Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Zamani ilikua ni kawaida sana kukuta mwanaume anateseka na kuumia kwa wakati mmoja kisa mwanamke. Wengi walikua wanateswa na ule ulimbukeni na ushamba wa wanawake – mwanaume akipenda, anapenda mpaka anasahau kabisa yeye ni nani.
Mtu alikuwa tayari kutoa kila kitu ili tu ampate mwanamke. Anaweza kutumia pesa, muda, nguvu na hata kuvumilia vitu ambavyo leo ukimwambia mwanaume avumilie, atakuuliza, “Kwani mimi nimekosea nini?”
Lakini kadri miaka ilivyokwenda, ule ulimbukeni ukapungua. Wanaume wakaanza kujitambua, wakaanza kuweka boundaries na mambo yakaanza kubalance.
Lakini sasa kuna kitu nimeanza kukiona kwa miaka ya karibuni...
Mzani umegeuka tena.
Siku hizi naona wanawake ndio wanaonekana kuteseka zaidi kwenye upande wa mahusiano.
Mfano mdogo tu:
Unamtongoza mwanamke, anakwambia “nitakupa majibu.”
Unakaa kimya.
Siku zinapita...
Wiki inapita...
Halafu ghafla anakutafuta:
"Jambo lako nalifanyia kazi, sijakusahau.”
Unamwambia sawa.
Baada ya hapo anakupa jibu ambalo ni “YES.”
Sasa hapa ndipo huwa najiuliza...
Tatizo ni nini mpaka siku hizi mwanamke anakumbusha mwanaume aje kuchukua majibu ya utongozi wake?
Zamani mwanaume angekuwa anasubiri majibu kama vile anasubiri matokeo ya mtihani.
Leo mwanamke mwenyewe anakufuatilia kuhakikisha umechukua majibu yako.
Na hii haipo kwenye kutongozana tu.
Unaweza kuachana na mwanamke, ukamnyamazia, ukajipanga na maisha yako...
Baada ya muda unakuta ameanza kukutafuta yeye mwenyewe.
Mwingine anakumbusha memories, mwingine anaanza kuuliza unaendeleaje, mwingine anakwambia “mbona umenikata hivi?”
Kwa kifupi, kuna wakati mwanaume alikuwa anaonekana kama ndiye mwenye emotional dependence kubwa kwenye mahusiano.
Lakini siku hizi naona mambo yamebadilika.
Mwanaume akiona mambo hayakai sawa, anaondoka. Mwanamke anabaki anajiuliza: “Hivi huyu mwanaume amebadilika nini?”
Swali langu kwa wadau wa JF:
Ni nini hasa kimebadilika kwenye mahusiano ya siku hizi mpaka mzani ukaonekana kuelemea upande wa wanawake?
Je, ni kwamba wanaume wameacha kuwa wale wanaume wa zamani waliokuwa tayari kuvumilia kila kitu?
Au ni kwamba wanawake wa sasa ndio wameanza kuwa emotionally invested zaidi kuliko wanaume?
Na kwa nyie wanawake wenyewe – mnaona kweli shilingi imegeuka?