Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

Shigongo anahoja. Naseeb ni mfanyabiashara zinagitia hili
Show za kiingilio cha 10,000 anaweza kufanya Diamond na kuingiza pesa ndefu tu ila inabidi aandae mwenyewe
Mfano tamasha la Wasafi lililofanyika iringa kwa idhamini wa vodacom liliingiza zaidi ya milioni 120
 
Reactions: BAK
Amina mkuu
 
Kwa mtu anayejua maadili ya kazi hizi, kutoa habari za dau gani mnapatana na msanii ni kumvunjia msanii huyo faragha yake ya kibiashara.

Shigongo ama hajui hili, au anajua lakini anapuuza.

Yote mabaya.

Kama nina kazi yangu kubwa siwezi kufanya naye,kwa sababu hana usiri wa kibiashara unaotakiwa.
 
Hahaha mbona shigongo analialia so akamchukue Alikiba akajaze pale Darlive kwa 10,000 kama alivyojaza kule Dodoma kwenye pub
 
Braza kunywa viroba ...mi ntalipia popote ulipo na jela ntaenda kwa niaba yako
 
atamwandama na magazeti yake balaa anatakiwa asome alama za nyakati Diamond ni level nyingine sasaivi
 
Wengi mnachangia kwa mahaba na ushabiki zaidi kuliko hata kuangalia faida ya miaka 20 ijayo ya huyu msanii unaempenda...jibu kwa hoja huku unajiuliza pia ww shabiki hapa tz Mara ya mwisho kuhudhuria show ya diamond kwa kiingilio cha kawaida ni lini kulingana na kipato chako????
 
Kifupi asipangiwe cha kufanya..
 
Zama zimebadilika Mno. Muziki umekua na Wasanii wamezidi kujiongeza. Diamond kwa Milioni mia ni sawa kulingana na Brand yake.
 
Reactions: MC7
Mnh!!ngoja tu nicheke mama[emoji23][emoji23][emoji23]
Karibu biriani hapa na ndizi mbivu mpenzi
 
Kesho akifeli unaanza kumsakama na magazeti yako. Shigongo acha ubahili povu lote limekutoka baada ya WCB kukuchomolea shoo ambayo umeiandaa pasaka DarLive, kwa kutaka kumpa harmonize ela MBUZI. Mimi naona sawa waache wakaze, mtazameni SAIDA KAROLI leo yupo hoi, dunia imebadilika watu wamewekeza mda na ela zao, kwa hiyo lazima ela yao kwanza irudi, alafu mbona mwaka jana diamond platnumz amefanya show Mbeya, Iringa na Mwanza kwa sh 10000 ela ya kawaida na matamasha mengi ya Fiesta yalifanyika kwa sh 10000 na nina uhakika ata tour yao ya WASAFI inayodhaminiwa na VODA ktk mikoa kumi kiingilio kitakuwa 10000 ni bei ya kawaida. Ila shishangai usimchukie diamond platnumz ichukie mitandao ya jamii ambayo imeharibu biashara yako, siku hizi umbeya wa moto moto unapatika instagram, Facebook, whatsup na ndio maana magazeti yako yanadoda, naomba ww Shigongo usiwe mmoja wa mapromota wanaowafanya wasanii wetu wawe MASIKINI WENYE MAJINA MAKUBWA.
 
Kule iringa ata mimi niliona amna mtu aliye kwenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…