Shikamoo kilimo

Shikamoo kilimo

Mwaka sisi wakulima tuzidishe maombi maan hali ni tete.
Nilitenga milioni kumi. Ndiyo 10m!.
Nikaingia porini. Niliweka watu wakasafisha pori. Hiyo ilikua December last year.
Ila kila nikikaa machale yananicheza.
Page pendwa yangu ikawa tma.
Yes bila hiyana nikasoma kua mvua zitanyesha chini ya wastani.
Refer hapa.
Basi nikajipa moyo. Nikaendelea na process za kulima na kisha ilinyesha mvua kidogo. Tukazika mbegu shamba lote.
Ekari 30.
Tuliweka camp nikiambatana na wafanyakazi wangu wa mkataba wa 3.
Vibarua hawakukauka shambani kwangu.
Kwakweli kazi ilifanyika kwa ustadi wote.
Sikutaka kurudi mjini mpaka nione hatima ya pesa yangu ninayoizika siku hadi siku.
Huku nikipewa matumaini na wakulima wenzangu kua mvua ziko karibuni.
Siku zinakatika jua linazidi kudhoofisha mimea yangu.
Inasikitisha sana kushuhudia mimea inanifia machoni mwangu.
Nimekata tamaa.
Inasikitisha sana.
 
Niliona nakumbuka lakini siku kufuatilia kama ulikuwa na MILION kumi ulitakiwa uchimbe kisima Chako na ununue pampu ya solar kipindi hiki Cha jua inafanya kazi vyema sana Kisha mipira ya kazaa ya kusambazA maji katika Eka 5 tu asee ungepiga mazao hiyo tulishaacha kipindi Cha nyuma huko jitahidi kishirikiana na watu
Mkuu nakufollow PM
 
Nilitenga milioni kumi. Ndiyo 10m!.
Nikaingia porini. Niliweka watu wakasafisha pori. Hiyo ilikua December last year.
Ila kila nikikaa machale yananicheza.
Page pendwa yangu ikawa tma.
Yes bila hiyana nikasoma kua mvua zitanyesha chini ya wastani.
Refer hapa.
Basi nikajipa moyo. Nikaendelea na process za kulima na kisha ilinyesha mvua kidogo. Tukazika mbegu shamba lote.
Ekari 30.
Tuliweka camp nikiambatana na wafanyakazi wangu wa mkataba wa 3.
Vibarua hawakukauka shambani kwangu.
Kwakweli kazi ilifanyika kwa ustadi wote.
Sikutaka kurudi mjini mpaka nione hatima ya pesa yangu ninayoizika siku hadi siku.
Huku nikipewa matumaini na wakulima wenzangu kua mvua ziko karibuni.
Siku zinakatika jua linazidi kudhoofisha mimea yangu.
Inasikitisha sana kushuhudia mimea inanifia machoni mwangu.
Nimekata tamaa.
Inasikitisha sana.
Ulilima zao gani,? Kuna Watu wanalima mpunga wa kumwagilia hawalii mvua kutokunyesha!
 
mkuu pole sana ungefanya utaratibu wa umwagiliaji drip irrigation imekuwa mkombozi wa wengi eneo dogo lakini output ni kubwa.
 
Pump ya kuvuta maji ya kumwagilia Eka Tano Haizid laki tatu ya Sola na kisima mfano Geita nilipo wanachimba kwa 300000 kinatosha kumwagilia Eka Tano mpaka 10 kwakuwa unamwagilia HAIZIDI masaa 6 kwa siku kina kuwa na matumizi hayo ni kawaida kabisa
Nikadhani kisima cha kuchoronga na machine Nicholas cha wachimba na motor ni sawa but sio permanently sana. Pia naomba uniunganishe na hao wachimbaji nipo geita msalala mkuu
 
Kilimo pia kinataka pilot plant ( ikiwa ndio mara yako ya kwanza kulima ) haijalishi umejiridhisha kiasi gani kwamba lazima utapata mavuno na mtaji kurudi kwa kuwasikiliza wataalamu na wakulima tuu ,Hii itasaidia mtu binafsi kuweza kung'amua baadhi ya huduma za uendeshaji kama ziongezwe au zipunguzwe ili kukuza mtaji ( maximize profit) pindi utakapo lima kwa mara nyingine zaidi. Mfano mtaji wa mil 8 ,lazima ubakize hata mil 4 kama backup usiweke wote kwa mara moja,baada ya muda faida itakayopatikana itakupeleka karibia na 8mil au zaidi ,hapo ndio unaweza rudia wazo la kuweka 8mil yote.
 
Pole sana mpambanaji!! Kaza buti bila kuchoka. Kila bznes ina Changamoto Yake.
Oh okay sawa
 
Hamjui tu kwanini mvua inatagemewa sana.

Nyumbani tuna migomba mingi na maji ya kutosha lakini inakauka na jua pamoja na kulaza maji mpk ardhi inasema basi lkn wapi jua ni Kali mno.

Hali ya hewani ikibadilika maji hayawezi kusimama kama UTI wa mgongo wa kusimamisha mmea.
 
Mil 10 unawekeza kwenye kilimo? Akati watu wanalima kuitafuta hiyo Mil 10.

Poleee sanaa.
Yes. Niliwekeza 10m kwa kulima eka 30.
Ingeenda poa ningevuna na kupata wastani wa 1m kwa eka.
Hiyo si pdf, ni real figure niliishuhudia misimu miwili iliyopita.
Means total ningevuna 30m ndani ya miezi sita.
 
Back
Top Bottom