Shikamoo ni salamu ya ovyo

Shikamoo ni salamu ya ovyo

Umetumia lugha chafu sn na kweli umeonesha jinsi usivyo na adabu. Yani mama wa watu tena mtu mzima unamuita "kimama". Kizazi hiki laana tupu. Vipi angekuwa mama yako ndo anaitwa"kimama" utajiskiaje.
Inategemea na yeye aliniingia vipi, angeniheshimu ningemuheshimu pia, huwezi mvunjia mtu heshma kisa ww mkubwa
 
Yaan nlipokuwa nasoma adv kuna walimu wa kik walikuwa hawaitikii shkamoo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaona una wachoresha, eti "shikamoo " na midevu yako [emoji23]
 
Kila watu wana mila na desturi zao,na ndio inafanya utofauti katika ya MTU na mtu, Nchi na Nchi-sasa unataka watu wote wawe na mila zinazofanana?
Kwa nini undhanie mila na desturi ya mwingine ni bora kuliko ya kwako? He elimu yao ndio imekupelekea kuwa na fikira hizo?

Ukiwa Roma fanya kama Waroma wanavyotaka.
Wewe pia una support hii salamu ya hovyo ?
 
"Shikamoo pesa"

Uislam raha sana.


Asalaam Alaikum, haina mkubwa kwa mdogo wala mdogo kwa mkubwa. Haina mwanamke kwa mwanamme wala mwanamme kwa Mwanamke.
Hata " habari za saa hizi/jioni/ asubuhi" haina pia
 
Basi tumia: Hello, How U Doing? Kama hawakuelewi tumia: Hi, Dude!
Wakishanga tena na hiyo, waamkie hivi: whatsup, mother f....ker?
[emoji23][emoji23] sio bure kuna aina flani ya majani unatumiaga
 
Tangu nimerudi nchini nimekuwa nikipata tabu sana kutambua yupi anastahili shikamoo na yupi hastahili, kuna nalingana nao umri ila wana maumbo makubwa hivyo najikuta nikiwapa shikamoo na hawaitikii.

Kuna watu ni wakubwa ila wanaonekana ni wadogo ki-umbo hivyo nimekuwa nawa-skip na huniona sina adabu, najiona nimekuwa.

Yaani kwa kifupi nimechoshwa na hii salamu,, ni salamu ya hovyo mnoo, nimechoshwa kila ninapokutana na mtu nianze kufikiria salamu ya kumpa.

Mbona wenzetu mfano Uganda salamu ni hiyo hiyo mdogo ana msalimia mkubwa na mkubwa ana msalimia mdogo..

Anyway, nguvu moja [emoji881]
Salamu ya kutakiana amani ambay haibagui umri unaeza mtolea mtu yyt awe mkubw wako au hata mdg wako mmeikataa. Pambaneni
 
Kuna nchi nilikuwa sasa jamaa wa huko ana hamu kinoma ya kujua kiswahili sasa akakariri kwamba shkamoo ni salamu kwa yeyote. Yule jamaa mkubwa kuliko mimi ila akiniona tu anakimbilia kusema SHKAMOO... Nikawa nakwepa kupita hata maeneo anayokaa.
 
Mtoto wa miaka kumi akikusalimia 'habari yako'' au akasema 'hello'ni sahihi?

Mimi naona kama ni dharau
Ni sahihi ila tatizo ni mind set yako imejengeka kuwa shikamoo ndo heshima
 
Mimi kuna kimoja kiliniletea miyeyusho kwenye bajaji kisa shikamoo
 
Hiyo salam naamini imemsumbua karibia kila mtu katika makuzi yake. .ukiwa mtoto inajulikana wazi, ni yupi anastahili shikamoo, na yupi hastahili. Na huyo asiye stahili manaake ni mtoto mwenzio kwahyo mnatazamana tu.

Kuna kaumri flani kanafikaga yani unashindwa kabisa kujua yupi ni wa shikamoo na yupi ni wa habari yako. Na wote unatakiwa kuwasalimia[emoji28]
Mimi ndo nipo kwenye umri huo mkuu basi ni mtihani kweli kumjua wa kumpa shikamoo
 
Back
Top Bottom