Shindano kwa wapishi wa JF

Shindano kwa wapishi wa JF

snowhite, Kaunga, KOKUTONA na shansarie nabadilisha ratiba ya jikoni kwangu now!
The Boss asante sana kwa kutusaidia hili

Unajua hata mimi nimejikuta napenda hii ratiba baada The Boss kutuhamasisha
Mama yangu hupiga vita sana vyakula hivi tunavyokula vyenye madhara, lakini tunaonaga anatubaniiia pamoja na uelewa tulionao kuhusu madhara yake.
Vitu asili na michemsho bila mafuta meeengi ndo mpango mzima.

Mzima lakini dada yetu? Siku ukipika TOKE unikaribishe dadaee

Thanks to The Boss
 
Last edited by a moderator:
D1
B: Ndizi mzuzu za kukanga (zilizoiva kidogo) & chai
L: Steamed vegetable & fresh juice
D: Fried fish, chips & salad

D2
B: Mayai ya kuchemshwa & fresh juice
L: Fruit salad & mtindi
D: Mashed potatoes & chicken stew

D3
B: Viazi vitamu vya kuchemshwa na mchaichai
L: mishikaki & salad
D: Coconut fish curry & cassava

D4
B: Fruit smoothie
L: Kitimoto & salad
D: Ndizi za kupikwa na nyama ng'ombe (mshale mgumu) & spinach pembeni

D5
B: Mayai ya kukaanga, sosegi & chai
L: Mchemsho wa kuku na ndizi
D: Beef stew & baked potatoes

D6
B: Mtoriii
L: Mchemsho wa samaki na veggies
D: Maharage ya nazi & yam

D7
B: Uji wa ulezi
L: Roast ya firigisi za kuku & ndizi choma
D: Nyama ya ng'ombe choma & fried vegetables

* Mchemsho/supu&veggies ina mchanganyiko wa vitu kama kama carrot, paprika, vitunguu, nyanya, broccoli, majani ya giligilani, uyoga, pilipili kwa mbali nk.
* Chai inaweza kuwa ya rangi au maziwa na/bila viungo na unaweka asali.

Asante kwa hili zoezi The Boss.
 
Day 1;

A;chai rangi, magimbi ya kukaanga,roast maini na juisi fresh ya matunda
B;viazi vikuu vilivyoungwa na Karanga na njegere bila kusahau mbona za majani
C;futari ya mihogo,kunde ukishushia na chai ya maziwa na kipande cha chungwa

Day 2;

A;Maziwa fresh, omllete ,bagia za dengu na kipande cha tikiti maji
B;chips, mishikaki na salad(nyanya,vitunguu,karoti na tango) na glass ya red wine kupambana na cholestol
C;makande ,maziwa fresh na parachichi

Day 3;

A;uji wa ulezi uliochanganywa na maziwa mtindi ,siagi na Karanga
B;ndizi mshale za kupika na utumbo na juice ya ukwaju
C;fried coated potato with egg, salad (nyanya, kitunguu, carrot, pilipili na tango), kuku wa kukaanga na juice ya passion.
(dah! Siku heavy hii lazma iwe jumamosi)

Day 4;

A;chai rangi, sausage, maboga ya kuchemsha na kipande cha embe
B;firigisi za kusaga zilizochanganywa na mayai, ndizi za kuchoma, kachumbari na juice ya ubuyu
C;mchemsho wa mbogamboga na samaki, juice ya uyoga( hii juice weka mbali na watoto)

Day 5;

A;mihogo ya kuchemsha,chai ya maziwa na tango lenye mayonise
B;ndizi choma mbuzi choma, kachumbari na glass ya red wine
C;ndizi matoke zilizochanganywa na maharage, mboga za majani (hapa chinees itafaa) na chai ya maziwa

Day 6;

A;chai ya maziwa, vitumbua, yai la kuchemsha na juice ya parachichi
B;maboga ya nazi, maini roast na mboga za majani
C;futari ya viazi vitamu ilochanganywa na maharage na chai ya rangi

Day 7;

A;supu ya pweza, bagia za kunde na juice ya embe
B;salad ya matunda (embe,parachichi, ndizi, papai na tikiti) yenye asali baadae unashushia maziwa mtindi
C;kuku roast wa kusaga, na mkate wa mchele uliopakwa asali na juice ya uyoga.

Nb; kila mlo hapo utaseviwa na maji ya kunywa safi na salama

menu hii nimezingatia upishi wa asili na kisasa, na makundi yote ya chakula...bila kusahau vyakula maalum (aphrodisiac) kama vile juice ya uyoga, asali, supu ya pweza, parachichi na wine kumuweka mzee fit......
 
Jamaniii,na me ntacontest,napenda kupika,ntaleta my menu ,af siku ya kutaja washindi mtu'mention kabisa ili tuone kwenye notification,namimi naandaa yangu af ntaipost badae
Cc@The Boss
 
Jumamosi:
Asubuhi: Uji wa lishe na vitumbua.

mchana. Kande za mahindi mabichi yaliyochanganywa na maharagwe mabichi kisha kuungwa na nazi. kisukumia maziwa ya mtindi.

Jioni: Rosti ya maboga yaliyochanganywa na nyama ya kuku ya kukaanga

N.B. Matunda na maji ni wakati wowote au saa moja baada ya mlo au kabla ya mlo.

JUMAPILI:

Asubuhi: Saa kumi na moja Maji ya kunywa ya moto with lemon/ asali. nusu lita.
Saa nne uji wa lishe na vinailon (aina ya viazi mbatata vya kukaanga)

Mchana: Ugali wa ndizi pamoja na rosti ya karanga iliyochanganywa na nyama ya ng'ombe.
ikisindikizwa na avocado, na juisi ya embe

Jioni: Maziwa fresh pamoja na mchemsho wa viazi mbatata.

Jumatatu: Asubuhi: Saa kumi na moja Maji ya kunywa ya moto with lemon/asali mdalasini
Saa Nne Uji lishe with mayai ya kukaanga yaliyochanganywa na vitunguu, green beans, celery,
karoti, kitunguu saumu na hoho.

Mchana: Michembe (wasukuma wanajua) with majani ya kunde ya kukausha pamoja na maziw mtindi.

Jioni. Samaki sato chukuchuku (mchemsho) pamoja na viazi mviringo mchemsho.

Jumanne: Asubuhi saa kumi na moja (maji ya kunywa ya moto kama kawa hapo juu)
Saa nee Supu ya mabogo iliyochanganywa na utumbo.

Mchana: Ugali wa ulezi na bamia.

Jioni. Chai ya maziwa na chips.

Nitaendelea.................
 
Haya mapishi nimeyapenda, menu zote ziko swafiiii.
 
My menu is a Local one,kwa kutumia vitu ambavyo watanzania wa kawaida,na hali ya juu wanaweza nunua ,uandaaji pia ni rahisi,chakula ni BALANCED DIET,pia ladha/FLAVOUR imezingatiwa,so mpishi atapika kulingana na idadi ya walaji

MONDAY DAY1

B.FAST
Milk Tea,Gimbi la kuchemsha,egg ommelette(fried eggs)
LUNCH
Ndizi bukoba iliyoungwa na kuku , Spinach
SUPPER
Mchemsho wa viazi ulaya na kuku ile inayobaki mchana,Fruit Salad

TUESDAY

B.FAST
Black Tea (ya Tangawizi),Mihogo /mahindi ya kuchemsha
Sausage,Fruits of your choice

LUNCH
Mashed Potatoes,Samaki wa mchuzi ameungwa na nazi na mchicha(unaungwa na karanga)

SUPPER
Banana Fritters,Njegere,Vegetable,Salad

WEDNESDAY

B.FAST
Coffee,vitumbua na Samosa

LUNCH
Tambi na minced meat(beef),Mixed fruits salad

SUPPER
futari ya mihogo(inaungwa na nazi,pia nyanya),minced meat ilobaki mchana,na Vegetable salad

THURSDAY

B.FAST
fresh milk,(asiependa anaweka coffee,tea etc),Viazi vitamu fried /vya kuchemsha na mayai (boiled)

LUNCH
fried ndizi mzuzu,Pork roast,Kachumbari,Juice

SUPPER
Chapati,tomato soup au mchuzi mzito,maharage kidogo,Fruits of your choice

FRIDAY

B.FAST
Mtori Nyama,na vegetables kama matango ,vitunguu,carrots unaweka vinegar kdogo

LUNCH
Chips,Samaki fried,Cabbage Salad

SUPPER
Grilled Viazi Vitamu,Mishkaki(beef),Juice

SATURDAY
B.FAST
bajia/kachori,Juice na sausages

LUNCH
Makande,Fruits salad

SUPPER
Mchemsho wa ndizi Bukoba,nyama ya mbuzi na vegetable salad of your choice

SUNDAY

B.FAST
uji/mtori wa utumbo

Since sunday kuna kwenda church na shughuli za hapa na pale,itafata......

BRUNCH
Baked potatoes(viazi ulaya),ROast ya Maini,vegetable salad ,Juice

SUPPER
burger,french fries,fruits,cocktails

NB.:Menu inakuwa served na maji,juice( nimeandika sehemu baadhi),na any othr health drinks of ur choice ie rozela,nk
salads pia zina aina tofauti tofauti,utabadilisha upendavyo,Vyakula vinapikwa na viungo mbalimbali ili kuongeza ladha,na kuliwa na vikorombwezo kama chatni,chachadu nk,Pia vinakuwa served vikiwa garnished vizuri..
ni vyepesi kupika na vimezingatia kanuni za afya
WELCOME AND ENJOY!!
 
Day 1;

A;chai rangi, magimbi ya kukaanga,roast maini na juisi fresh ya matunda
B;viazi vikuu vilivyoungwa na Karanga na njegere bila kusahau mbona za majani
C;futari ya mihogo,kunde ukishushia na chai ya maziwa na kipande cha chungwa

Day 2;

A;Maziwa fresh, omllete ,bagia za dengu na kipande cha tikiti maji
B;chips, mishikaki na salad(nyanya,vitunguu,karoti na tango) na glass ya red wine kupambana na cholestol
C;makande ,maziwa fresh na parachichi

Day 3;

A;uji wa ulezi uliochanganywa na maziwa mtindi ,siagi na Karanga
B;ndizi mshale za kupika na utumbo na juice ya ukwaju
C;fried coated potato with egg, salad (nyanya, kitunguu, carrot, pilipili na tango), kuku wa kukaanga na juice ya passion.
(dah! Siku heavy hii lazma iwe jumamosi)

Day 4;

A;chai rangi, sausage, maboga ya kuchemsha na kipande cha embe
B;firigisi za kusaga zilizochanganywa na mayai, ndizi za kuchoma, kachumbari na juice ya ubuyu
C;mchemsho wa mbogamboga na samaki, juice ya uyoga( hii juice weka mbali na watoto)

Day 5;

A;mihogo ya kuchemsha,chai ya maziwa na tango lenye mayonise
B;ndizi choma mbuzi choma, kachumbari na glass ya red wine
C;ndizi matoke zilizochanganywa na maharage, mboga za majani (hapa chinees itafaa) na chai ya maziwa

Day 6;

A;chai ya maziwa, vitumbua, yai la kuchemsha na juice ya parachichi
B;maboga ya nazi, maini roast na mboga za majani
C;futari ya viazi vitamu ilochanganywa na maharage na chai ya rangi

Day 7;

A;supu ya pweza, bagia za kunde na juice ya embe
B;salad ya matunda (embe,parachichi, ndizi, papai na tikiti) yenye asali baadae unashushia maziwa mtindi
C;kuku roast wa kusaga, na mkate wa mchele uliopakwa asali na juice ya uyoga.

Nb; kila mlo hapo utaseviwa na maji ya kunywa safi na salama

menu hii nimezingatia upishi wa asili na kisasa, na makundi yote ya chakula...bila kusahau vyakula maalum (aphrodisiac) kama vile juice ya uyoga, asali, supu ya pweza, parachichi na wine kumuweka mzee fit......

ok! Good.......

naomba juisi ya uyoga.
 
ngoja nijaribu

Monday
B: chai ya rangi yenye mdalasini na hiliki kitafunwa muhongo wa kuchemsha

L: viazi vitamu vimesongwa na maharagwe

D: ndizi mzuzu za nazi

Tuesday
B: uji wa soya

L: makande ya karanga na njugu mawe

D: viazi ulaya mix na nyegere

Wednesday

B: ndizi mzuzu za kuchemsha na chai ya rangi yenye tangawizi

L: mihogo ya nazi na mchicha

D: ndizi bukoba na maharagwe

Thursday

B: uji wa mtama

L: makande ya mahindi mabichi njegere

D: ndizi mshale ya moshi ya kukaanga na parachichi na chai ya mchaichai

Friday
B: chai na maboga ya kuchemsha

L: viazi vitamu na mtindi

D: viazi ulaya vya kuponda saved na choloko

Saturday
B: supu ya mboga mboga mix na viazi ulaya

L: ndizi mshale ngumu ya mbeya na utumbo

D: viazi vitamu na samaki wa kukausha na unatia na nazi, ngogwe

Sunday
B: chai na mzuzu iliyoanza kuwiva ya kukaanga

L: viazi vikuu na figiri

D: muhogo wa nazi na dagaa uwono la chukuchuku

Nimejaribu kutoweka nyama theboss
 
Last edited by a moderator:
RATIBA YA MLO MAALUM:

Jumatatu : viazi, na mchemsho wa nyama
Jumanne : magimbi yalichemshwa na chai ya maziwa
Jumatano : pika maharage weka nazi kisha kula na mkate yabisi
Alhamisi : chakula cha mchannganyiko wa makande na bamia
Ijumaa : kula matunda kwa wingi kisha tupiamo maji mengi
Jumamosi : kula mbogamboga sana na mbatata
Jumapili kula samaki na viazi mviringo changanya katika samaki waliotiwa nazi

sijui kama nitashinda shindano hili kwani nimelikuta limebandikwa muda mrefu
 
Hivi katika mchakato huu tumezingatia kwa ajili ya familia au mtu mmojammoja The Boss kama ni kwa familia tena hizi za kwetu za kiafrika basi bado watu hawajaitendea haki hii topic yako kwanza kwa kuzingatia hali yz uchumi na hali ya hewa.Hivi kweli fikiria upike mashed potato na scrambled egg kwa kuli au mwanafunzi eti lunch au breakfast inakuja kweli?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom