Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza pesa nyingi shows za ndani...

Shingongo bana,yake hayaoni anaona ya wenzie. Enzi hizo hata sasa anatajirika kwa migongo ya wasanii hasa bongo movie kawatumia sana kwa skendo za uongo na kweli.

Ameshauri..unaweza kupokea au kupotezea
 
huyu shigongo alizoea kitonga kutoka kwa wasanii
na kuwanyonya sasa wasanii wameanza kuamka anaanza kuisoma namba..
yeye mbona semina zake za ujasilia mali anatoza pesa nyingi tu wakati ndio zinawahusu watu wa tabaka la chini ili wajikwamue kiuchumi....

tena diamond na wasanii wengine endeleeni kukaza hadi watapike nyongo hawa wanyonyaji..
tena msikubali kupangiwa na mtu sababu wakati mnatunga hizo nyimbo hakuna aliyewashawishi,
wala hakuna aliyewasindikiza studio kurekodi
Semina za shigongo bei gani??
 
Bahat nzur nmesoma maon yote kabla ya mm kuchangia,,,labda tujiulize bila kuweka ushabiki kwanza nadhan tutapata jibu..

Milion 100 yes ni nying ila sio nyingi sana kwa brand kama dimond kwa sasa,, swali hapa je wapi?? Tanzania au nje ya tanzania? Kama nje ya tanzania sawa lakn km ni hapa shigongo ndio akipoegemea hoja yake...

Shigongo hajasema hana hadhi hyo ya milion mia,hapana kasema kwa nyumban ni kias kikubwa ambacho ni bora waandae matamasha yale ya buku tatu kama walivyokua wanafanya mwanzo lakin sio promota anamchukua then ategemee kupata faida..

Shigingo ni mmoja wa wafanyabiashara wa kubwa pia,,anajua masuala ya biashara kuliko wengi wetu tunaopakua nyimbo za dimond bure kule u tube,kuna ubaya gan kumshauri?

Siku zote masikini ndio wanaofanya matajiri wang'are zaid maana sisi ndio mtaji wao,,sasa km sisi ndio mtaji wao hawawez kuweka gharama za bidhaa zao mpka tushindwe kununua mwsho watafeli hata wao....

Shigongo ana hoja tena halisi kabsa,,ila siku zote tumeumbwa kupinga na hili sishangai kupingwa,,,ila muda utasema,,,
Amenikumbusha akichomshauri Mbatia kua kuingiza NCCR kwenye ukawa utaimaliza NCCR na watu wake,,,leo kiko wap?? Nccr chali kifo cha mende lakin huku bado mnaikaushia ile...ha ha ha
 
Mapromota wamewanyonya sana wasanii kwa muda mrefu, ni wakati wa wasanii sasa kurudisha walichonyonywa kwa muda mrefu!

Kwanza muziki ni biashara kama zingine, anayemudu bei ndio ananunua, mie sina shida na kuhudhuria show ya msanii yoyote, nikishadownload wimbo natulia zangu ghetto kusikiliza, hizo show mtaenda nyie!
 
Shigongo naye mbona anatoza gharama kubwa kwenye semina zake za ujasirimali.? Huku akijitapa kuwa ni kwa ajili ya tabaka la chini..! Lakini mbona sisi hatujamuoneshea kidole..!

Hivyo basi, mimi naona aanze yeye kufanya hiyo charity kwenye semina zake kwa kutoweka kiingilio, kama kweli anataka asaidie tabaka la chino kuliko kuzidi kuwadidimiza na viingilio vikubwa kuliko uwezo wao..!
 
Majibu ya SK:

IMG_20170401_082536.JPG
 
Shigongo toka aanze kujihusisha na siasa ukijumlisha na hela aliyodhulimiwa na mabwana wale, akili yake haiko vizuri kichwani. Anataka Diamond afanye show za buku tatu kama zamani wakati brand ya Diamond haiko kama dhamani, fikra zake zimekaa kimgando mgando sana, kila siku tunaombea wasanii wetu wakue kimziki wawe na brand kubwa afu huyu kiumbe anataka malipo yasibadilike, afu mbona wasanii wa buku tatu wengi tuu si aende akachukue hao ( Msanii unakuta anakula madawa ya kulevya, mvuta bangi, mchafu, skendo za kijinga jinga kibao).
 
Bahat nzur nmesoma maon yote kabla ya mm kuchangia,,,labda tujiulize bila kuweka ushabiki kwanza nadhan tutapata jibu..

Milion 100 yes ni nying ila sio nyingi sana kwa brand kama dimond kwa sasa,, swali hapa je wapi?? Tanzania au nje ya tanzania? Kama nje ya tanzania sawa lakn km ni hapa shigongo ndio akipoegemea hoja yake...

Shigongo hajasema hana hadhi hyo ya milion mia,hapana kasema kwa nyumban ni kias kikubwa ambacho ni bora waandae matamasha yale ya buku tatu kama walivyokua wanafanya mwanzo lakin sio promota anamchukua then ategemee kupata faida..

Shigingo ni mmoja wa wafanyabiashara wa kubwa pia,,anajua masuala ya biashara kuliko wengi wetu tunaopakua nyimbo za dimond bure kule u tube,kuna ubaya gan kumshauri?

Siku zote masikini ndio wanaofanya matajiri wang'are zaid maana sisi ndio mtaji wao,,sasa km sisi ndio mtaji wao hawawez kuweka gharama za bidhaa zao mpka tushindwe kununua mwsho watafeli hata wao....

Shigongo ana hoja tena halisi kabsa,,ila siku zote tumeumbwa kupinga na hili sishangai kupingwa,,,ila muda utasema,,,
Amenikumbusha akichomshauri Mbatia kua kuingiza NCCR kwenye ukawa utaimaliza NCCR na watu wake,,,leo kiko wap?? Nccr chali kifo cha mende lakin huku bado mnaikaushia ile...ha ha ha
Mkuu ukumbuke Diamond ameajili vijana zaidi ya 50 kuanzia madance hadi ma IT na kumbuka bado TRA analipa kodi Mara mbili
Kwanza analipa campany yake ya WCB, pili analipa Diamond platnumz kama brand inayojitegemea
Moja ya vyanzo vyake vikuu ya mapato in shows anazofanya
Show yoyote ya nyumbani Diamond anatoza dola 55,000 no lazima iwe hivo kutokana na cost ya production kumbuka sasahivi anamiliki bend.
Diamond show ya nje ya Tanzania anatoza kuanzia dola 75,000 na anapata shows kibao.
Labda kama shigongo anazungumzia charity show anaweza kuwa na hoja kwa kiwango hicho
 
Ni kweli.
WCB walitafakari hilo...nyumbani ni nyumbani lazima kuwe na upendeleo...
 
Eric Shigongo, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amelalamika kitendo cha Diamond kuwatoza mapromota wa nyumbani kiwango kile kile anachowatandika wale wa nje.

View attachment 489308

Shigongo ni mmoja wa waandaji wakubwa wa matamasha kupitia ukumbi wake wa Dar Live na huenda miaka ya hivi karibuni ameshindwa kuzimudu gharama za kumchukua kutumbuiza.

Kupitia Instagram, haya ndio mambo aliyoandika:

Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma,aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo.

Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya.Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno. Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo katika ardhi yake ya nyumbani, lakini badala yake wamekuwa wakimuona mara nyingi akifanya shoo Marekani, Ulaya, Nigeria,Afrika Kusini, kwenye Mashindano ya Afcon na sehemu nyingine nyingi ambazo ni nje ya Tanzania, mahali alipozaliwa na kuthaminiwa, mahali ambapo aliweza kujijazia mashabiki wengi.

Mashabiki zake wanahitaji shoo, kumsoma kwamba amejenga nyumba, amenunua au amepata watoto na Zari si kitu ambacho mashabiki wanakihitaji zaidi kutoka kwake, wanachohitaji ni kuona shoo zake kwa wingi kama kilivyokuwa kipindi cha Moyo Wangu, Kamwambie na nyimbo nyingine.

Ni kweli ana jina kubwa, ana mashabiki wengi, amepambana sana kufika alipokuwa lakini kwa upande mwingine anatakiwa kuangalia gharama za shoo zake hasa anapofanya nchini Tanzania,kwa watu ambao walimfanya leo kujulikana zaidi kama Diamond na si Naseeb Abdul.

Leo, Diamond anafanya shoo kwa dola 55,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100. Hii inamaanisha kwamba kwa mtu kama mimi,nikimchukua Diamond kwa gharama hiyo inamaana kwamba nitataka niingize kiasi kikubwa kama faida, kwa hiyo badala ya kufanya shoo Dar Live, Diamond Jubilee au sehemu nyingine, nitaihamishia shoo yangu Mlimani City na kufanya kiingilio cha shilingi elfu hamsini.

Swali la kujiuliza, je, yule bodaboda anayepiga sana nyimbo za Diamond ataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini? Yule kijana anayatafuta riziki kwa kuingiza nyimbo za Diamond kwenye simu za wateja ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza.

Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi.

Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona?

Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza.

Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa.Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo.

Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU”

Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki.

TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!!
Hatari sana Jehanamu inanunuliwa Kwa pesa lukuki,pepo ya bure watu hawataki
 
Hoja za Shigongo kumbe ndio hizi? Yani mtu afanye show kisa amefanya tuu...... yani afanye show kufurahisha watu huku yeye na familia yake waendelee kuteseka au baadae tuje kutoa lawama kuwa alikuwa anafanya show lakini amekufa masikini....Shigongo acha ujinga..
Muziki ni biashara kama biashara zingine Shigongo aache ujinga kuna watu wanatoa laki hapa Tanzania kwenye kumuona msanii sasa asimpangie msanii bei ya show kisa watakao kuja ni watanzania...

Kwanza asilete uongo kuwa Diamond anatoza 100m kila show,Diamond si mjinga bali ana angalia aina ya mteja na aina ya show ya kufanya... Shigongo anatakiwa kujua kuwa si lazima Diamond afanye kila show wakati anapewa pesa mbuzi kwa alipofikia Diamond anatakiwa akifanya show imlipe kweli kweli maana asipo ingiza hela sasa baadae watakuja kumuandika kwenye magazeti yake kuwa alicheza na hela.

Shigongo unatakiwa kujua hutoweza kumuharibia Diamond kwa kuweka hadharani mambo yake binafsi ili asipate show bali kupitia makala yako umemuongezea thamani.. na hii ulio fanya ni dhambi na ni kosa.

Shigongo hata yeye hatukuwai kumpangia bei ya magazeti yake bali wanaoweza kununua wana nunua wasio weza wana acha...na yeye aanze kuuza magazeti Tsh 100/= hadi sasa sijaona hoja ya maana...
Nchi hii ina wasanii wengi hizo million 4 akawape wasanii wengine....

Mtu kama Diamond ana majukumu makubwa sana tena sana angalia watu walio mzunguka wote wale wana haki ya kulipwa hivi kweli Shigongo anategemea ataweza kumlipa Diamond kwa kutegemea mapato ya mlangoni hahahahaha ...kweli nimeamini ameanza kuchanganyikiwa ..
Na pata shida kumuelewa ukomo wa ufikiri wake akili elimu aliyonayo thinking capacity yake imekaa kibashite [HASHTAG]#asiwapangie[/HASHTAG] WCB namna ya kufanya biashara zao.huyu msukuma naye mkolomije
 
Back
Top Bottom