Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change 2022)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change 2022)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
SOC 2022 (1).png

SOC 2022 (2).png
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 15, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 15, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.

ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.

Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 116
Tayari nimeshaweka andiko langu
1) sera za kodi ba ushuru zinavyozoretesha ukuaji wa uchumi
2) Mitaala ya elimu ni chanzo cha vijana wengi kuwa maskini

Naombeni ushiriki wenu kwenye mijada hii km umeipenda naomba kura yako
Ukisha andika unatuma wapi?
 
TAALUMA YA NDOTO YAKO.

Kutambua taaluma yako ni jambo la muhimu wakati ukiwa shuleni. Hasa wakati ukiwa sekondari kwenda chuo. Kipindi hiki ni muhimu zaidi, kwa sababu ni wakati ambao mwanafunzi hufanya maamuzi yanayoathiri maisha yake kitaaluma.

Hata hivyo, wengi tunajua kwa kiasi kidogo sana kuhusiana na chaguzi za taaluma wakati tukiwa shuleni. Wengi tunaenda vyuoni kusoma kozi fulani kwa sababu mama au baba kasoma. Au jamii inasema nini kwa wakati huo. Kuweza kutambua taaluma yako mapema huweza kukusaidia mwanafunzi kupenda kujifunza, kusoma kwa bidii na kukua kitaaluma kutokana na kuzingatia misingi sahihi. Ni kichocheo kuelekea kufikia maisha ya taaluma ya ndoto yako. Humsaidia mwanafunzi kupima wapi anahitaji kuwa katika mipango yake ya kazi na jinsi gani anaweza kufikia malengo hayo. Maisha yana fursa nyingi ikiwa umetambua taaluma inayoendana na uwezo wako. Unaweza kufanya mambo makubwa kwa njia nyepesi kabisa. Kwa sababu iko ndani ya uwezo wako.

Chukua muda wa kujiweka katika nafasi ya kuingia katika uwanja maalum wa taaluma ya ndoto yako. Kwa kufikiria kwa upana hatima ya taaluma ya ndoto ya maisha yako. Mahali ulipo sasa hivi, ni hatua moja tu kwenye safari hii ndefu inayoiitwa maisha. Na uko katika hatua moja maalum lakini sio mwisho. Kuna upande mwingine haujauona bado. Kuna njia ambayo imewekwa mbele yako, ambayo bado haujaikanyaga. Kwa hivyo, usishawishike kuja au kufanya kazi fulani kwa sababu ya mshahara mzuri au kile ambacho jamii inasema au kuwa kama mtu mwingine. Unaweza kupata mkwamo katika kazi au taaluma uliyochagua. Kimbia mbio zako. Usijaribu kujilinganisha na wengine. Kinachofaa kwa mtu mmoja kinaweza kuwa ndicho kitakachokuua. Zingatia karama ulizopewa na Mungu na usiwe na wivu kwa baraka alizowapa wengine. Kila mtu ana eneo lake ambapo anaweza kufanya vizuri, itafute karama yako na kujenga juu yake.

Mwanafunzi lazima aimarishe ujuzi wake ili aweze kufanya maamuzi sahihi sehemu ambapo hapana maelezo ya kutosha. Na aweze kufahamu vitu anavyovithamini na uwezo wake wa kitaaluma, ili kuondokana na utata wakati wa uteuzi wa taaluma ya ndoto ya maisha yake. Fanya uchunguzi wako ili uweze kuelewa kwa uwazi taaluma inayoendana na vitu unavyovithamini, sambamaba na uwezo wako. Pangilia ufaulu wako kwa uangalifu. Japokuwa ufaulu wa darasani pekee hautoshi. Hivyo basi, lazima ujiandae kwa ajili ya kuingia katika taaluma ya maisha yako. Anza kwa kukuza mtandao wako wa kitaaluma. Kwa mfano, jiunge na vilabu vya wanafunzi katika taaluma ya kazi unayoipenda. Hudhuria darasa lenye kuzungumzia mambo ya taaluma ya kazi unayoipenda. Zungumza na mwalimu wako wa taaluma. Au mzungumzaji mtaalamu aliyealikwa katika hafla maalum ya kitaaluma, na ujifunze zaidi jinsi ya kujikita katika nyanja mahususi ya taaluma yako. Na kuelewa kozi ambazo unaweza kuzisoma kutokana na ufaulu wako. Kitabu cha Mwongozo cha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kinaweza kukusaidia kukupa mrejesho mzuri kuelekea taaluma ya ndoto yako.

Kumbuka vile vitu unavyovithamini ndivyo kitovu cha maamuzi yako. Thamani ni kitu cha kimsingi ambacho unadhani ni muhimu. Vitu unavyovithamini ni kipimo ambacho unaweza kutumia kutathmini ikiwa maisha yako yanaenda vile unavyotaka. Kukumbuka kile ambacho ni muhimu kwako kitakusaidia katika mchakato wa kufanya maamuzi na kukusaidia kupata ufafanuzi juu ya kile unachotaka. Kwa mfano, ikiwa unathamini muda wa kuwa nyumbani na watoto wako, basi huenda usingependa kuchukua kazi inayohitaji kusafiri sana. Zaidi ya hayo, unaweza kujifunza zaidi au kutafiti taaluma ya chaguo lako moja kwa moja kutoka kwa mfanyakazi wa taasisi unayemwamini. Kazi kivuli au kujitolea ni njia nyingine muhimu ya kujua kuhusu kazi fulani. Ili kuelewa mahitaji ya kazi unayoipenda katika soko la ajira, ujuzi unaohitajika kutekeleza majukumu ya kazi, sanaa za watu fulani katika jamii (utamaduni) kama unaweza kuendana nazo kulingana na vitu unavyovithamini, uwezo na maslahi yako.

Chukua muda wakati wa tathmini yako ili kusikiliza sauti ya ndani yako na jaribu mbinu za mawazo yako na maamuzi yako dhidi ya uzoefu ulionao. Jiulize, maisha yako bora ungependa yangekuwaje, ikiwa ungeweza kuwa na chochote unachotaka, au ikiwa ungeweza kufanya chochote unachotaka? Unapoamka asubuhi na kufungua macho yako, ungependa kunaona nini? Unajisikiaje? Unapoamka asubuhi siku yako ungependa iweje? Ungependa kwenda wapi? Nini ungependa kuona? Nani ungependa awe karibu nawe? Nini ungependa kufanya? Unahisi nini ukiwa unafanya hiyo kazi? Hili ni jambo kubwa zaidi, hakikisha unajumuisha maswali haya yote katika kufahamu taaluma ya ndoto yako. Chora picha ya taaluma unayoipenda. Paka rangi yake vizuri. Ifanye iwe ya rangi uipendayo. Ielezee siku yako vizuri vile ungependa iwe, kwa maelezo ya kutosha kwa kujiuliza maswali hapo juu. Baada ya muda kutaanza kubadilika kwa baadhi ya mambo ndani yako. Itakusaidia kukuongoza kutoka katika mitazamo ya ndani namna ya kufanya mambo, kutaka vitu na fursa ambazo pengine hungekuwa nazo hapo awali. Kwa hiyo, fikiri chaguo za taaluma ambazo zinazoendana na vitu unavyovijali pamoja na uwezo wako. unaweza kuziorodhesha na kuziondoa kwa kutumia mchakato wa kuondoa moja baada ya nyingine hadi upate taaluma ambayo uipendayo kwa kuzingatia vitu unavyovithamini, uwezo na maono yako.

Mpango wa Mungu kwa kila mwanadamu ni maisha bora yenye amani, wingi kuridhika na upendo. Maono yangu unaposoma andiko hili ni kwamba, lichochee kile kilichomo ndani yako, na kukufanya uchukue hatua kuelekea mpango mkuu ulionao kwa ajili ya maisha yako. Siku zote uwezo wetu wa kufanya maamuzi ndiyo unaoweza kujenga au kubomoa maisha yetu. Nakutakia kila heri kwenye maamuzi sahihi ya taaluma ya ndoto yako.


Mwandishi:
Endobile Herman.
Mawasiliano:
Namba ya Simu: 0754015554/0675098447
 
View attachment 2291152
View attachment 2291153
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 14, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:

Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 14, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.

ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.

Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Mawasiliano

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
Opportunity nzuri sana hiyo
 
SERIKALI INATAKIWA KUA NA MIPANGO ENDELEVU NA KAMILIFU .
Kwa miaka mingi tumeshuhudia kila kiongozi anapoingia madarakani huja na mipango yake na namna ya utekerezaji wake.inasikitisha Sana kuona hata pale anapokuta kuna miradi ilianzishwa na watangulizi wake lakini tunashuhudia mingine haikamiliki,je hatuoni kwamba tunapoteza pesa ambazo zingetumika kuimalizia ile miradi ambayo ilishanzishwa bila kumalizika?

Je hatuoni kwamba hii inaleta taswira mbaya kwa wale wanaotusaidia kea namna Mona au nyingine?

Je nini kifanyike ,tunapaswa kusimama imara ili kuhakikisha yale tuliyoanza na yo yanakamilika ndo tunakuja namipango ya miradi mingine maana kutofanya hivyo nisawa tunaenda mbele alafu tunarudi nyuma kuanza upya.

Viongozi wajuu wanapaswa kuangalia wasaidizi wanaoteuliwa wawe msaada wakweli kwao na sio wakuadanganya kwakutaka kuonekana wanafanya kazi nzuri mbele za wakubwa sao.

Pamekua nakasumba ya wasaidizi waviongozi wajuu kua watu wababaifu na wasiosema ukweli kwa viongozi waliowateua ili wawasaidie majukumu katika sehemu mbalimbali.

Wasaidizi wengi wamekua niwatu wakujikweza na kujipamba badala yakufanya kazi yakuhudumia wananchi Kama wanavyoagizwa na viongozi waliowateua.

Yanahitajika mageuzi makubwa kea viongozi wasaidizi wanamna hii kuwajibishwa pasipo kuoneana aibu maana wamechaguliwa ah wameteuliwa kwenda kuwahudumia wananchi.

Ni Mimi wen u@Steven mpangala 0672367780
 
MWANDISHI: MAKI D SILWIMBA
Mawasiliano:0745265780
MAADA:TISHIO LA USUGU WA DAWA NA UANDAAJWI WA MATABIBU WAJAO KATIKA KUKABILIANA NA TATIZO NCHINI TANZANIA.

Ustahimilivu wa viuavijidudu (usugu wa dawa) hutokea wakati bakteria, vimelea, virusi na fangasi wanapokuwa sugu kwa dawa . Upinzani dhidi ya viuavijasumu (dawa zinazotumika kuzuia na kutibu maambukizi ya bakteria) ni tatizo la dharura kwa sababu antibiotics ni msingi wa dawa za kisasa na taratibu nyingi za matibabu katika afya ya binadamu na wanyama hutegemea dawa hizi.
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasisitiza kwamba "usugu wa dawa ni moja ya hatari kubwa kwa usalama wa chakula, maendeleo, na afya ya ulimwengu leo." Kuenea kwa bakteria sugu kumeongezeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya viuavijasumu(dawa) katika matibabu ya binadamu na kilimo kote ulimwenguni. Mojawapo ya sababu kuu zinazochangia kuundwa kwa bakteria sugu ni taarifa zizizo sahihi na/au matumizi mabaya ya dawa kwa wagonjwa.
Usugu wa dawa unazidi kuleta wasiwasi mkubwa, na hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika mataifa yanayoendelea kutokana na matumizi mabaya ya madawa. Matumizi ya dawa isivyotakiwa, yanachangia kuibuka kwa usugu; Upatikanaji wa dawa za kuua viini kwenye kaunta(kiurahisi), bila agizo la daktari, na kupitia mitandao ya usambazaji isiyodhibitiwa inachochea zaidi matumizi yawe yasiyo faa katika mataifa yanayoendelea.

BAADHI YA SABABU ZINAZOCHANGIA ONGEZEKO LA TATIZO
Wasambazaji wa dawa na ubora wa dawa
Upatikanaji na matumizi mabaya ya dawa za kuua viini pia huathiriwa na ukosefu wa sheria madhubuti zinazosimamia mauzo yao. Dawa za kuua viini kwa kawaida zinaweza kununuliwa bila agizo la daktari katika mataifa maskini na kwa kawaida hutolewa na watu wasio na ujuzi mitaani. Wauzaji hawa wa dawa watauza dawa ili kupata mapato na kutosheleza mahitaji ya kifedha ya mgonjwa.

Wataalamu wa afya
Wataalamu wa afya ni muhimu katika utambuzi, matibabu, na kuzuia magonjwa, lakini wana hatari ya kuhatarisha juhudi hizi ikiwa mbinu zao hazitaungwa mkono na utafiti. Katika mataifa mengi yanayoendelea, kuna uwiano wa juu wa mgonjwa na daktari, jambo ambalo huwafanya madaktari kufanya kazi kupita kiasi na kutompa muda wa kumuelekeza mgonjwa kuhusu viwango vya ufuasi wa dawa na athari za kutofuata utaratibu wa kutumia dawa.


Wagonjwa
Uzingatiaji una changia sehemu kubwa katika ukuaji wa usugu wa dawa. Wagonjwa wanaweza kukosa dozi kwa makusudi au bila kukusudia. Baadhi ya wagonjwa wanaweza kuruka dozi wanapoalikwa kwenye karamu inayohusisha unywaji pombe kwa sababu wanafahamu madhara ya kufanya hivyo wanapotumia dawa. Taratibu hizi huweka bakteria hai kwenye viwango vya dawa chini ya viwango vya matibabu, jambo ambalo huongeza uwezekano kwamba wanaweza kupata usugu wa dawa.

Matumizi yasiyo ya binadamu ya dawa
Utumiaji wa dawa za kuua vijidudu kwa wanyama, haswa zile zinazotumika kwa uzalishaji wa chakula, una athari kubwa kwa afya ya binadamu na wanyama kwani inaweza kusababisha kuibuka kwa bakteria sugu kwa matibabu. Bakteria hawa sugu katika wanyama wanaweza kuenea kwa binadamu kwa njia ya chakula, kuwasiliana kwa karibu na wanyama wanaotumiwa kwa chakula, au usambazaji wa mazingira (kama vile maji taka kutoka kwa watu na kutiririka kutoka kwenye maeneo ya kilimo.

Ufuatiliaji duni na upimaji mdogo katika maabara.
Kutokana na matatizo ya uwezo, upimaji wa uwezekano wa antimicrobial haufanywi mara kwa mara katika maabara nyingi za vijijini. Kwa sababu viwango vya upinzani vinaweza kubadilika kwa wakati katika eneo moja la nchi, ufuatiliaji kama huo lazima ufanyike mara kwa mara na bila kukoma.

MIKAKATI YA KUDHIBITI UKUAJI WA TATIZO LA DAWA SUGU
Ukweli kwamba mashirika mengi ya kimataifa ya dawa huona kufanya utafiti juu ya usugu wa dawakama "faida ndogo" kwa hivyo, wanapendelea ufadhili wa uundaji wa dawa za magonjwa sugu kama vile kisukari na shinikizo la damu pamoja na zile zinazosaidia watu kuishi maisha yenye afya kama vile Cialis na Viagra. Kufanya tafiti, na kuja na njia bora za kuzuia maambukizi ya viumbe sugu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine lazima iwe lengo la msingi la ufumbuzi wa muda mrefu.

Jukumu la wadau katika udhibiti wa usugu wa dawa
Wataalamu wa matibabu na wanasayansi hawawezi kuwajibika pekee yao kudhibiti usugu wa dawa. Umma kwa ujumla na washikadau wengine wana jukumu muhimu la kutekeleza, mambo kama elimu ya mara kwa mara ni muhimu katika kutatua tatizo hili. Serikali pia inapaswa kuyapa kipaumbele masuala ya afya ya umma yanayohusiana na usugu wa dawa(1).

Jukumu la mashirika ya udhibiti serikalini
Ili kuhakikisha usugu wa dawa unapungua katika vituo vyote vya huduma za afya, kilimo, na sekta ya mifugo, utafiti mkubwa na unaoendelea, sera, sheria na maendeleo zinahitajika ili kutatua tatizo la usugu wa dawa na kuajiri madaktari zaidi ili kuleta uwiano sawa kati ya idadi ya wagonjwa na madaktari.

MATABIBU WA BAADAE NA TISHIO LA USUGU WA DAWA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Dodoma, asilimia 48.8 ya wanafunzi wanaosoma udaktari wa binadam na 27.3% ya wanafunzi wa kada zingine hawakumaliza kozi nzima inayohusu usugu wa dawa na waliacha kutumia dawa mara pale dalili za ugonjwa zinapopungua.
Kwa kuwa watakuwa wakitoa dawa kila siku bila uangalizi mara tu watakapohitimu na kupewa leseni ya udaktari, wanafunzi wa kitiba wanahitaji kujifunza jinsi ya kutoa dawa kwa usalama na kwa ufanisi. Ikizingatiwa kwamba wanafunzi wa siku za usoni wa utabibu watatumika kama kizazi kijacho cha watoa huduma za afya, ni muhimu kwamba waelezwe kikamilifu kuhusu tatizo linaloongezeka la usugu wa dawa. Kwa bahati mbaya, ni sehemu ndogo tu ya mitaala ya wanafunzi wa udaktari wa Tanzania ambayo inasisitiza juu ya usugu wa dawa, na hakuna taarifa za ASP hata kidogo. ASPs huwaelimisha watumishi wote muhimu wa mfumo wa huduma ya afya, wakiwemo madaktari, wafamasia, na wauguzi, kuhusu umuhimu wa kuzingatia maagizo ya utumizi wa dawa ili kuzuia matumizi yasiyo yasiyo faa ya viuavijasumu.

HITIMISHO
Malengo ya kujifunza yanayohusisha viuavijasumu na usugu wa dawa yanapaswa kujumuishwa katika uundaji upya wa mtaala wa kitaifa wa shule za msingi na sekondari. Katika vyuo vya tiba lazima kuwe na kozi maalum kuhusu usugu wa dawa. Kwa ujumla, ni kazi yetu kuzuia kueneza vijiumbe hai ambayo ni sugu kwa kizazi kijacho.


TUUNGANE KUDHIBITI USUGU WA DAWA….INAWEZEKANA KWA USHIRIKIANO WA ASASI ZA KIRAIA NA ZISIZO ZA KIRAIA.
 
SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Habari za wakati huu, kama ambavyo tunavyojua vitu hivi viwili vinafuatana kulingana jinsi vilivyo sayansi ni elimu itolewayo kuhusu maendeleo ya kidunia na teknolojia ndio mfumo mzima wa matumizi ya vifaa vinavyorahisisha kazi ambayo huenda ingechukua muda mrefu kuifanya,katika kuchochea maendeleo kupitia sayansi na teknolojia chukulia zama zile ili mlazimu mtu kutembea umbali mrefu lakini kwa sasa baada ya teknoljia kukua imeweza kurahisisha usafiri wa eneo husika la kijografia kufikia kwa urahisi hii ikimaanisha kupitia barabara,anga,majini na hata kwa reli,katika hili la imeweza kusaidia kilimo kwa maana ya kwamba haimlazimu mkulima kutumia muda mrefu kupitia uandaaji wa mashamba na hata kilimo kwa ujumla,imesaidia pia vifaa vya kimawasiliano kwa maana ya simu,kompyuta mpakato ili kurahisishia kupitia elimu[kwa kufundushia],afya kwa,ajili ya ajili kwa maana ya kutumia mashine za kiutabibu,vile vile hata pia kuchochea suala la ungozi kupitia mashine saidizi kwa maana ya gari kwa kiongozi kufika katika eneo husika ili kutatua kero kubwa kwa wananchi na kwa wakati sahihi,pia kuna suala la maendeleo ya kibenki na miamala ya simu hii imemgusa kila mtu kwa namna ya kiurahisi wa matumizi mnufaika ni serikali na mwananchi wa kawaida
 
UKOSEFU WA ELIMU.
Suala la elimu kwa jamii ya watanzania ni swala ambalo halipo kama linavyotazamwa na serikali na jamii kwa ujumla. Sehemu kubwa ya jamii bado haijakombolewa kutoka katika zile imani potofu zinazoletwa na mila na tamaduni za jamii, tunaweza kuweka takwimu wazi lakini tafiti nyepesi zinaonyesha kuwa bado jamii haijakombolewa kwa sehemu kubwa. Kuna matendo ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unaendelea katika jamii zetu, lakini kwa leo tuzungumzie haswa juu ya suala la ukeketaji kwa mwanamke.
Kile kiwango ambacho serikali na jamii kwa ujumla inahisi kwamba elimu imeikomboa jamii sio kweli kwamba elimu imekomboa jamii kwa kiwango hicho, Katika tafiti nyepesi na matendo tunayoyaona katika jamii zetu suala la ukeketaji bado linaendelea kwa kiasi kikubwa sana tena katika zile jamii ambazo hazijategemewa kama suala kama hilo linaweza kutendeka. Jamii inapatikana pembezoni kidogo sana mwa jiji lakini masuala ya ukeketaji bado yanaendelea kwa kiasi kikubwa sana japo kwa siri.
 
MATUMIZI YA BANGI JIJINI ARUSHA
Ni miaka mingi sasa tangu jiji la Arusha nchini Tanzania kuwa maarufu kwa matumizi haramu ya bangi. Ni kweli kwamba jiji hili linaongoza kwa matumizi haramu ya bangi na jamii kubwa iliyoathirika ni vijana na watoto. Kutokana na uzoefu wangu wanafunzi wa kwanzia darasa la nne huanza matumizi ya bangi kwa siri pasipo wazazi kufahamu na imeleta athari kubwa sana kwa watoto na vijana. Matumizi ya bangi yamekua ni nyenzo kubwa sana katika kuharibu nguvu kazi katika jiji hili kwani imesababisha idadi kubwa ya vijana kuachana na masomo na kujiunga na makundi ya mtaani ya watumiaji wa bangi na hatimaye kuongeza uhalifu mtaani kama vile wizi, ubakaji na mengine mengi, matumizi haya yamebadilika kuwa ni utamaduni kwa vijana wanaozaliwa katika jiji hili, kila kijana anayezaliwa katika jiji hili utamaduni mkubwa uliopo ni kuvuta bangi.
-qq5x9d.jpg
-qq5x9d.jpg-qq5x9d.jpg
-qq5x9d.jpg



Hili suala linahitaji hatua muhimu za serikali na jamii kwa ujumla haraka iwezekanavyo ili kuokoa jamii kubwa ya vijana inayoteketea, miongoni mwa hatua ambazo serikali na jamii inaweza kuchukua
Kwaanza ni kutafuta na kuharibu vyanzo vya bangi katika jiji hili kwani bangi ni zao na linalimwa kiharamu pembezoni mwa jiji hili hivyo jamii na serikali visaidiane katika kuharibu vyanzo vyote vya bangi katika jiji hili.
Pili kutoa elimu pamoja na kuweka sheria ngumu kwa vijana ikiwemo kuharibu vijiwe, kukamata vijana wasiojukumika lakini pia wanafunzi wote wapangiwe kusoma shule za bweni ama nje ya mkoa
Kwa kuhitimisha tu, Hadi sasa jamii kubwa sana ya vijana imekwisha haribika katika jiji hili la Arusha.
 
Ushinde halafu uwe verified kwa 200K!

Hii ni sooo mazee.

Yule binti aliyeshinda shindano la "China Made" toka wamtundike (baadae walifuta) kwenye page ya Jf kule Instagram naona hata hiyo ID imepotea sana humu.

Fungueni IDs mpya otherwise ni fedheha ukishinda hasa wale akina Dully Sykes wazee wa bragging.
 
Jaman naomba kuuliza...wapi naclick kwa ajili ya kuandika story of change....
 
Sote tushikane mkono kuelekea mafanikio.... Andiko NGAZI ILIYOACHWA NA VIJANA" andiko linaloweza kubadili maisha ya mtu fulani kwa kiasi kikubwa katika nyanja mbali mbali: twende tukasome tafadhali kisha tupigie kura.
Ukiweza share na watu wengine wapate maarifa.
 
Back
Top Bottom