familia, taifa na jamii ikuzungukayo nk. Biblia pia inakupa Nguvu ya kushinda vita ktk ulimwengu wa roho(Efe6:10.... 13). Biblia pia inakulpa uhakika wa maisha maxuri nara utapakoihama dunia hii(maana hapa wote ni wapitaji tu). Shida ipo kwenye kuisoma, kutafsiri na kuielewa kwa ufasaha kisha ndiyo utende yanayopaswa kutendwa nawe, bila hivyo utabaki kuisoma tu kama vitabu vinginevya riwaya tu, na ndipo utakapoina haikusaidii!
Yakobo 1:22-24 SRUV
Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
Yoshua 1:8-9
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
[9]Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.