Shikamoo kilimo

mkuu pole sana ungefanya utaratibu wa umwagiliaji drip irrigation imekuwa mkombozi wa wengi eneo dogo lakini output ni kubwa.
Asante mkuu. Drip irrigation kwenye eka 30 budget yake sio poa.
Mostly ni wanaolima kilimo cha bustani ndio wanaweza fanya hivyo.
 
Anzia tu hapo mkindo Morogoro, achilia mbali mabonde kibao yaliyojaa Tanzania, kuna sehemu ndani ya hii nchi maji hayakauki...
Mpunga haulipi kama zao hili.
 
Hakupaswa kuweka pesa yote shambani, na ukizingatia kwamba alikuwa anategemea mvua kwa kiasi kikubwa,

Na ni kweli kwenye kilimo ukiwa ndio unaanza, watakaokubeba ni wataalamu wa kilimo kwa 40% na wakulima kwa 60% (hasa wa eneo husika). Hawa wakulima wawe wa eneo husika, sababu wao ndio wanajua uhalisia wa eneo lao kijiografia kwa kipindi kirefu, na usishangae kukutana na mkulima anakuambia "safari hii sipeleki mbegu shambani", hawa wanajua eneo lao kuliko mamlaka ya hali ya hewa na watu wa soil pale SUA
 
Huu msimu jua kali, pamoja nawadudu wakutosha kwawale waliochelewa panda,
Walioenda na Maharage wamewin sana
 
Pesa ndogo ndo kiasi gani mkuu? Huenda 10M kwake ndo pesa ndogo.
Kwa malalamiko aliyotoa na hasira aliyonayo inaonekana kwake 10m ni pesa ndefu.

Aliposema, "pesa ndogo ndo ingefanya mvua inyeshe" ni wazi kwamba anakubali 10m ni kubwa.
 
Asante mkuu. Drip irrigation kwenye eka 30 budget yake sio poa.
Mostly ni wanaolima kilimo cha bustani ndio wanaweza fanya hivyo.
Badala ya 30 unalima hata 5 kama test,kuna mkurugenzi alilima 1 heka ya nyanya alivunja rekodi ambayo wakulima wa nyanya wa kumwagilia kwa kutapanya maji hawakuwah kutoa.

binafsi najiandaa na heka 1 ya maharage ya njano kwa drip irrigation nitaleta mrejesho.

N.B:kuna kampuni ziko arusha wanalima kwa greenhouse dah wale jamaa wanasupply mpaka kwenye supermarket za arusha.
 
Nimemuomba jamaa aniambia anajishughulisha na nini,kapiga pause.
Ushauri wangu kwake ajikite zaidi alikopata hizo 10million. Mungu ana kanuni ya kubariki kazi za mikono yetu wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…