Shikamoo biashara

Shikamoo biashara

Kuna jamaa kakodi frame mbezi mwisho frame ya laki 4 kwa mwezi (4,800,000 kwa mwaka). Sasa angalia bidhaa anazouza ni maua ya plastic kayajaza na vikorombwezo vya sikukuu za kuzaliwa na harusi! Sasa biashara ya aina hii inaweza hata kurudisha kodi ya mwezi/siku?
Hao wameshindikana wako wengi mno mno unakuta mtu aanalipa laki tano. Fremu alfu kutaa anacho USA sasa
 
Shida wana uwa wanakurupuka sana yaani akishika chenji yeye yumo kwenye bussiness tayari .

Kifuatacho ni kupost mambo whatsap kila kukicha ila ground hali ni tete .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Hat kula mchna Hali

Kuna bint mmoja anaduka sinza la kuuza oil za magari Sasa anacho fanya Ni kupost kila siku mtaandaoni

Na ukikah nae hat kula hawezi Hulu akilipia fremu laki 500k
 
Hakuna sehem nzur ya kufanya biashara kama Africa. Unatakiwa tu kujua kudance according the tune. Ngoja niishie hapo. Achanen na biashara ya people power mzee. Kuna huna kitu huna power.
 
Ndugu pale matumizi ya kawaida ya familia yanapokuwa makubwa kuliko faida ni stress kubwa, huoni pakutokea tena kwenye biashara, halafu unatakiwa ulipe kodi za watu hujui unaipatia wapi, madeni ya mikopo kila siku hodiii dukani, huna backup, only option ilikuwa kujiondoa.

Nikatangaza kuuza biashara watu wengi wakajitokeza kuinunua kwa historia yake, nikaiuza bei nzuri sana.

Niliyemuuzia naye ameshaifunga [emoji3] sidhubutu hata kumsalimia ananiulaumu balaa.
Hahaha biasha ganj hii ya mageneza nn
 
Hahahaha inafurahishaga na kuhuzunisha, anakuuliza biashara kama hii mtaji kiasi gani, soko likoje na changamoto.

Kiuhalisia huwezi kumwambia changamoto unazopitia ila unatamani Umwambie lete hela nikuuzie hii yangu.
Tatizo huwenda nae akataka kufungua Happ Happ jirnaj kwangu alfu tugawane wateja
 
Kudumu kwa biashara inategemea na factors nyingi Location, demand, mtaji, msimamizi, sera za kiuchumi n.k

Mfano mwaka 2014 nilianzisha biashara ile biashara ilianza vizuri sana na akachanganya sana, ilifanya vizuri kwa sababu ya mazingira biashara ilipokuwepo kulikuwa hakuna access ya barabara pana ya kupita malori, barabara pana ilikuwa inaishia kwangu kwahiyo wateja walikuwa wanatoka maeneo mbalimbali kuja kununua bidhaa kwangu kwa jumla halafu wanasomba na mikokoteni kuingia huko ndani ndani.

Mwaka 2018 ukaja mradi wa kukarabati barabara za mitaani, watu wakalipwa na barabara zikapanuliwa kwa kiwango cha lami.

Nikapoteza wateja wa jumla wote, biashara yangu mauzo yakadrop ile mbaya mwisho ikafa.

Biashara ya pili ilikuwa ya duka baada ya barabara kukarabatiwa zilijengwa frame nyingi sana, yakafunguliwa maduka mengi biashara zinazofanana, bidhaa nyingi wateja wachache. Duka likaangukia pua.

Kwahiyo kudumu kwa biashara muda mrefu kuna sababu nyingi sana. Ila nilichojifunza jitahidi kuwa mfanyabiashara wa kati wa Jumla/mtaji mkubwa na sio mfanyabiashara wa mwisho.
Safi mzee, kwaio kwa sasa bado unafanya biashara za jumla ??
 
Dah hiyo ilinitokeaga kuna jamaa alikuja jirani yangu akafungua huduma za mpesa kumbe lengo lake ni kuja kubadilisha biashara ifanane na yangu.

Nilimkaribisha vizuri na nikawa nampa ABCD za biashara yangu kumbe nampa madini

Siku nashangaa anashusha bidhaa kama zangu dah yalikuwa maumivu sana. Nilimeza kidonge kichungu sana.

Ila biashara za maduka zenye mitaji midogo za kijinga sana full kuigana na kuwa saresare maua. Biashara ya duka nzuri iwe ya kuuza jumla jumla yale maduka madogo yaje kwako.
Brother Tubariki na mawazo mawili matatu ya biashara. Tushike peni na karatasi tuandike tuchukue notes
 
Biashara inakuhitaji uwe na nidhamu kwa kila shilingi, unaweza kuwekeza pesa nyingi ila faida ikawa kidogo sana kama bei ya kreti; usipokuwa na nidhamu lazima biashara ife.
Majuzi nilimtembelea rafiki yangu mmoja, amenunua mashine ya kudarizi 30m, nilimkuta anaweka nembo kwenye mashati 30, lakini malipo aliyopata ni shilingi 60,000/=; kwa mazingira hayo kama huna nidhamu ya pesa, unaweza kuhisi hiyo milioni 30 aliyowekeza kwenye mashine imepotea.
 
Hat kula mchna Hali

Kuna bint mmoja anaduka sinza la kuuza oil za magari Sasa anacho fanya Ni kupost kila siku mtaandaoni

Na ukikah nae hat kula hawezi Hulu akilipia fremu laki 500k
Binti ukiona anafanya biashara sio wa kushindana naye! Kwanza kodi ya pango ni chupi! Mtaji ni chupi! Hawanaga mahesabu zaidi ya kukuelekeza kwenye 'V' ya mapaja yake ukitaka kudai kodi! Wanaofanya biashara za piga/ua/komaa ni wanaume!
 
Back
Top Bottom