Kutokana na nature ya kiuumbaji, Mwanamke anachukuliwa kama kiumbe dhaifu kuliko mwanaume (japo wote tuna udhaifu in general kama wanadamu)
Kutokana na udhaifu huo by nature hata uhalisia kwenye maisha kua mwanamke ni kiumbe dhaifu.. Mwanaume kupigwa na mwanamke linaweza lisiwe jambo la ajabu sana kama mwanaume kumpiga mwanamke, kama umesoma moja ya comment yangu huko juu kuna mtu nimemjibu kua mwanamke kupigwa hata makofi mawili matatu kwenye ndoa hilo suala lipo ila sio kwa stage hiyo aliyofikia Uchebe, mpaka anamvizia mwanamke amelala usingizini ndio unampiga ngumi sasa si uboya huo.
Halafu mambo mengine mwanaume unatakiwa kujiongeza, umeshaona mwanamke amekuzidi kipato au upendo umepungua si uite ndugu m solve, ikishindikana si basi muachane, wanaume wangapi wanawapa wake zao talaka? Hapa inaonekana kawaida kwa sababu Shilole ni mzima, angefariki mfano huyo Uchebe angekua wapi sasa hivi? Au yule aliyemchoma mke wake na mkaa kaishia wapi sasa hivi?
Haya mambo yapo na yanaumiza lakini mwanaume lazima uwe na uwezo wa kutazama mbali, siku zote hasira ni hasara, haya alivyompiga kafaidika nini? Kwani hayo matatizo ya Shilole yameisha?