Shija Richard, mtia nia Urais TFF kumpeleka Rais wa TFF kamati ya maadili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shija Richard ambae ni mtia nia ya Kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho la soka nchini TFF, amesema amerudisha fomu yake ya Urais wa TFF bila ya kupata Endorsement hata moja.

Richard Shija ambae aliwahi kuja mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga SC amesema wakati anapambana kupata Endorsement alikuta Endorsement 46 kati ya 47 zimeshachukuliwa.

Hivyo Shija Richard amesema atamshitaki kwenye kamati ya maadili, Rais wa TFF Wallace Karia lakini pia atamshitaki Rais Karia kwenye kamati ya rufaa.

Shija Richard amesema Rais wa TFF Wallace Karia amefanya makosa ya kimaadili kwa kuchukua Endorsement zote.

Hizo endorsement huwa zinapatikana vipi kwani?
 
Eti amechukua endorsement?Watu hawachukui wanatafuta. Malalamiko yameanza mapema sana.
 
Kumbe aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji pale yanga, kule kuna watu wawili tu ambao Haji Manara aliwataja hao wengine ni kama yule mwenye zero matokeo ya advance
 
Eti amechukua endorsement?Watu hawachukui wanatafuta. Malalamiko yameanza mapema sana.
Kipindi cha kutafuta wadhamini ni kipi? Yaani unatafuta wadhamini kwa utaratibu upi?
 
Yule mjinga mwenye ameshajimilikisha shirikisho kwa kuwahonga wajinga wenzake wenye njaa, pasipo kuangalia maslahi mapana ya mpira wa migiuu nchini.
 
Akichaguliwa nani ndio yatakuwa maslahi mapana😎
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Hiyo moja aliyoiacha itakuwa ya Yanga.

Maana naona waliojitokeza kutokea Yanga, na waliokuwa viongozi wa Yanga ni wengi sana kwa nafasi ya Rais.

Karia kacheza kete zake vizuri, kilichobaki ni kuona je hajakiuka kanuni kwa kuchukua zote au kuzipata kabla ya utoaji fomu. Lakini kama alizibook tu na akasubiri fomu, basi yipo sawa
 
Kipindi cha kutafuta wadhamini ni kipi? Yaani unatafuta wadhamini kwa utaratibu upi?
Yaani anagombea na hajui endorsement zinatafutwaje?Unapochukua fomu unajaza wadhamini waliokudhamini katika nafasi tajwa.
 
Shija Richard ambae ni mtia nia ya Kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho la soka nchini TFF, amesema amerudisha fomu yake ya Urais wa TFF bila ya kupata Endorsement hata moja.

Richard Shija ambae aliwahi kuja mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga SC amesema wakati anapambana kupata Endorsement alikuta Endorsement 46 kati ya 47 zimeshachukuliwa.

Hivyo Shija Richard amesema atamshitaki kwenye kamati ya maadili, Rais wa TFF Wallace Karia lakini pia atamshitaki Rais Karia kwenye kamati ya rufaa.

Shija Richard amesema Rais wa TFF Wallace Karia amefanya makosa ya kimaadili kwa kuchukua Endorsement zote.

Hii Paskali aliniambia inaitwa election flaud, sasa hapa Takukuru inabidi wawaangalie hawa watoa endorsement ni watu wa tabia zipi na huyo mgombea aliye chukua endorsement kwanini kachukua zote Badala ya 5 ansc
 
Yaani anagombea na hajui endorsement zinatafutwaje?Unapochukua fomu unajaza wadhamini waliokudhamini katika nafasi tajwa.
mkuu hao kina mayay kukosa wadhamini ni kama vile wamefanyiwa hujuma tu za makusudi ili wakose vigezo vya kugombea..endorsement yaani wadhamini wapo 47 na masharti kwenye fomu ni lazima kila mgombea apate endorsement zisizopungua 5..na kila endorsenent moja ni kwa mgombea mmoja tu haitakiwi kujirudia kwa mgombea mwingine..kilichotokea sas endorsement zoote 47 na hivyo endorsement 46 zimesaini kwa Karia..hivyo wagombea wengine wamekosa wa kuwadhamini hivyo wanahisi labda karia kawahonga rushwa na wadhamini wote wakamsainia yeye peke yake wakati kanuni imeomba angalau wa 5 tu wanatosha ila Karia kafanya kuwakomoa wenzie kuwasainisha kwake wote hivyo wagombea wengine watakuwa nje ya vigezo kwa kutotimiza masharti hivyo wanaweza kuenguliwa na Karia kupita bila kupingwa...kama kanuni iliweka endorsement zisipungue 5 kwa kila mgombea basi pia ingeweka na ukomo wa maximum limit endorsement labda 10 ili na wagombea wengine nao wapate wa kuwadhamini badala kanuni haijaweka ukomo pia imeweka kizingiti eti mdhamini ukimsainia ngombea mmoja hurusiwi tena kumsania mgombea wa pili..kama karia kawasainisha wote kwake hivyo wenzake wanakosa sifa za kugombea kwahiyo wanasubiri huruma tu kwa kamati ya uchaguzi kama wataona aibu kumpitisha karia bila kupingwa.!
 
Yaani kukosa endorsement kwa wagombea iwe ni tatizo la Karia?Kama huwezi hata kupata endorsement hata 1 utawashawishi vipi wajumbe wa Mkutano Mkuu wakuchague?Mkutano Mkuu ndio uliokubali kanuni za Uchaguzi na wajumbe wakapitisha.Sasa kama waliompa endorsement Karia wameridhika kumpa na kanuni zinaruhusu tatizo ni nini?
Wajumbe wa Mkutano Mkuu ndio wanamchagua Rais wa TFF sio mashabiki,wachambuzi hilo ni muhimu kulielewa.Kuhusu rushwa anayetuhumu aende Takukuru.
 
Hii Paskali aliniambia inaitwa election flaud, sasa hapa Takukuru inabidi wawaangalie hawa watoa endorsement ni watu wa tabia zipi na huyo mgombea aliye chukua endorsement kwanini kachukua zote Badala ya 5 ansc
Unatakiwa uwe na endorsement zisisopungua 5.Kanuni haisemi zisizidi 5.Hakuna kosa kuwa na endorsement 40 au 46.
 
Back
Top Bottom