Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mi nshamjua mshindi....
Jumamosi:
Asubuhi: Uji wa lishe na vitumbua.
mchana. Kande za mahindi mabichi yaliyochanganywa na maharagwe mabichi kisha kuungwa na nazi. kisukumia maziwa ya mtindi.
Jioni: Rosti ya maboga yaliyochanganywa na nyama ya kuku ya kukaanga
N.B. Matunda na maji ni wakati wowote au saa moja baada ya mlo au kabla ya mlo.
JUMAPILI:
Asubuhi: Saa kumi na moja Maji ya kunywa ya moto with lemon/ asali. nusu lita.
Saa nne uji wa lishe na vinailon (aina ya viazi mbatata vya kukaanga)
Mchana: Ugali wa ndizi pamoja na rosti ya karanga iliyochanganywa na nyama ya ng'ombe.
ikisindikizwa na avocado, na juisi ya embe
Jioni: Maziwa fresh pamoja na mchemsho wa viazi mbatata.
Jumatatu: Asubuhi: Saa kumi na moja Maji ya kunywa ya moto with lemon/asali mdalasini
Saa Nne Uji lishe with mayai ya kukaanga yaliyochanganywa na vitunguu, green beans, celery,
karoti, kitunguu saumu na hoho.
Mchana: Michembe (wasukuma wanajua) with majani ya kunde ya kukausha pamoja na maziw mtindi.
Jioni. Samaki sato chukuchuku (mchemsho) pamoja na viazi mviringo mchemsho.
Jumanne: Asubuhi saa kumi na moja (maji ya kunywa ya moto kama kawa hapo juu)
Saa nee Supu ya mabogo iliyochanganywa na utumbo.
Mchana: Ugali wa ulezi na bamia.
Jioni. Chai ya maziwa na chips.
Nitaendelea.................
karibu wakati wowote. Hivi shindano liliisha jamani maana sikumaliza menu yangu kwa ajili ya kuwa occupied. sijui mshindi alikuwa nani.Nimependaje menyu yakooo jamanniii..nije nikupe visit lini asee
karibu wakati wowote. Hivi shindano liliisha jamani maana sikumaliza menu yangu kwa ajili ya kuwa occupied. sijui mshindi alikuwa nani.
Eeh aasante kwa kunijuza ngoja niandae nitarudi.imalizie tu menu yako,deadline ni ni aprili mwisho wa mwezi
ha ha ha iko wapi menu yako?mshindi ni mimi bila shaka loh
The Boss iiiiiiiiiiiiiiiii,
come this way bhana!!!!
ha ha ha iko wapi menu yako?
Huna lolote mtazame vile 🙂Mhh,,ngoja shindano liendelee kwanza, ikifika fainali ntaitoa haha
Juice ya uyoga plzDay 1;
A;chai rangi, magimbi ya kukaanga,roast maini na juisi fresh ya matunda
B;viazi vikuu vilivyoungwa na Karanga na njegere bila kusahau mbona za majani
C;futari ya mihogo,kunde ukishushia na chai ya maziwa na kipande cha chungwa
Day 2;
A;Maziwa fresh, omllete ,bagia za dengu na kipande cha tikiti maji
B;chips, mishikaki na salad(nyanya,vitunguu,karoti na tango) na glass ya red wine kupambana na cholestol
C;makande ,maziwa fresh na parachichi
Day 3;
A;uji wa ulezi uliochanganywa na maziwa mtindi ,siagi na Karanga
B;ndizi mshale za kupika na utumbo na juice ya ukwaju
C;fried coated potato with egg, salad (nyanya, kitunguu, carrot, pilipili na tango), kuku wa kukaanga na juice ya passion.
(dah! Siku heavy hii lazma iwe jumamosi)
Day 4;
A;chai rangi, sausage, maboga ya kuchemsha na kipande cha embe
B;firigisi za kusaga zilizochanganywa na mayai, ndizi za kuchoma, kachumbari na juice ya ubuyu
C;mchemsho wa mbogamboga na samaki, juice ya uyoga( hii juice weka mbali na watoto)
Day 5;
A;mihogo ya kuchemsha,chai ya maziwa na tango lenye mayonise
B;ndizi choma mbuzi choma, kachumbari na glass ya red wine
C;ndizi matoke zilizochanganywa na maharage, mboga za majani (hapa chinees itafaa) na chai ya maziwa
Day 6;
A;chai ya maziwa, vitumbua, yai la kuchemsha na juice ya parachichi
B;maboga ya nazi, maini roast na mboga za majani
C;futari ya viazi vitamu ilochanganywa na maharage na chai ya rangi
Day 7;
A;supu ya pweza, bagia za kunde na juice ya embe
B;salad ya matunda (embe,parachichi, ndizi, papai na tikiti) yenye asali baadae unashushia maziwa mtindi
C;kuku roast wa kusaga, na mkate wa mchele uliopakwa asali na juice ya uyoga.
Nb; kila mlo hapo utaseviwa na maji ya kunywa safi na salama
menu hii nimezingatia upishi wa asili na kisasa, na makundi yote ya chakula...bila kusahau vyakula maalum (aphrodisiac) kama vile juice ya uyoga, asali, supu ya pweza, parachichi na wine kumuweka mzee fit......
Juice ya uyoga plz