Shigongo: Kuna Wafanyabiashara wanashirikiana na Viwanda Kushusha ubora wa Dawa Nchini

Shigongo: Kuna Wafanyabiashara wanashirikiana na Viwanda Kushusha ubora wa Dawa Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-09-22 at 14.49.16.jpeg
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo James, inachukua nafasi hii kuipongeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA), chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake, Dkt. Adam Mitangu Fimbo, kwa kazi nzuri inayoendelea kufanywa katika kudhibiti uingizaji wa dawa bandia nchini.

Dawa bandia zimekuwa tatizo kwa muda mrefu na zimeendelea kuhatarisha afya na maisha ya Watanzania, ikiwemo kuchangia usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Antimicrobial Resistance-AMR), hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya jamii na vifo.

Kwa muda mrefu, Kamati ya Bunge ya Afya na UKIMWI, ambayo Mbunge wa Buchosa ni mjumbe wake, imekuwa ikifuatilia na kupambana na changamoto hii. Kamati hiyo imekuwa ikiitaka TMDA kuchukua hatua madhubuti na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha dawa bandia hazipati nafasi ya kuingia ndani ya mipaka ya nchi.

Hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia TMDA ikikamata shehena za dawa zenye thamani ya mamilioni ya shilingi ambazo zimebainika kuwa na viashiria vya kutokuwa salama au kutokidhi viwango vinavyotakiwa.

Hatua hizi zinaonesha juhudi kubwa zinazofanywa na TMDA katika kulinda afya za Watanzania, hivyo kazi hiyo inastahili pongezi na inapaswa kutiwa moyo ili mamlaka iendelee kuimarisha udhibiti wa dawa nchini.

Aidha, Ofisi ya Mbunge inamwomba Dkt. Fimbo pamoja na timu yake ya TMDA kuendelea na kuimarisha ziara za kushtukiza katika maghala ya kuhifadhia dawa yanayomilikiwa na wafanyabiashara na waagizaji wa dawa. Katika ziara hizo, sampuli za dawa zichukuliwe na kupelekwa katika maabara za mamlaka kwa ajili ya uchunguzi na uhakiki wa ubora na kiwango cha dawa (potency).

Ofisi ya Mbunge imezisikia taarifa zinazosema kwamba baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa ya kujipatia faida wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya viwanda vinavyotengeneza dawa kwa kushusha kiwango cha dawa (potency), jambo linaloweza kusababisha dawa kutokuwa na uwezo unaostahili wa kutibu (efficacy).

Vitendo vya aina hii, endapo vitathibitika, ni hatari kwa afya za Watanzania, kwani vinaweza kuchangia usugu wa vimelea dhidi ya dawa na hatimaye kugharimu maisha ya watu.

Kwa msingi huo, Ofisi ya Mbunge inaiomba Serikali kuendelea kuiwezesha TMDA kwa kutenga bajeti ya kutosha, pamoja na kuongeza watumishi na vitendea kazi, ili mamlaka iweze kutekeleza jukumu lake kwa ufanisi zaidi.

Tanzania ni nchi kubwa yenye mipaka mingi, ikiwemo mipaka isiyo rasmi, hivyo kuimarisha uwezo wa TMDA ni muhimu katika kudhibiti uingizaji na usambazaji wa dawa zisizokidhi viwango.

Pia soma ~ Kwanini Tanzania imekuwa kama dump ya bidhaa feki almost kila kitu sasa hivi ni feki
 
Back
Top Bottom