Shikamoo ni salamu ya ovyo

Shikamoo ni salamu ya ovyo

Bro angu ras alishatuambiaga home shkamoo ni salamu ya kishamba, salamu yetu ni amani na upendo, unajibu idumu milele, na ukimjia na shkamoo yako haitikii.[emoji3]
Bora hiyo ina sound vyema kuliko utumwa wa shikamoo
 
Dah hii kitu ilishawahi nitokea kipindi nahudumu pale serena hoteli nilikua mlangoni nakaribisha wageni wa aina tofauti tofauti kiumri, jinsia na mataifa hivyo alikuja mzee wa makamo na gari moja kali sana kwa rafudhi yake tu nikajua huyu ni mTZ

Hivyo nikaanza kwa kumsalimu "habari boss shikamoo, karibu sana boss" Dah basi yule mzee alinijia juu anadai mimi ni sawa na mwanawe wa mwisho halafu namsalimu habari yaani mzee alinifokea mno muda wote huo mzee anafoka mimi nilishikwa na mshangao nisijue nianzie wapi kujitetea

Ukweli ni kwamba nilimsalimu habari kisha nikatanguliza na shikamoo ila yule mzee ile shikamoo hakuisikia
 
Tangu nimerudi nchini nimekuwa nikipata tabu sana kutambua yupi anastahili shikamoo na yupi hastahili, kuna nalingana nao umri ila wana maumbo makubwa hivyo najikuta nikiwapa shikamoo na hawaitikii.

Kuna watu ni wakubwa ila wanaonekana ni wadogo ki-umbo hivyo nimekuwa nawa-skip na huniona sina adabu, najiona nimekuwa.

Yaani kwa kifupi nimechoshwa na hii salamu,, ni salamu ya hovyo mnoo, nimechoshwa kila ninapokutana na mtu nianze kufikiria salamu ya kumpa.

Mbona wenzetu mfano Uganda salamu ni hiyo hiyo mdogo ana msalimia mkubwa na mkubwa ana msalimia mdogo..

Anyway, nguvu moja [emoji881]
utamaduni wetu na wa waganda tofauti

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
Ishiiiiiy watembee na kadi za clinic.

Swali la kizushi: juzi tulikuwa na mashoga zangu umbea wa hapa na pale likazuka swali!

Let say mdada ana 30yrs ana date mbaba wa 55 yrs. Kabla ya kudate heshima kibao kama anapokea ekaristi.

sasa ndo ku date haswa hivi kikatiba isiyo rasmi huyu mwanaume shikamoo yafaa kuendelea kumzeesha tena?

Wanaume mkuje mjibu haraka mnatuchanganya. Sasa mtu umelala nae the same bed at asubuhi "shikamo" hii imekaaje?

Mko wapi wanaume nawasubiri hapa!!!
Shikamoo kwa Mume kutoka kwa mkewe inategemea na asili ya familia na mahusiano baina ya mke na mume bila kujali umri. Mfano:
1. Mke humuamkia mume mbele ya watoto ili kujenga kwa watoto kuwa baba ni kichwa cha nyumba na watoto hupokea hilo maishani mwao. Lakini wazazi wanaweza kuwajenga pia watoto wao katika salamu za kiimani kwa hivyo shikamoo sio lazima.
2. Kuna shikamoo ya mahaba ambayo mke huwa anampa mumewe. Narudia hii huwa ni shikamoo ya mahaba na utani wa kimapenzi yaani mke na mume huwa katika hali hiyo nyakati fulani fulani si mara zote ( hili hutokea automatic kwa mke wangu mara chache sana hasa nikirudi nikiuliza hujambo mke wangu nae hujibu kwa kusema "sijambo mume wangu shikamoo" na wote huwa tunaishia kucheka. Jambo hilo hutokea kwa mwaka mara moja au mara mbili. Mke wangu ni age mate wangu kabisa.
3. Shikamoo ikitumika visivyo itajenga distance kati ya mke na mume. Hasa kwenye familia yenye migongano kwa wingi na mawasiliano hafifu.
NB: shikamoo, salamu inayoweza kukubaliwa na wanandoa husika kuwa sehemu ya maisha yao au kutokea mara chache kama ajali. Au isitokee kabisa lakini maisha yakasonga. Kikubwa kila mwanandoa awajibike kwa nafasi yake hapo ndipo heshima ya kweli hutokea. Hasa baba kutoa mitonyo ya kulea familia.
 
Tangu nimerudi nchini nimekuwa nikipata tabu sana kutambua yupi anastahili shikamoo na yupi hastahili, kuna nalingana nao umri ila wana maumbo makubwa hivyo najikuta nikiwapa shikamoo na hawaitikii.

Kuna watu ni wakubwa ila wanaonekana ni wadogo ki-umbo hivyo nimekuwa nawa-skip na huniona sina adabu, najiona nimekuwa.

Yaani kwa kifupi nimechoshwa na hii salamu,, ni salamu ya hovyo mnoo, nimechoshwa kila ninapokutana na mtu nianze kufikiria salamu ya kumpa.

Mbona wenzetu mfano Uganda salamu ni hiyo hiyo mdogo ana msalimia mkubwa na mkubwa ana msalimia mdogo..

Anyway, nguvu moja [emoji881]
Salimia asalam aleykum, salamu hiyo haina mkubwa wala mdogo
 
SHIKAMOO == Nipo chini ya miguu yako.
Ni salam ya kitumwa mtumwa kumsalimia mmiliki wake .
 
Binafsi siitumii tena, hata kwa wazee. Kuna salamu zenye heshima kuliko hiyi ambayo hata haieleweki.
Mimi pia siitumii sana japo kuna wengine huwa wananisema
 
Tangu nimerudi nchini nimekuwa nikipata tabu sana kutambua yupi anastahili shikamoo na yupi hastahili, kuna nalingana nao umri ila wana maumbo makubwa hivyo najikuta nikiwapa shikamoo na hawaitikii.

Kuna watu ni wakubwa ila wanaonekana ni wadogo ki-umbo hivyo nimekuwa nawa-skip na huniona sina adabu, najiona nimekuwa.

Yaani kwa kifupi nimechoshwa na hii salamu,, ni salamu ya hovyo mnoo, nimechoshwa kila ninapokutana na mtu nianze kufikiria salamu ya kumpa.

Mbona wenzetu mfano Uganda salamu ni hiyo hiyo mdogo ana msalimia mkubwa na mkubwa ana msalimia mdogo..

Anyway, nguvu moja [emoji881]
Watasema tusalimiane kwa kazi iendelee
 
Ahaha..Kwan kabla haya nje ya "inji" si alikua anafahamiana na hawa watu ndio mana hata amerud bado kawagundua?

Atumie utaratibu ule ule kabla hajaenda nje ya "inji"
Maringo tu 😀😀tutajuaje kama alikua nje ya inji
 
Back
Top Bottom