Shikamoo kilimo

Shikamoo kilimo

mkuu pole sana ungefanya utaratibu wa umwagiliaji drip irrigation imekuwa mkombozi wa wengi eneo dogo lakini output ni kubwa.
Asante mkuu. Drip irrigation kwenye eka 30 budget yake sio poa.
Mostly ni wanaolima kilimo cha bustani ndio wanaweza fanya hivyo.
 
Anzia tu hapo mkindo Morogoro, achilia mbali mabonde kibao yaliyojaa Tanzania, kuna sehemu ndani ya hii nchi maji hayakauki...
Mpunga haulipi kama zao hili.
 
Kilimo pia kinataka pilot plant ( ikiwa ndio mara yako ya kwanza kulima ) haijalishi umejiridhisha kiasi gani kwamba lazima utapata mavuno na mtaji kurudi kwa kuwasikiliza wataalamu na wakulima tuu ,Hii itasaidia mtu binafsi kuweza kung'amua baadhi ya huduma za uendeshaji kama ziongezwe au zipunguzwe ili kukuza mtaji ( maximize profit) pindi utakapo lima kwa mara nyingine zaidi. Mfano mtaji wa mil 8 ,lazima ubakize hata mil 4 kama backup usiweke wote kwa mara moja,baada ya muda faida itakayopatikana itakupeleka karibia na 8mil au zaidi ,hapo ndio unaweza rudia wazo la kuweka 8mil yote.
Hakupaswa kuweka pesa yote shambani, na ukizingatia kwamba alikuwa anategemea mvua kwa kiasi kikubwa,

Na ni kweli kwenye kilimo ukiwa ndio unaanza, watakaokubeba ni wataalamu wa kilimo kwa 40% na wakulima kwa 60% (hasa wa eneo husika). Hawa wakulima wawe wa eneo husika, sababu wao ndio wanajua uhalisia wa eneo lao kijiografia kwa kipindi kirefu, na usishangae kukutana na mkulima anakuambia "safari hii sipeleki mbegu shambani", hawa wanajua eneo lao kuliko mamlaka ya hali ya hewa na watu wa soil pale SUA
 
Huu msimu jua kali, pamoja nawadudu wakutosha kwawale waliochelewa panda,
Walioenda na Maharage wamewin sana
 
Pesa ndogo ndo kiasi gani mkuu? Huenda 10M kwake ndo pesa ndogo.
Kwa malalamiko aliyotoa na hasira aliyonayo inaonekana kwake 10m ni pesa ndefu.

Aliposema, "pesa ndogo ndo ingefanya mvua inyeshe" ni wazi kwamba anakubali 10m ni kubwa.
 
Asante mkuu. Drip irrigation kwenye eka 30 budget yake sio poa.
Mostly ni wanaolima kilimo cha bustani ndio wanaweza fanya hivyo.
Badala ya 30 unalima hata 5 kama test,kuna mkurugenzi alilima 1 heka ya nyanya alivunja rekodi ambayo wakulima wa nyanya wa kumwagilia kwa kutapanya maji hawakuwah kutoa.

binafsi najiandaa na heka 1 ya maharage ya njano kwa drip irrigation nitaleta mrejesho.

N.B:kuna kampuni ziko arusha wanalima kwa greenhouse dah wale jamaa wanasupply mpaka kwenye supermarket za arusha.
 
Pole sanaa nimependa ulivyokuwa muwazi, kwamba kwenye kilimo wewe ni mgeni! Kosa ulilolifanya ni ku-invest a huge amount of capital kwa trial project kulingana na uwezo wako. Maana mwengine hiyo 10M ni hela ya kawaida. Pole sanaa Mkuu, ni kweli kilimo kinalipa tena sanaa lakini inahitaji kuwa adaptive to the latest technologies ili kuweza kupata matokeo makubwa tarajiwa. Ni ukweli usiopingika kama unataka kufanya kilimo serious basi andaa miundombinu ya kilimo kwanza, mtafute mtaalam kwa hiyo amount ungeweza kufanya irrigation layout nzuri tuu na kuitumia kwa muda mrefu.
Nina mengi ya kusema lakini naomba niishie hapa.
Mimea haihitaji mvua ili ipate kustawi, la hasha mimea inahitaji MAJI ili iweze kustawi. Tuondokane na dhana za karne za zamani tunasubiri msimu wa mvua ili tulime. Hapana twende kitaalam wasomi tunao tuwatumie ili mambo yaende vizuri. Kwa kusema hivi simaanishi kwamba usilime eneo lako ambalo lipo free tuu kwa kutegemea mvua, unaweza ukalima ila kaa chini CALCULATE RISK kwanza then ndiyo uingie mzigoni.
Narudia tena, natoa Pole nyingi sana kwako kwani hiyo inahitaji ujasiri. Usivunjike moyo
Nimemuomba jamaa aniambia anajishughulisha na nini,kapiga pause.
Ushauri wangu kwake ajikite zaidi alikopata hizo 10million. Mungu ana kanuni ya kubariki kazi za mikono yetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom