Shida ya mtoto kutopenda kula kwa hiari yake

Shida ya mtoto kutopenda kula kwa hiari yake

Nsennah

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2021
Posts
1,947
Reaction score
1,554
Habari zenu wana jamvi!! Moja kwa moja kama mada inavyojieleza, kuna mtoto wa miaka miwili hivi sasa ila bado chakula kwake ni kama anapigana vita hadi akabwe na mama yake ndo anyweshwe uji ila chakula hata akilishwa ni kulia na hatokimeza.

Nini suluhu ya hili jambo? Msaada wenu please.
 
Apime wingi wa damu kama iko chini apwe dawa za kuongeza damu
 
Habari zenu wana jamvi!! Moja kwa moja kama mada inavyojieleza, kuna mtoto wa miaka miwili hivi sasa ila bado chakula kwake ni kama anapigana vita hadi akabwe na mama yake ndo anyweshwe uji ila chakula hata akilishwa ni kulia na hatokimeza. Nini suluhu ya hili jambo? Msaada wenu please.
Cheza nae atakula, akikataa mwache, akiwa na njaa mwenyewe atakula, usimlazimishe sana atachukia kabisa kula.

Mwache ale mwenyewe, usimlishe, mwache ajipake, ajisiribe achafuwe, ajichafuwe, usimwingilie. Wewe mtazame tu na video clip juu mchukuwe.
 
Watu wengi Bado wanakula Kwa ratiba yaani asubuhi mchana jioni.
No sivyo ,mtu ale anaposikia njaa na sio kufuata ratiba.
Huyu mtoto apewa chakula Bora chenye lishe nzuri pindi anaposikia hamu ya kula .
Pia Kuna swala la taste na kila binadamu na taste yake Kuna wengine disposition Yao ni vyakula vya uchachu au mwingine vitamu , chumvi au uchungu n.k
Ajaribiwe taste mbalimbali kujua Nini anapenda zaidi .
Jaribu pia kubadili upishi huku ukijifunza ni vyakula gani anapenda.
Badala ya kupika unaweza kukaanga ,kuchoma,mchemsho au kubake hata kama ni mboga za majani.
 
Watoto ni changamoto mkuu. Mimi mwenyewe wa kwangu miaka2 chakula pekee anachokula ni wali, chips na mayai ya kukaanga. Lakini sijui ugali, ndizi, na aina nyingine iwayo ni bora umuue tu. Bahati niliyonayo anakunywa maziwa mgando. Wengine wanasema watoto ambao hawapendi kula kiasili wanakuwa ma intelligent sana.
 
Watoto ni changamoto mkuu. Mimi mwenyewe wa kwangu miaka2 chakula pekee anachokula ni wali, chips na mayai ya kukaanga. Lakini sijui ugali, ndizi, na aina nyingine iwayo ni bora umuue tu. Bahati niliyonayo anakunywa maziwa mgando. Wengine wanasema watoto ambao hawapendi kula kiasili wanakuwa ma intelligent sana.
Chips zinamsaidia nini mtoto?? Mtoto hawezi kujipangia nini cha kula..

Mpime wingi wa damu.
Mpe vyakula vyenye lishe
 
Chips zinamsaidia nini mtoto?? Mtoto hawezi kujipangia nini cha kula..

Mpime wingi wa damu.
Mpe vyakula vyenye lishe

Wewe ndo wale watu mnaokaririshwa vitu na akina JJ Mwaka na mnaamini bila kufikiria hata kidogo.
Chips- Viazi vina wanga nzuri kuliko ugali wenu mnaodhania ndo lishe bora
Chips- Mayai yana protein nzuri sana kuliko maharage mnayoaamini ndo chakula

Mind you nchi zote za wenzetu hawali ugali hata hawaujui na hayo maharage yenu ila daily wanakula viazi mviringo na ndiyo maana watoto wao wanakuwa na afya na akili kuliko hawa wa ugali maharage.

Toka nje ya box mkuu!!
 
Back
Top Bottom