Shija Richard ambae ni mtia nia ya Kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho la soka nchini TFF, amesema amerudisha fomu yake ya Urais wa TFF bila ya kupata Endorsement hata moja.
Richard Shija ambae aliwahi kuja mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga SC amesema wakati anapambana kupata Endorsement alikuta Endorsement 46 kati ya 47 zimeshachukuliwa.
Hivyo Shija Richard amesema atamshitaki kwenye kamati ya maadili, Rais wa TFF Wallace Karia lakini pia atamshitaki Rais Karia kwenye kamati ya rufaa.
Shija Richard amesema Rais wa TFF Wallace Karia amefanya makosa ya kimaadili kwa kuchukua Endorsement zote.