Kuna mshikaji mmoja natamani nimtag aje atoe neno hapa maana kukiwa na BB siku hiyo mkizubaa hakuna kitakachoendelea kisa anaangalia show.
Maudhui yake nadhani, mbali na kuburudisha hasa katika kizazi hiki kinachoabudu celebrities hata kama hawana kipaji cho chote, ni kuonyesha ushindani; na hasa undumilakuwili na unafiki wa binadamu maana mule hakuna kuaminiana. Hata mtu mnayenyanduana naye anaweza kukugeuka wakati wo wote na kukuleftisha.
Ni show isiyoeleweka hasa katika uwasilishaji wake wa maudhui japo inapendwa sana na vijana wa kizazi kipya wanaotafuta mashujaa wapya na role models katika maisha yao.