Shindano la big brother lina maudhui gani?

Missy Gf

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2022
Posts
5,441
Reaction score
15,201
Naomba kujua kuhusu hili shindano la BIG BROTHER. Yaani huwa sielewagi watu wanashindanishwa nini na mshindi anapatikanaje.

Kila nikiingia kwenye hiyo channel naona vijana wadogo wamefungiwa mahali wanakula bata humo ndani halafu baadae anatangazwa mshindi.

Kuna watu hawalali, wakifatilia hili shindano... Sasa mimi sijui ni ushamba au nini sielewagi kabisaaa

Hili shindano Lina maadili gani pia kwa Hao washiriki na watazamaji maana naona kuna muda washiriki wanafanya sex usiku au kwenye swimming pool.

Hebu naomba leo mnitoe ushamba jamani...
 
Wanaofatilia BIG BROTHER wanajikutaga wa kishua sana 🀣🀣🀣
Kuna mshikaji mmoja natamani nimtag aje atoe neno hapa maana kukiwa na BB siku hiyo mkizubaa hakuna kitakachoendelea kisa anaangalia show.

Maudhui yake nadhani, mbali na kuburudisha hasa katika kizazi hiki kinachoabudu celebrities hata kama hawana kipaji cho chote, ni kuonyesha ushindani; na hasa undumilakuwili na unafiki wa binadamu maana mule hakuna kuaminiana. Hata mtu mnayenyanduana naye anaweza kukugeuka wakati wo wote na kukuleftisha.

Ni show isiyoeleweka hasa katika uwasilishaji wake wa maudhui japo inapendwa sana na vijana wa kizazi kipya wanaotafuta mashujaa wapya na role models katika maisha yao.
 
Kuna mshikaji mmoja natamani nimtag aje atoe neno hapa maana kukiwa na BB siku hiyo mkizubaa hamli chakula kisa anaangalia show...
Mi nilipenda sana maisha plus ila hiyo big brother watu wanafanya vitu vya hovyo kabisa.

Wanapima vitu kibao kama sex intention yaani ile watu wanaoga pamoja wote wapo uchi, lakini eti mwanaume asione tamaa ila wengine wananyanduana wanashindwa na wanakosa point za kuendelea yaani hovyo sielewi.
 
Binafsi imenishinda hata nikijaribu kufit-in na wenzangu niingalie naona sitoboi naachana nayo.

Kuna show ya Netflix inaitwa The Circle.

Mi nimeifuatilia na kuipenda, inahusiana na namna ambavyo unaweza kumanipulate watu kupata influence ya mapenzi/urafiki/uongozi ukiwa nyuma ya keybord.

Unachagua profile unaweka iwe ya uongo au ya ukweli.
 
I Iyo big brother ipo king'amuzi gani na inarushw channel gan ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…